KESI INAYOMKABILI MAXENCE MELO YAAHIRISHWA TENA HADI APRILI 3
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kesi namba 456 inayomkabili Mkurugenzi
Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na mwenzake na
Mwanahisa Mike Mushi isipoendelea itafutwa.
Hayo
yalisemwa alhamisi hii na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya
kukerwa na upande wa Jamhuri ambao ulishindwa kuwasomea washtakiwa
maelezo ya awali badala yake ukaomba kuahirisha kesi.
Mwendesha
Mashtaka, Inspekta Hamis Said, alidai mbele ya Hakimu Simba kwamba kesi
ilitakiwa kuanza kusikilizwa awali lakini wakili anayeiendesha anaumwa.
Mwendesha mashtaka aliomba kesi hiyo iahirishwe mpaka tarehe nyingine
itakayopangwa.
Hata
hivyo Hakimu Simba alieleza kukerwa na tabia ya kesi kuahirishwa na
kusema wakati mwingine kama kesi hiyo haitaendelea ataifuta. Aliahirisha
kesi hiyo hadi Aprili 3, mwaka huu na dhamana ya washtakiwa inaendelea.
By: Emmy Mwaipopo
Comments
Post a Comment