Taarifa Muhimu ya TCU kwa Wanafunzi Waliokosa Vyuo


Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa  awamu ya kwanza ya Udahili wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ulimalizika tarehe 30 Agosti 2017.
Tume inawaarifu kuwa imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji wote walioomba kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo wa 2017/18.
Hata hivyo kutokana na  waombaji wengi  kutochaguliwa  kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 4 hadi 10 Octoba 2017 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili:
•  Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza;
•  Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika  awamu ya kwanza;
•  Waombaji wenye vigezo vya Stashahada  walioshindwa kupata Namba ya Uhakiki wa Tuzo (AVN);
•  Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge”  mwaka 2017 na matokeo yao yameshatoka; na
•  Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitsho toka vyuo vyao vya awali.
Aidha Tume inapenda kusisitiza kuwa utaritibu wa kutuma
maombi ni ule ule uliotumika katika awamu ya kwanza ya Udahili.
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
4 Oktoba 2017.

Comments

Popular posts from this blog