Rais Magufuli Amwagia Sifa Makonda..Adai Hata Kama Hajui Kusoma Lakini Kama Anashika Madawa ya Kulevya Kwake ni Msomi Mzuri
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe
Magufuli amemsifia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa
kupambana vita dhidi ya dawa za kulevya aliyoianzisha huku akitaka
viongozi wengine kuiga mfano wa kiongozi huyo . Rais Magufuli amesema
hayo kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao
umefanyika leo katikaUkumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam ambapo amemtaka Waziri mkuu, Kassim Majaliwa kuwaambie wakuu wa Mikoa wengine kujifunza kwa Makonda. “RC wa Dar es salaam alipojaribu kusema kuhusu dawa za kulevya kelele zikawa nyingi kweli, mara ooh hajasoma.
Mimi hata kama hajui ‘a’ lakini kama anashika madawa ya kulevya huyo ni msomi mzuri,” alisema Rais Magufuli. Hata hivyo Rais Magufuli amesema kuwa wakati anaanza Urais alitoa milioni mbili kwaajili ya ujenzi wa darasa mkoa wa Dar es salaam, hivyo amemtaka Mkuu wa mkoa huyo kujiandaa maana ataenda kukagua.
Comments
Post a Comment