Posts

Wolper Anapozomeana na Kivuli Chake

Image
Jacqueline Wolper Massawe, aliye pia na a.k.a nyingi zikiwemo za Gambe na Amber Rose wa Bongo. MIONGONI mwa waigizaji wa kike niliowahi kufanya naye kazi kwa kipindi kirefu na kwa ukaribu zaidi ni pamoja na mrembo Jacqueline  Wolper Massawe, aliye pia na a.k.a nyingi zikiwemo za Gambe na Amber Rose wa Bongo. Mkononi nimefumbata miaka saba sawa tangu nianze kazi ya uandishi wa habari, kwenye magazeti haya pendwa. Ninao uzoefu mkubwa kwa kuwafahamu watu wengi maarufu kwa maana ya maisha yao ndani na nje ya kazi zao, nawajua sana hususan wasanii wa filamu ambao nafanya nao kazi mara kwa mara. Hata wengi wao wananijua vyema , kwenye eneo la kazi kwamba huwa siruki sentensi kwenye kuanika ukweli. Hivi karibuni, Wolper alikaririwa na mmoja wa waandishi wenzangu akisema kitendo cha kumshika na kumbeba mtoto wa mwigizaji mwenzake, Faiza Ally kimemuondolea gundu ya kutopata mtoto hivyo na yeye kutarajia kupata wa kwake mwakani. Sawa, Wolper yuko sahihi lakini mbona m

FAIZA ALLY AJITOSA SAKATA LA DIAMOND PLATINUMZ NA ZARI THE BOSS LADY,AFUNGUKA LIVE

Image
Huku Tetesi na Stori kibao zikikamata headlines mitandaoni kuwa couple ya @diamondplatnumz Na mama watoto wake @zarithebosslady SASA IMEBAKI STORI, Faiza Ameandika ujumbe Huu :. By @faizaally_ – Diamond kijana mdogo sana anahitaji ku have funny na watoto wenzie na sisi wa dada watu wazima tuangalie watu wa kutoka nao… Go baba and have funny enjoy the world ndio useto down …. jiachie uwe huru ikibidi usiwe na mahusiano , bado hujaiona dunia hata robo, we ni star , hela ipo there is lot to see…nasema with clean heart no hate kwa zari au kwa yoyote , nimezurula sana duniani kabla ya kuzaa na kutulia…jiachie life is today buana

Taarifa Muhimu ya TCU kwa Wanafunzi Waliokosa Vyuo

Image
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa  awamu ya kwanza ya Udahili wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ulimalizika tarehe 30 Agosti 2017. Tume inawaarifu kuwa imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji wote walioomba kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo wa 2017/18. Hata hivyo kutokana na  waombaji wengi  kutochaguliwa  kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 4 hadi 10 Octoba 2017 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili: •  Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza; •  Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika  awamu ya kwanza; •  Waombaji wenye vigezo vya Stashahada  walioshindwa kupata Namba ya Uhakiki wa Tuzo (AVN); •  Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge”  mwaka 2017 na matokeo yao yameshatoka; na •  Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitsho toka vyuo vy

PENZI LA ZARI THE BOSS LADY NA DIAMOND PLATINUMZ LAYUMBA VIBAYA

Image
  Ule uhusiano maarufu zaidi Afrika Mashariki wa Diamond Platnumz na Zarina Hassan inaelekea upo katika hatua mbaya ya uhai wake kutokana na yanayoendelea katika mitandao ya kijamii. Katika kipindi cha miezi miwili uhusiano huo umepamba vichwa vya habari kabla na baada ya Diamond kukiri kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto. Hata hivyo, baada ya sekeseke hilo kupita ilionekana huenda hali imekuwa shwari hasa baada ya Diamond kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa Zari, Septemba 23 mwaka huu nchini Afrika Kusini. Inavyoonekana moto unafukuta ndani kwa ndani kwani tangu juzi wapendanao hao wamekuwa wakifuta picha zao za pamoja katika akaunti zao za Instagram. Pamoja na kufuta picha, Zari anaonekana kurusha vijembe katika mtandao wa Snapchat akisema hawezi kufanywa mjinga katika mitandao ya kijamii. Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa Diamond, mashabiki walisubiri kwa hamu kuona atakachoandika Zari kama ilivyo kawaida yake lakini ilipita kimya. Wengi wametafsiri kuwa pamoja na

IGP Sirro Kuhusu Miili Iliyookotwa Coco Beach

Image
IGP Simon Sirro. MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amesema wameunda timu ya wataalamu kuchunguza miili iliyookotwa na sampuli kutoka miili hiyo zimechukuliwa. Amesema iwapo kuna watu ambao ndugu zao wamepotea ni vyema wakafika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya vipimo na kufanyika upelelezi. “Bahari ni kubwa inapita katika nchi nyingi na inachukua kila kitu, haya mambo yanapotokea hata nchi nyingine yanatokea, kwa hiyo kimsingi tumeunda timu ya wataalamu ya kupeleleza kuhusu miili hii, wamechukua majimaji kutoka mwilini,” alisema. IGP Sirro alisema, “Kama kuna mtu ambaye ndugu yake amepotea afike makao makuu ya Polisi upande wa DCI tuweze kufanya uchunguzi kuona kama ni ndugu yake.” Alisema miili hiyo haijabainika kuwa ni ya watu wa Taifa gani. “Tatizo letu Watanzania ni kwamba moja kwa moja wanaanza kuhisi, sijui kwa nini tunakuwa tunaishi kwa hisia na hii hisia hisia si nzuri, tuseme kitu tukiwa na uhakik

ACT- WAMJIBU RAIS MAGUFULI ISHU YA KUTOONGEZA MISHAHARA

Image
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, akizungumza na  waandishi wa habari. CHAMA cha Act-Wazalendo kimesikitishwa  na kauli ya Rais Magufuli aliyoitoa jana kwenye ufunguzi wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) kuhusu mishahara ya wafanyakazi aliposema  alipoingia madarakani hakusema ataongeza mishahara kwa vile hakuchaguliwa kuongeza mishahara na kwamba ana jukumu la kuwahudumia wananchi. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ACT Wazalendo,  Ado Shaibu, alisema: “Swali la kujiuliza baada ya kauli hiyo ni, je, wafanyakazi wa Tanzania wanastahili kufanyiwa hivi na serikali wanayoihudumia? Jibu bila shaka ni hapana.  Serikali inatoa wapi ujeuri wa namna hii dhidi ya wafanyakazi nchini wakati kiuzalishaji na kimapato inawategemea wafanyakazi? “Licha ya mchango wao madhubuti katika ujenzi wa taifa kwenye sekta mbalimbali, kwa utumishi wao wa kutukuka, ukweli wa mambo ni kuwa wafan

NASSARI: Maisha Yangu Yapo Kwenye Bonde la Uvuli wa Mauti

Image
Nassari na Lema. MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA) Joshua Nassari amefunguka na kusema maisha yake yapo hatarini na kudai kuwa watu ambao amewaanika kwenye sakata la ununuzi wa madiwani wanamtafuta. Nassari amesema hayo ikiwa imepita siku moja toka alipokwenda kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupeleka ushahidi wake juu ya madiwani wa CHADEMA waliohama chama kwa kuhongwa rushwa na wateule wa Rais John Pombe Magufuli. “Maisha yangu yapo kwenye bonde la uvuli wa mauti, Maisha yangu yapo hatarini kwani Watesi wetu wananitafuta” aliandika Nassari kupitia ukurasa wake wa Facebook. Mbali na hilo wachangiaji mbalimbali kwenye ukurasa wa Mbunge huyo walimtaka azidi kumuomba Mungu huku wakimshauri kuongeza ulinzi zaidi katika maisha yake ya kila siku kutokana na jambo ambalo ameliibua na kumtaka aendelee kupambana, baadhi ya wachangiaji wengine wamedai kuwa anachofanya ni njia ya kujitafutia umaarufu kisiasa. Juzi  Mbung

Rais Magufuli Amwagia Sifa Makonda..Adai Hata Kama Hajui Kusoma Lakini Kama Anashika Madawa ya Kulevya Kwake ni Msomi Mzuri

Image
        Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemsifia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kupambana vita dhidi ya dawa za kulevya aliyoianzisha huku akitaka viongozi wengine kuiga mfano wa kiongozi huyo . Rais Magufuli amesema hayo kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam ambapo amemtaka Waziri mkuu, Kassim Majaliwa kuwaambie wakuu wa Mikoa wengine kujifunza kwa Makonda. “RC wa Dar es salaam alipojaribu kusema kuhusu dawa za kulevya kelele zikawa nyingi kweli, mara ooh hajasoma. Mimi hata kama hajui ‘a’ lakini kama anashika madawa ya kulevya huyo ni msomi mzuri,” alisema Rais Magufuli. Hata hivyo Rais Magufuli amesema kuwa wakati anaanza Urais alitoa milioni mbili kwaajili ya ujenzi wa darasa mkoa wa Dar es salaam, hivyo amemtaka Mkuu wa mkoa huyo kujiandaa maana ataenda kukagua.

Kortini Kwa Kusambaza Uongo Kuhusu Mazungumzo ya Serikali na Acacia

Image
Obadia Frank alipofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. MKAZI wa Chato mkoani Geita, Obadia Frank (41), mapema leo  amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kuhusu mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia. Akisomewa  hati ya mashtaka na wakili wa serikali, Leonard Challo, amedai mshtakiwa huyo ambaye ni wakala wa Bayport ametenda  kosa hilo Agosti 8 mwaka huu, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita. Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri, kuwa siku hiyo mshtakiwa alichapisha taarifa kupitia ukurasa wake wa Facebook uliokuwa ukihusiana na mazungumzo kati ya serikali na kampuni ya Acacia. Mshtakiwa huyo anadaiwa kusambaza maneno kuwa “Taarifa kutoka  kikao cha mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia kuwa wanasheria wa upande wetu wanashindwa kutafsiri baadhi ya vifungu vya sheria hadi kufikia kuom

JAMAA ALIYEOA NG,OMBE INDIA MAZITO YAFICHUKA ,SIRI NZITO NDANI YAKE

Image
GUJARAT, INDIA - MARCH, 2016: Arjun, a bull, is dressed and made ready for his wedding to Poonam, a cow, in Ahmedabad city in Gujarat, India. The wedding of Poonam (cow) and Arjun (bull) was solemnised by priests according to Hindu rituals. Vijay Parsana, 44, organized a grand wedding for his Gir cow, Poonam with Arjun, a bull. He spent lakhs to adorn the cow in a sari and gold jewellery. To welcome the first offspring of the cow the 'parents' of the bull came with sweets as the calf named Saraswati turns one month old. Pictures supplied by: Cover Asia Press Unaambiwa ukistaajabu ya Musa, utaona ya firauni! basi firauni kapatikana. Baba mmoja mfugaji nchini India amewatelekeza mkewe na binti zake wawili kwa kudai kuwa hana furaha kuishi nao kwenye nyumba moja na kuamua kufunga ndoa ya kifahari na Ng’ombe. Baba huyo aliyetambulika kwa jina la Vijay Parsana (44) amechukua uamuzi huo baada ya kukosa faraja kutoka kwa mkewe akidai kunyanyaswa na familia yak

GIGY MONEY,AUNT LULU WAZUA GUMZO,WALINENEPA SASA ‘WAMEPUKUTIKA’

Image
Gift Stanford ‘Gigy Money’. KUNA mastaa ambao walijikuta wakiwaacha wengi midomo wazi kutokana na kuwa na miili iliyoshiba lakini ghafla wakaonekana katika muonekano tofauti wakiwa ‘wamepukutika’ na kuzua viulizo, huku wengi wao wakitoa visingizio mbalimbali. GIGY MONEY Mwanadada huyu anayejulikana kwa jina halisi la Gift Stanford alitikisa mno kwa muonekano wake, jinsi alivyokuwa amenona na kujazia kwenye msambwanda, lakini kitu kilichowaacha wengi hoi ni baada ya kupukutika ghafla, huku sababu mbalimbali zikitajwa, ikiwemo kuharibika kwa mimba kadhaa na `stress’ za mapenzi na hadi sasa mwili wake haujarudi. Amanda Poshy AUNTY LULU Ni moja ya wadada ambao walikuwa gumzo kila kona, huku mara kadhaa akijitapa kuwa wowowo lake ndo kila kitu maishani mwake, lakini siku chache zilizopita mwanadada huyo aliibua taharuki baada ya kuonekana akiwa modo na kalio limeiisha, huku akidai ni kutokana na kufanya mazoezi, hivyo mpaka sasa hajarudi kwenye ubora wake.

ANGALIA DIAMOND PLATINUMS NA WCB WASAFI WALIVYOFANYA KUFURU JANA USIKU

Image
officialbelaire for Life! @sallam_sk ….. TABATA KINYEREZI Kinyerezi @wcb_wasafi iko hapo Leo! Tuseme #Hallelujah!    

LEMA NA NASSARI WAANIKA USHAHIDI WA MADIWANI WA CHADEMA WALIVYONUNULIWA

Image
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, leo wamewasilisha ushahidi wa jinsi madiwani wa Chadema waliotangaza kukihama chama hicho na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), walivyohongwa ili wachukue uamuzi huo. Wakizungumza na waandishi wa habari, Lema na Nassari wameonesha ushahidi wa video na sauti, ukiwahusisha mkuu wa Wilaya ya Arumeru, katibu tawala na mkurugenzi wa wilaya hiyo, walivyokuwa wakipanga michakato ya kuwanunua madiwani hao. Kwa mujibu wa Lema na Nassari, madiwani hao, kila mmoja amepewa fedha ambazo walitakiwa kulipwa posho kwa vikao vyote walivyotakiwa kukaa mpaka 2020 wakiwa madiwani, wamesaidiwa miradi yao mbalimbali nakila mmoja amepewa shilingi milioni kumi. see more at :- https://youtu.be/yTbqJUmZeag

Hatimaye Zamaradi Mketema wa Clouds Aolewa!

Image
Mtangazaji wa Kipindi cha Take One kinachorushwa na Clouds TV, Zamaradi Mketema akiwa katika pozi la kimahaba na mume wake baada ya kufunga ndoa. Zamaradi na mumewe wakiongea jambo kwa furaha. Shangwe zikiendelea. Mtangazaji wa Kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds, Zamaradi Mketema amefunga ndoa na mwanaume anayetajwa kuwa mtoto wa kigogo mmoja mkubwa wa serikali. Picha za wawili hao wakifunga ndoa, zilipoanza kuzagaa mitandaoni, zilizua gumzo kubwa ambapo baadhi ya watu walidai kuwa si picha za ndoa bali ni filamu huku wengine wakidai kwamba ni ndoa halisi. Habari zaidi kuhusu ndoa hiyo, endelea kutembelea mtandao huu na kusoma magazetila Global Publishers.

Nyumba ya Professor Jay Yabomolewa, Afunguka Mazito

Image
Kushoto ni muonekano wa nyumba ya Professor Jay baada ya kubomolewa. Mbunge wa Mikumi Mjini, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amekumbwa na zoezi la bomoa bomoa linaloendelea maeneo ya Kimara, jijini Dar es salaam kwa kuvunjiwa nyumba yake huku akieleza kuwa uvunjaji huo haukufuata sheria. Professor Jay akithibitisha taarifa hizo kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii amesema zoezi hilo limefanyika wakati yeye akiwa jimboni kwake na mbaya zaidi hakupewa taarifa na zoezi hilo limeendeshwa jioni ambapo sio muda wa kazi kiserikali. Mbunge wa Mikumi Mjini, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay. “Jana nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu. Sijawahi kuumia kiasi hiki, nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyowe

China Yaipatia Tanzania Msaada Wa Sh. Bilioni 29.4

Image
Serikali ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi 29.4bilioni kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu, utalii wa kijiolojia na kuukarabati Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong. Katibu huyo amesema 22.4bilioni  zitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera. “Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” amesema   James Ameeleza kwamba  kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho. “Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kujenga uwezo wa wataalamu

Serikali Yalifungia Gazeti la Raia Mwema kwa Kuandika Taarifa za Uongo Kuhusu JPM

Image

Aliyeandika Uongo WhatsApp Kuhusu Polisi Kuonekana Hospitali ya Nairobi

Image
MKAZI mmoja wa Kigamboni, Mbutusyo Mwakihaba (40), amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kusambaza ujumbe katika mtandao kwamba kachero wa Usalama wa Taifa ameonekana jijini Nairobi karibu na hospitali aliyolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Mbutusyo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa. Wakili wa Serikali Janeth Magoho alidai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kusambaza taarifa za uongo chini ya kifungu namba 16 cha Sheria ya mtandao namba 4 ya mwaka 2015. Janeth amedai Septemba 11, mwaka huu kupitia mtandao wa ‘WhatsApp’ mshtakiwa aliandika “Huyu ni Kachero wa Usalama wa Taifa anatambulika kwa jina la Jose anaonekana Nairobi karibu na hospitali alikolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu…Mwaxcheni mwenzenu” . Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo, upelelezi wa kesi haujakamilika ambapo Hakimu Nongwa alikubali kumpa dhamana kwa masharti ya kuwa n

Magazeti Ya Tanzania Leo Jumamosi, Septemba 30, 2017

Image