Wafahamu Wanawake 4,000 Wanaojifunza Kuwa Maninja Iran
WANAWAKE nchini Iran hivi sasa wanajifunza mbinu za wapiganaji wa Ninja kupitia mbinu za Ninjutsu katika klabu ya mafunzo hayo iliyofunguliwa mwaka 1989 iliyopo Jughin, kilomita zipatazo 52 kutoka jiji la Tehran.
Mafunzo hayo yanayofanyika jangwani, yamelenga kuwafanya wanawake hao kuwa ‘kunoichi’, yaani maninja wa kike. Katika mafunzo yao wanawake hao wanafanya mazoezi ya kupanda na kuruka kutoka katika kuta mbalimbali, kujificha katika milima na kuweza ‘kukata’ shingo ya adui bila kelele yoyote.
Comments
Post a Comment