Faida za kutumia juisi ya miwa katika kuimarisha afya zetu
Bila shaka unaifahamu juisi ya miwa, watu wengi tumekuwa tunakunywa na wengine tukiwa tunaibeza pia, hii ni kwasababu tumekuwa hatujui faida zitokanazo na unywaji wa huisi hiyo. Leo nataka nikupashe japo kwa uchacje faida za kunywa juisi ya miwa katika afya zetu. Kunafaida nyingi za juisi ya miwa. Baadhi ya faida hizo ni kama zifuatazo; 1. Juisi ya miwa inauwezo mkubwa wa kuipatia miili nguvu kwa haraka na kukata kiu ya maji. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari "sucrose" ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwahiyo wakati mwingine ukiwa na nguvu au uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa. 2. Husaidia figo kufanya kazi vizuri. Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na ku-imarisha ufanyaji kazi wa figo. Juisi a miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu hasa yanayosababishwa na mawe yaliyopo kwenye figo. 3. Hupunguza uwezrkano wa kupata ugonjwa wa kansa....