Posts

HUU NDIO UJUMBEE ALIOANDAKA STAA WEMA SEPETU KABLA YA MKUTANO WA MBUNGE LEMA

Image
MSANII wa filamu na malkia wa mtandao nchini Wema Sepetu ‘Madam’,  amejikita zaidi katika siasa baada ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivi karibuni. Wema ameendelea kuzianika mitandaoni  baadhi ya harakati zake za kisiasa ikiwa ni pamoja na kujihusisha na shughuli za kijamii kama vile upandaji wa miti,  uliofanywa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na leo kabla ya Lema kuhutubia, ameweka picha na ujumbe mtandaoni unaowahamasisha watu kufika katika mkutano huo. “All Ready Kwa Ajili ya Mkutano wa Mhe. GodBless Lema… See you there…. Giving MY Chadema A New Look… Y’all Know Black And Khaki Be our Colour…. A lil White to add Flavor wont Hurt Nobody…. #CallMeKamanda cc @upendosimwita1 @ _ elm _ @blowassa”, alimaliza Wema. Share this

UN SECRETARY GENERAL STOPS IN DAR ON HIS WAY TO NEW YORK

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres (kushoto) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam jana. Mhe. Guterres alisimama kwa muda katika uwanja huo akitokea nchini Kenya kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Balozi Mahiga.  Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe Guterres aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa Mgogoro huo Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Benjamin Willium Mkapa. Aidha, Dkt. Mahiga aliwasilisha Salamu Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.  Waziri Mahiga akizungumza jambo huku Mhe. Guterres akimsikiliza kwa makini.  Dkt. Mahiga akiendelea kuzungumza na Mhe. Guterres huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa S

KESI INAYOMKABILI MAXENCE MELO YAAHIRISHWA TENA HADI APRILI 3

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kesi namba 456 inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na mwenzake na Mwanahisa Mike Mushi isipoendelea itafutwa. Hayo yalisemwa alhamisi hii na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kukerwa na upande wa Jamhuri ambao ulishindwa kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali badala yake ukaomba kuahirisha kesi. Mwendesha Mashtaka, Inspekta Hamis Said, alidai mbele ya Hakimu Simba kwamba kesi ilitakiwa kuanza kusikilizwa awali lakini wakili anayeiendesha anaumwa. Mwendesha mashtaka aliomba kesi hiyo iahirishwe mpaka tarehe nyingine itakayopangwa. Hata hivyo Hakimu Simba alieleza kukerwa na tabia ya kesi kuahirishwa na kusema wakati mwingine kama kesi hiyo haitaendelea ataifuta. Aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 3, mwaka huu na dhamana ya washtakiwa inaendelea. By: Emmy Mwaipopo

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA.

Image
Picha namba 1-5. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo tarehe 9/03/2017. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU

SAIDA KAROLI ASIMULIA JINSI ALIVYOIBIWA KAZI ZAKE KISA KUTOJUA KUSOMA NA KUANDIKA

Image
Jana kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, mtangazaji Zamaradi alimuhoji mwimbaji wa muziki wa asili Saida Karoli ambapo alikiri kuwa hana haki kwenye nyimbo zake kutokana na mikataba aliyosainishwa na Meneja wake sababu na yeye hakuwa anajua kusoma na kuandika na akadai zaidi ya album tano hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye haki nazo .Kingine alichozungumza Saida ni kuhusu wimbo wa Salome ambao Diamond Platnumz aliurudia ambapo alisema ana hesabu kama alitoa bure kwani hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea. ”Siwezi kulalamika hata kidogo, mara nyingi naulizwa nasema sina tatizo, sina haki na zile nyimbo maana yeye ndio alinipa mikataba na yeye ndio alinitengenezea, hata hii ya Diamond naweza nikasema ikawa mbaya zaidi maana fedha niliyoipata siyo ya kuongelea, kwahiyo mimi najiona nimetoa bure”Waandishi kila siku wanakuwa wananiuliza nawambia nimempa Diamond nyimbo bure na nimetoa kwa moyo mmoja kweli, roho yangu moja  

Paul Makonda Aenda Mapumziko ya Miezi Miwili South Africa

Image
Wakati utata ikigubika kuhusu safari ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenda nchini Afrika Kusini, imebainika kuwa kiongozi huyo atakuwa likizo nchini humo kwa zaidi ya miezi miwili. Kwa mujibu wa habari iliyoandikwa katika gazeti la TanzaniaDaima imeeleza uwepo wa RC Makonda nchini Afrika Kusini ndio sababu ya kushindwa kuhudhuria sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia ambapo ilitangazwa kuwa angekuwa mgeni rasmi katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Mwembeyanga. Kuondoka kwake nchini kumekuwa kwa kutatanisha wakati mamlaka husika zikishindwa kutoa taarifa kamili kuhusuana na safari yake. Wadadisi wa mambo wanahoji uhalali wa Makonda kupewa mapumziko hayo nje ya nchi huku serikali ilitangaza kuzuia ziara zote za watumishi nje ya nchi ili kubana matumizi. Kutokana na zuio la safari za nj

Tundu Lissu Afunguka Baada ya Kusikia Mwakyembe Amemzuia Kugombea Nafasi ya Rais wa TLS

Image
Anaandika Wakili Msomi Tundu Lissu: Waheshimiwa mawakili na wananchi wa nchi yetu. Nimesoma taarifa katika magazeti kadhaa ya leo kwamba Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison George Mwakyembe amenizuia kugombea nafasi ya Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS). Kama taarifa hizo ni za kweli basi naomba kuweka masuala yafuatayo wazi: (1) Waziri wa Sheria na Katiba hana mamlaka yoyote, kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha TLS na kanuni zake, ya kuzuia ama kuruhusu mwanachama yeyote wa TLS kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya TLS. Hivyo, kama kweli Dkt. Mwakyembe ametoa kauli hiyo, basi huo utakuwa uthibitisho wa ama upungufu mkubwa wa uelewa wa Sheria au hulka ya ukiukaji wa sheria (culture of impunity) ambayo imeshamiri sana katika utawala huu wa sasa. (2) Mamlaka pekee inayohusika na uchaguzi wa TLS ni Kamati ya Uteuzi (Nominations Committee) ambayo ilikwishafanya uteuzi wa wagombea wote kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa na Sheria na Kanuni za

VANESSA MDEE MIKONONI MWA POLISI

Image
Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia Mwanamziki Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya. Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha biashara hiyo pamoja na watumiaji mapema mwezi uliopita. Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza kuwa Polisi walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi. Vanessa Mdee ni Mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV VJ, Mdee, alizaliwa mwaka 1988 Arusha, alianza kufahamika zaidi mara baada ya kutangaza kwenye Redio na Luninga kwenye vipindi kama Epic Bongo Star Search na Dume Challenge na baadae kidogo wakati ananza kujikita kwenye muziki alikuwa ch

VIROBA VYA BILIONI 5 VYAKAMATWA DAR

Image
KATONI 32,634 za pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5.18 zimekamatwa jana, katika operesheni maalumu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uingizaji, uuzaji na matumizi ya pombe hizo. Pombe hizo zimekamatwa katika operesheni inayoendelea katika mikoa mitatu ya Kikodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dar es Salaam ambayo ni Temeke, Kinondoni na Ilala. Akizungumza katika operesheni hiyo, Mkaguzi kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), John Nzila alisema walikamata katoni 14,393 za konyagi, katoni 9,964 za Vradmill, Zanzi 31 na Valeur. 268. Alisema mzigo huo ulikutwa katika ghala la Loverira Enterprises lililopo Kimara Temboni na kwamba mzigo huo umezuiwa kwa hatua zaidi. Kwa upande wake Mwanasheria Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Heche Suguta alisema kuwa walikamata katoni 7,000

MTANGAZAJI DJ FETTY KUREJEA CLOUDS FM LEO

Image
Dunia inaadhimisha mchango na thamani ya Wanawake duniani kila inapofika Tarehe 8 March kila mwaka.Kila nchi inakuwa na utaratibu wake wa namna gani wa kusherehekea ama kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.Wapo Wanawake wengi ambao wameleta alama chanya ya mabadiliko kwenye tasnia mbalimbali ikiwepo tasnia ya Burudani.Huwezi kuwataja kwa majina Wanawake wote ila wapo wengi ambao walileta mabadiliko yakaonekana kwa kile walichokuwa wanafanya. Clouds Fm kulikuwa na sauti moja nzuri hivi katika Dakika 180 katikati ya wanaume wawili wakorofi in town.Ushajua namzungumzia nani eeeh! Basi vunga Kama umeshamfahamu niwatonye washkaji ambao hawakubahatika kumsikiliza sauti yake.Binti wa kisukuma Fatma Hassan muite Dj Kwefeee ukipenda Fetty siku ya kesho anadondoka mjengoni kuiongoza show namba moja ya kijanja Xxl kuadhimisha siku ya Wanawake duniani.Dj Fetty ambaye aliondoka Clouds mwaka 2015 baada ya kuomba kupumzika aendelee na mishemishe zake siku ya kesho atakuwepo mje

Mama Mlezi wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Afariki Dunia

Image
Mama mlezi wa aliyekuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Bi Nuru binti Halfani Shomvi amefariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akitibiwa asubuhi ya leo. Kupitia mtandao wa twitter, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akishukuru jamii kwa salamu za pole alizopokea amesema shughuli za msiba ziko nyumbani kwa marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo na maziko yatakuwa Bagamoyo mjini, kesho Jumatano Machi 8, 2017 saa 10 Alasiri. “Mama amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu, Mzee Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998. Mama yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee Halfani Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo”. Kauli ya Jakaya Kikwete Naye Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete ambaye ni mjukuu wa marehemu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho asubuhi ya leo. “Ndugu na marafiki nasikitika kuwatangazia

WAZIRI MBARAWA AWATAKA TEMESA KUONGEZA UJUZI UTENGENEZAJI WA VIVUKO.

Image
  Meneja Mradi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport inayojenga Kiuvko cha MV. Kazi, Bw. Major Songoro,   akitoa ufafanuzi wa mashine kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alipokagua Kivuko hicho jijini Dar es Salaam.   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akiangalia moja ya vifaa vilivyoko kwenye chumba cha kuendeshea kivuko katika kivuko cha MV. Kazi kinachojengwa jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kitakabidhiwa tarehe 15 Mwezi huu. Wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), Dkt. Musa Mgwatu.   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia),  akifafanua jambo kwa Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV Kazi ambacho kinatengenezwa jijini Dar es salaam na Kampuni ya Songoro Marine Transport.   Mafundi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport, wakiendelea na kazi ya

BOSI ALIYEMPA RC MAKONDA HEKARI 1500 AHOJIWA

Image
Mkurugenzi wa kampuni ya Azimio Housing Estate, Mohamed Ikbal, ambaye hivi karibuni alimgawia ardhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amehojiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka za Serikali. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha jana kwamba mfanyabiashara huyo aliitwa kwa ajili ya mahojiano, lakini aliachiwa kwa dhamana baada ya muda kuonekana hautoshi. “Alikuja na wakili wake, lakini ameachiwa kwa dhamana ataripoti siku nyingine (hakutaja siku),” alisema Sirro. “Anatuhumiwa kughushi nyaraka za Serikali na sasa upelelezi unaendelea.” Mfanyabiashara huyo inadaiwa kuwa aliripoti polisi jana saa tano asubuhi na kuhojiwa kabla ya kuachiwa kwa dhamana jioni. Kuhojiwa kwa Ikbal, ambaye kampuni yake iliwahi kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika miradi kadhaa tata ya ujenzi, kumekuja siku chache baada ya kumgawia Makonda eneo la ekari 1500 katika kitong