Aliyeandika Uongo WhatsApp Kuhusu Polisi Kuonekana Hospitali ya Nairobi
MKAZI
mmoja wa Kigamboni, Mbutusyo Mwakihaba (40), amefikishwa mahakamani kwa
tuhuma za kusambaza ujumbe katika mtandao kwamba kachero wa Usalama wa
Taifa ameonekana jijini Nairobi karibu na hospitali aliyolazwa Mbunge wa
Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mbutusyo amefikishwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu
Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa.
Wakili wa Serikali Janeth Magoho
alidai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kusambaza taarifa za uongo chini
ya kifungu namba 16 cha Sheria ya mtandao namba 4 ya mwaka 2015.
Janeth amedai Septemba 11, mwaka huu kupitia mtandao wa ‘WhatsApp’ mshtakiwa aliandika “Huyu
ni Kachero wa Usalama wa Taifa anatambulika kwa jina la Jose anaonekana
Nairobi karibu na hospitali alikolazwa Mbunge wa Singida Mashariki,
Tundu Lissu…Mwaxcheni mwenzenu”.
Mshtakiwa alikana kutenda makosa
hayo, upelelezi wa kesi haujakamilika ambapo Hakimu Nongwa alikubali
kumpa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika
watakaosaini dhamana ya Sh milioni tano kila mmoja ambapo mshtakiwa
alishindwa kutimiza masharti hayo na kurudishwa mahabusu hadi Oktoba 12,
mwaka huu.
Comments
Post a Comment