Nape Apigilia Msumari Kauli ya Msekwa Kuhusu Ukomo wa Madaraka kwa Rais
MBUNGE wa jimbo la Mtama, Mh Nape
Nnauye amepigilia msumari kauli iliyotolewa na Spika wa zamani wa Bunge,
Pius Msekwa kuhusu miaka ya uongozi na kusema misimamo hiyo ndiyo
misimamo ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwalimu Julius Nyerere.
Nape Nnauye ameweka video ya Pius
Msekwa akielezea juu ya ukomo wa kiongozi madarakani na kusema chama
hicho kilishafikiria miaka ya nyuma kuongeza miaka kutoka 10 na
kuendelea lakini waliona miaka kumi inatosha kwa mtu kuongoza na
kusisitiza ikiwa miaka 15 ikatokea mkapata kiongozi mbaya miaka hiyo
itakuwa ni mingi sana.
“Miaka 15 mkipata kiongozi mbaya ni
mingi sana, nashauri ibaki miaka 10 kama kiongozi ni mbaya angalau
tumvumilie kwa miaka 10 tu halafu basi ndivyo hoja ya miaka 10
ilivyopita si kama hiyo mingine hatukufikiri ilifikiriwa ndiyo maana
naposikia kuna Mbunge mmoja anataka kupendekeza twende kwenye miaka saba
kwa vipindi viwili ninataka kumjulisha kwamba hili si wazo jipya
tulishafikiri na lilikataliwa kwa hiyo mimi na imani CCM itaendelea
kulikataa hilo, tutabaki kwenye miaka mitano tu mara mbili basi”
alisisitiza Msekwa
Kufuatia kauli hiyo ndipo Nape Nnauye
alipigiria msumari na kusema hicho ndicho Chama Cha Mapinduzi (CCM) cha
Mwalimu Julius Nyerere anachokijua yeye.
Siku za karibuni Mbunge wa Chemba
(CCM), Juma Nkamia alidai anataka kupeleka hoja bungeni kuongeza muda wa
utawala hadi miaka 7 badala ya miaka mitano ya sasa.
Comments
Post a Comment