Posts

ACACIA Wapinga Ripoti ya Kamati ya Pili ya Rais JPM Kuhusu Mchanga wa Madini

Image
12 Juni 2017 Mwitikio wa Acacia kwenye matokeo ya kamati ya pili ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Acacia imeona matokeo ya kushtua ya kamati ya pili ya Rais iliyowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Mh. Dk John P. Magufuli leo asubuhi ambayo imeangalia nyanja za historia za kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini. Kamati ya Pili imetoa matokeo yake kwa kutumia matokeo ya Kamati ya Rais ya Kwanza, iliyotangazwa tarehe 24 Mei 2017, ambayo Acacia imeikanusha vikali. Kamati hiyo ilipata matokeo yake kwa kutumia sampuli ya kontena 44. Kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha matokeo yetu na yaliyokutwa na kamati, na kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10 kuliko thamani halisi ya makanikia Kamati ya Pili inadai kuwa Acacia imetangaza kiasi cha chini cha mapato kuliko inavyopata na kulipa kodi kidogo kuliko inavyostahili kwa miaka mingi na kuficha mabilioni ya dola ya Marekani. Na hivyo imefanya mapen...

Spika Ndugai apigilia msumari Ripoti ya madini

Image
"Hakuna kitu kibaya kuwa katikati ya dhiki ambayo hukuistahili"-amesema Spika Ndugai baada ya kukabidhiwa ripoti ya pili ya kamati maalumu iliyoundwa na Rais Magufuli kuchunguza sakata la mchanga wa Madini Leo Ikulu Jijini Dar es salaam "Haya ni mambo ya ajabu, ni mikataba ya kijinga na ya hovyo, Mimi na wabunge wenzangu wote kuhakikisha sheria zote zitakazoletwa tutazitendea haki"- Alisema Spika Ndugai Hatua hiyo imefuata baada ya Mapendekezo ya kamati ya hiyo iliyotaka sheria za nishati Madini zifanyiwe marekebisho ya haraka, ambapo Rais Magufuli ametaka bunge lifanye haraka iwezekanavyo.

Kilichouzwa nje ni Madini, Sio mchanga

Image
  "Biashara ya uuzwaji wa Makinikia haikufanyika kwa ushindani na si kweli kwamba wanauza Makinikia, kinachouzwa ni madini." amesema Mwenyekiti wa Kamati ya kuchunguza mchanga wa madini, Profesa Nehemiah Osoro Prof. Osoro ameyasema hayo wakati akikabidhi ripoti ya kamati yake kwa Rais John Magufuli leo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa gharama za shughuli za utafutaji na upembuzi madini nchini zimejumuishwa katika mauzo yake kwa kupunguza faida hivyo hawatozwi kodi. "Faida yote iliyopatikana katika uuzwaji wa dhahabu nje haikujumuishwa katika mahesabu ili kukwepa malipo ya mrabaha" alisema Prof. Osoro Ameongeza kuwa uchunguzi wa kamati yake umebaini kuwepo kwa utakatishwaji haramu wa fedha na faida kurudishwa kama mkopo kwa makampuni ya madini kitu ambacho ni kinyume cha taratibu.

KAMPUNI YA KUCHIMBA MADINI ACACIA ILIINGIA KINYEMELA NA HAINA KIBALI CHOCHOTE

Image
Taarifa ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Joseph Magufuli, imebaini kuwa kampuni ya ACACIA Mining Plc haina kibali na inafanya kazi kinyume cha sheria.Prof. Osoro amesema kwamba Kamati yake imebaini kuwa Acacia haina uhalali wa kufanya shughuli zake hapa nchini na imetenda makosa yakiwemo kujipatia mali kwa udanganyifu, uhujumu uchumi, jinai na kuitia hasara taifa.Aidha Kamati ya Prof. Osoro imebaini kwamba Makinikia yaliyouzwa nje ya nchi hayakuwa makinikia hasa, bali yalikuwa ni madini mbalimbali huku ikiongeza kwamba katika mikataba ya uuzwaji wa makinikia hayo, serikali haikuwa sehemu ya mikataba hiyo.Prof. Osoro ameongeza kwamba jumla ya mapato yote ambayo serikali imepoteza ni Tsh. trilion 68.6 sawa na bajeti ya miaka miwili ya nchi kodi ya mapato ambayo taifa imepoteza ni Tsh. tril 55.07, mrahaba tril 11, bandari tril 1.6. na kwamba jumla ya thamani ya madini ...

MTOTO WA MIAKA 12, MOHAMED ABDULLAH AIBUKA MSHINDI MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN BARANI AFRIKA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) MTOTO wa miaka 12 kutoka Somalia, Mohammed Abdullahi Aden ameibuka kidedea na kitita cha dola za Marekani 7,000 (sawa na sh. milioni 15.75) katika mashindano ya 18 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.  Mohammed ambaye ni miongoni mwa washiriki wadogo zaidi wawili kuliko wote (mwenzake anatoka Burundi), amejishindia pia IPAD, cheti, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ahadi ya kwenda nchi yoyote aitakayo kutoka kwa kampuni ya Sky Bus Travel Agency ya jijini Dar es Salaam.  Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa j...

Fundi Seremala Mbaroni kwa kuwabaka binti zake

Image
FUNDI Seremala, Japhet Lendiman (38) mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya kubaka watoto wake wa kike wa darasa la sita na kidato cha kwanza. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kiini cha tatizo hilo ni nini na kufuatiwa na hatua ya kufikishwa mahakamani. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la polisi tangu Juni 6, mwaka huu na upelelezi unaendelea kubaini undani wa tukio hilo. Akimzungumzia mtuhumiwa huyo, mmoja wa majirani wa eneo hilo la Daraja Mbili (jina limehifadhiwa) alidai kuwa mzazi huyo amezoeleka kwa tabia hiyo mbaya mtaani kwao. Alidai kuwa mtuhumiwa huyo amezoea kubaka watoto wake mara kwa mara wakati mama yao akiwa kazini na kwamba Mei 28 majira ya saa 9:00 alasiri alimbaka tena mtoto wake (Jina tumelihifadhi) wa darasa la sita shule ya Msingi Daraja Mbili ndipo taarifa zilipoanza kuzagaa mtaani. “Siku hiyo ya tukio lililo...

Zaidi ya wanafunzi 2000 watemwa kidato cha tano

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015. Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi. Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Simbachawene alisema ...

Dalili za Madhara ya Tezi Dume

Image
Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe za uhai katika tezi la kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalozunguka mirija ya kupitisha haja ndogo( mkojo).Ugonjwa huu kwa sasa unaweza kuwapata vijana wa kiume kuanzia miaka 25 na kuendelea tofauti na awali ilikuwa miaka zaidi ya 50. Dalili za ugonjwa huu; Kwenda haja ndogo mara kwa Mara,hasa usiku. Haja ndogo Za ghafla zisizoweza kudhibitiwa. Mkojo unaotoka kwa udhaifu ama kwa kukatika katika . Damu kuchanganyikana na mkojo. Maumivu  yanaendelea kwenye maeneo ya mgongoni sehemu Za kiunoni,kwenye kinena au sehemu juu ya mapaja. Madhara yake: 1.Kupungua kwa uwezo kufanya tendo la ndoa.Pia kusikia maumivu wakati wa kufikia kilele Na kukosa amani au kuhangaika  wakati wa tendo la ndoa. 2.Uambukizo wa magonjwa kwenye kipofu 3.Uambukizo  mwenge njia ua mkojo au figo. Ndugu ugonjwa huu unaua hata wenye uwezo wa kifedha maana ni hatari sana chukua tahadhari sasa pia msaidie n...

Halima Mdee na Ester Bulaya Kulipwa nusu Mshahara

Image
Wabunge wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) ambao wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge, watalipwa nusu mshahara na posho zinazoambatana nao kwa miezi kumi. Stahiki hizo ni kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya Bunge inayosema, “mbunge aliyesimamishwa hataingia tena sehemu yoyote ya ukumbi na maeneo ya Bunge kwa muda wote atakapokuwa amesimamishwa na atalipwa nusu mshahara na nusu posho zinazoambatana na mshahara huo.” Vilevile, kutokana na uamuzi huo wabunge hao watakosa siku 65 za Bunge zinazojumuisha siku 25 zilizobaki za Bunge la bajeti linaloendelea, Bunge la Oktoba na lile la Februari, 2018. Vikao vya mabunge hayo mawili; la Oktoba na Februari kila kimoja huwa na mikutano ya wiki mbili mbili. Wabunge hao walisimamishwa juzi kwa azimio la Bunge licha ya kutokuwapo au kujitetea kutokana na tuhuma zilizokuwa zinawakabili za kudharau kiti cha spika. “Tukutane Bunge lijalo la bajeti,” alisema juzi Spika wa Bunge, Job Ndugai. Bunge l...

IGP SIRRO AFANYA ZIARA KIBITI,ATANGAZA VITA KALI,ATANGAZA DONGE LA MILIONI 10 s

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amefanya ziara katika maeneo ya Kibiti na Mkuranga kutimiza ahadi baada ya kuombwa na wazee wa maeneo hayo kufuatia mauaji ambayo yamekuwa yakiripotiwa kutokea mara kwa mara.Mara baada ya kuzungumza na wazee hao, IGP Sirro amesema kuwa wazee hao wametoa ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na namna ya kuwapata waharifu ambao wamekuwa wakifanya mauaji katika maeneo hayo. Sirro amewaahidi wananchi wa maeneo hayo kuwa atatoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa raia mwema atakayetoa taarifa sahihi kwa watu wanaofanya mauaji mkoani. Tazama hapa

MSIBA WA IVAN WAMUIBUA BABA YAKE ZARI,AFUNGUKA MENGI MAZITO

Image
Kwa muda mrefu staa wa muziki na mjasiriamali wa Afrika Mashariki, raia wa nchini Uganda, mwenye maskani yake mengine huko Pretoria, Afrika Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, amekuwa akionekana Bongo na mama yake mzazi, Halima Hassan hivyo kuibua sintofahamu juu ya alipo baba yake, Hassan Tiale. Hata hivyo, kifo cha mkwe wake yaani aliyekuwa mume wa mwanaye, Zari, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ aliyefariki dunia Mei 25, mwaka huu, kimemaliza utata huo baada ya kumuibua mzee huyo aliyekuwa amejaa tele kwenye msiba huo nchini Uganda. Mzee Hassan alikuwa mmoja wa watu lukuki waliohuzunishwa na kifo cha Ivan ambapo alisema kuwa, alilazimika kuacha shughuli zake ili kuhudhuria msiba huo kwa namna alivyokuwa akiivana na Ivan. “Msiba huu umenigusa sana. Nilipigiwa simu nikiwa Nairobi (Kenya) ambako nilikwenda kumuozesha kijana wangu bibi (mke) “Nilisikia Ivan aliteleza kwa ajili ya presha, akaanguka chini, akachukuliwa, akapelekwa hospitalini Afrika Kusini, akawe...

MAREHEMU PHILEMON NDESMBURO AZIKWA MKOANI KILIMANJARO

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bw. Freeman Mbowe akiwasili nyumbani kwa marehemu Philemon Ndesamburo wakati alipohudhuria mazishi yake yaliyofanyika leo  Moshi mkoani Kilimanjaro Marehemu Ndesamburo alifariki wiki iliyopita na kuzikwa leo mkoani humo angalia matukio mbalimbali  katika picha kuhusu tukio zima la ibada ya mazishi.(Picha na Dixonbusagagablog).

Wafahamu Wanawake 4,000 Wanaojifunza Kuwa Maninja Iran

Image
 Miongoni mwa wanawake 4,000 wanaochukua mafunzo ya uninja jangwani nchini Iran. WANAWAKE nchini Iran hivi sasa wanajifunza mbinu za wapiganaji wa Ninja kupitia mbinu za Ninjutsu katika klabu ya mafunzo hayo iliyofunguliwa mwaka 1989 iliyopo Jughin, kilomita zipatazo 52 kutoka jiji la Tehran. Mafunzo hayo yanayofanyika jangwani,  yamelenga kuwafanya wanawake hao kuwa ‘kunoichi’, yaani maninja wa kike.  Katika mafunzo yao wanawake hao wanafanya mazoezi ya kupanda na kuruka kutoka katika kuta mbalimbali, kujificha katika milima na kuweza ‘kukata’ shingo ya adui bila kelele yoyote.