MSIBA WA IVAN WAMUIBUA BABA YAKE ZARI,AFUNGUKA MENGI MAZITO
Kwa muda
mrefu staa wa muziki na mjasiriamali wa Afrika Mashariki, raia wa nchini
Uganda, mwenye maskani yake mengine huko Pretoria, Afrika Kusini,
Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, amekuwa akionekana Bongo na mama
yake mzazi, Halima Hassan hivyo kuibua sintofahamu juu ya alipo baba
yake, Hassan Tiale.
Hata
hivyo, kifo cha mkwe wake yaani aliyekuwa mume wa mwanaye, Zari, Ivan
Ssemwanga ‘Don Ivan’ aliyefariki dunia Mei 25, mwaka huu, kimemaliza
utata huo baada ya kumuibua mzee huyo aliyekuwa amejaa tele kwenye msiba
huo nchini Uganda. Mzee Hassan alikuwa mmoja wa watu lukuki
waliohuzunishwa na kifo cha Ivan ambapo alisema kuwa, alilazimika kuacha
shughuli zake ili kuhudhuria msiba huo kwa namna alivyokuwa akiivana na
Ivan. “Msiba huu umenigusa sana. Nilipigiwa simu nikiwa Nairobi (Kenya)
ambako nilikwenda kumuozesha kijana wangu bibi (mke)
“Nilisikia
Ivan aliteleza kwa ajili ya presha, akaanguka chini, akachukuliwa,
akapelekwa hospitalini Afrika Kusini, akawekwa ICU (chumba cha wagonjwa
mahututi). “Niliendelea kupigiwa simu nyingi, nikaambiwa hali inazidi
kuwa mbaya. Niliambiwa mshipa wa kupeleka damu kwenye ubongo ulipasuka.
Hadi zilipopita saa ishirini na nne na kuendelea ndiyo niliambiwa
amefariki dunia.
“ B a s i
, n d i y o nikaacha shughuli z a n g u nikaja hapa (nyumbani kwa Ivan,
Kampala) k w e n y e m s i b a maana alikuwa mtu mzuri sana. Hayo
mengine ni manenomaneno ambayo ya nasemwa.
“Kwa kweli Ivan alikuwa mtu mzuri sana na ndiyo maana kila mtu anamzungumzia vizuri,” alikaririwa mzee huyo.
Naye dada
wa Zari aliyejitambulisha kwa jina la Madina Hassan alisema kuwa,
alifahamiana na Ivan alipofika nyumbani kwao kujitambulisha wakati Zari
alipopata mtoto wao wa kwanza wa kiume, Pinto.
“Nilishtushwa
sana na kifo chake kwa sababu alikuwa mtu aliyependa kufurahi wakati
wote, hivyo ni pigo kubwa kwangu,” alisema Madina. Ivan aliyezaa watoto
watatu wa kiume na Zari kabla ya kutengana alizikwa Mei 30, mwaka huu
kijijini kwao, Nakalilo nchini Uganda.
Credit GlopalPublisher
Comments
Post a Comment