IGP Sirro Kuhusu Miili Iliyookotwa Coco Beach
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amesema wameunda timu ya
wataalamu kuchunguza miili iliyookotwa na sampuli kutoka miili hiyo
zimechukuliwa.
Amesema iwapo kuna watu ambao ndugu zao wamepotea ni vyema wakafika
katika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa
ajili ya vipimo na kufanyika upelelezi.
“Bahari ni kubwa inapita katika nchi nyingi na inachukua kila kitu,
haya mambo yanapotokea hata nchi nyingine yanatokea, kwa hiyo kimsingi
tumeunda timu ya wataalamu ya kupeleleza kuhusu miili hii, wamechukua
majimaji kutoka mwilini,” alisema.
IGP Sirro alisema, “Kama kuna mtu ambaye ndugu yake amepotea afike
makao makuu ya Polisi upande wa DCI tuweze kufanya uchunguzi kuona kama
ni ndugu yake.”
Alisema miili hiyo haijabainika kuwa ni ya watu wa Taifa gani. “Tatizo
letu Watanzania ni kwamba moja kwa moja wanaanza kuhisi, sijui kwa nini
tunakuwa tunaishi kwa hisia na hii hisia hisia si nzuri, tuseme kitu
tukiwa na uhakika. Ikitokea jambo utasema ni Sirro, utasema ni nani, hii
si nzuri na niwaambie tumwogope Mungu pia,” alisema IGP Sirro.
Comments
Post a Comment