Waziri Lukuvi: "Bomoabomoa hainihusu"

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefunguka na kusema zoezi la bomoabomoa linaloendelea jijini Dar es Salaam katika maeneo ya Kimara na Kibamba yeye halimuhusu hivyo awataka watu wamuulize Waziri wa ujenzi, uchukuzi
Waziri Lukuvi alisema zoezi linaloendelea Kimara na Kibamba ni sheria ya barabara ndiyo inayofanya ile kazi na siyo yeye na kuwataka watu wamtafute Waziri husika ili aweze kuwapa maelezo juu ya jambo hilo.
"Hapana siwezi kuzungumzia hilo nenda kamuone Waziri wa Ujenzi kwani Sheria ya barabara ndiyo inayofanya ile kazi siyo mimi hivyo siwezi kuzungumza lolote kwenye hilo jambo kwani mimi bomoabomoa hiyo hainihusu, kwani kila mtu anaapa kwa kipande chake na mimi siyo Waziri wa jumla, Waziri wa jumla ni Waziri Mkuu" alisema Lukuvi 
Aidha Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani vikali zoezi la bomoabomoa linaloendelea katika maeneo hayo ya Kimara na Kibamba kwa kusema TANROAD hawajatenda haki dhidi ya wananchi kwa kuwa kulikuwa na zuio la mahakama kuzuia zoezi hilo mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa na wananchi hao itakaposikiliza lakini TANROD wamekaidi zuio hilo la mahakama.

Comments

Popular posts from this blog