Hatari ya kuvalia viatu bila soksi
Wanaume wengi katika maonesho ya mitindo pia mara nyingi huonesha mavazi wakiwa na viatu bila soksi.Mwanamuziki Tinie Tempah amejishindia tuzo nyingi kwa sababu ya mitindo na mara nyingi katika maonesho ya mitindo ya Londo huketi viti vya mbele.Yeye pia huwa mara nyingi havai soksi – lakini anafahamu madhara yake? “Miguu ya binadamu kwa kawaida hutoa nusu painti (ambayo ni sawa na lita 0.28) ya jasho kila siku,” Emma Stephenson anasema.”Unyevu mwingi na joto unaweza kusababisha maambukizi ya maradhi yanayotokana na kuvu mfano ugonjwa unaosababisha mwasho na kuchubuka kwa ngozi (kwa Kiingereza athlete’s foot).
Moja ya visa vibaya nilivyowahi kukumbana navyo ni cha mwanamume mmoja wa miaka 19 aliyefanya kazi ya kuosha magari. Miguu yake ilikuwa inatokwa na jasho sana na ilikuwa imechubuka sana.” Lakini bila shaka itachukua ujasiri kumwambia bingwa wa UFC Conor McGregor kwamba anaweza kupata matatizo kutokana na mtindo wake wa kuvalia viatu. Emma anashauri kwamba siri ni kutozidisha, iwapo bado utataka kutovalia soksi. Jaribu usivae viatu bila soksi kwa muda mrefu. Jaribu pia kuweka kitu cha kukausha jasho kwenye soli ya kiatu chako kabla ya kukivalia bila soksi. Kadhalika, kuwa makini kuchunguza miguu yako. Ukigundua unaumwa pahali tafuta usaidizi upesi.
Comments
Post a Comment