FAIDA ZA UGALI WA DONA
MARA nyingi baadhi ya watu huwahimiza watu wengine kutumia unga wa mahindi au nafaka zingine usiokobolewa bila ya kubainisha hasara ya unga wa aina hiyo. Watu wengi (bila shaka hata wewe msomaji wa makala haya), hawako tayari kutumia unga usiokobolewa maarufu kama dona. Kuwalazimisha watu wa aina hiyo kutumia unga usikobolewa (unga wa dona) ni sawa na kuwaweka watu hao katika hatari ya kuwa na lishe duni. UNGA WA MAHINDI Unga wa mahindi, ulezi, uwele, mtama na kadhalika ni chanzo kikubwa kwa watu wengi barani Afrika cha virutubisho kama vile wanga, protini, madini na vitamini. Hata hivyo, namna ya usagaji na matumizi ya unga wa mahindi na nafaka hizo inaweza kuukosesha mwili faida ya virutubisho vilivyomo katika nafaka hiyo. UNGA ULIOKOBOLEWA Mahindi yaliyokobolewa yaani sembe au nafaka zingine zikikobolewa kama mtama, ulezi n.k hupoteza sehemu fulani ya nafaka hizo. Kama mahindi au mtama na ulezi utasagwa bila kukobolewa unga wake huitwa unga wa dona (whole-g