Posts

VANESSA MDEE MIKONONI MWA POLISI

Image
Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemshikilia Mwanamziki Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya. Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha biashara hiyo pamoja na watumiaji mapema mwezi uliopita. Mwanasheria Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza kuwa Polisi walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi. Vanessa Mdee ni Mtanzania wa kwanza kuwa mtangazaji wa MTV VJ, Mdee, alizaliwa mwaka 1988 Arusha, alianza kufahamika zaidi mara baada ya kutangaza kwenye Redio na Luninga kwenye vipindi kama Epic Bongo Star Search na Dume Challenge na baadae kidogo wakati ananza kujikita kwenye muziki alikuwa ch

VIROBA VYA BILIONI 5 VYAKAMATWA DAR

Image
KATONI 32,634 za pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) zenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5.18 zimekamatwa jana, katika operesheni maalumu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uingizaji, uuzaji na matumizi ya pombe hizo. Pombe hizo zimekamatwa katika operesheni inayoendelea katika mikoa mitatu ya Kikodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dar es Salaam ambayo ni Temeke, Kinondoni na Ilala. Akizungumza katika operesheni hiyo, Mkaguzi kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), John Nzila alisema walikamata katoni 14,393 za konyagi, katoni 9,964 za Vradmill, Zanzi 31 na Valeur. 268. Alisema mzigo huo ulikutwa katika ghala la Loverira Enterprises lililopo Kimara Temboni na kwamba mzigo huo umezuiwa kwa hatua zaidi. Kwa upande wake Mwanasheria Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Heche Suguta alisema kuwa walikamata katoni 7,000

MTANGAZAJI DJ FETTY KUREJEA CLOUDS FM LEO

Image
Dunia inaadhimisha mchango na thamani ya Wanawake duniani kila inapofika Tarehe 8 March kila mwaka.Kila nchi inakuwa na utaratibu wake wa namna gani wa kusherehekea ama kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani.Wapo Wanawake wengi ambao wameleta alama chanya ya mabadiliko kwenye tasnia mbalimbali ikiwepo tasnia ya Burudani.Huwezi kuwataja kwa majina Wanawake wote ila wapo wengi ambao walileta mabadiliko yakaonekana kwa kile walichokuwa wanafanya. Clouds Fm kulikuwa na sauti moja nzuri hivi katika Dakika 180 katikati ya wanaume wawili wakorofi in town.Ushajua namzungumzia nani eeeh! Basi vunga Kama umeshamfahamu niwatonye washkaji ambao hawakubahatika kumsikiliza sauti yake.Binti wa kisukuma Fatma Hassan muite Dj Kwefeee ukipenda Fetty siku ya kesho anadondoka mjengoni kuiongoza show namba moja ya kijanja Xxl kuadhimisha siku ya Wanawake duniani.Dj Fetty ambaye aliondoka Clouds mwaka 2015 baada ya kuomba kupumzika aendelee na mishemishe zake siku ya kesho atakuwepo mje

Mama Mlezi wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Afariki Dunia

Image
Mama mlezi wa aliyekuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Bi Nuru binti Halfani Shomvi amefariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa akitibiwa asubuhi ya leo. Kupitia mtandao wa twitter, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akishukuru jamii kwa salamu za pole alizopokea amesema shughuli za msiba ziko nyumbani kwa marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo na maziko yatakuwa Bagamoyo mjini, kesho Jumatano Machi 8, 2017 saa 10 Alasiri. “Mama amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu, Mzee Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998. Mama yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee Halfani Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo”. Kauli ya Jakaya Kikwete Naye Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete ambaye ni mjukuu wa marehemu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho asubuhi ya leo. “Ndugu na marafiki nasikitika kuwatangazia

WAZIRI MBARAWA AWATAKA TEMESA KUONGEZA UJUZI UTENGENEZAJI WA VIVUKO.

Image
  Meneja Mradi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport inayojenga Kiuvko cha MV. Kazi, Bw. Major Songoro,   akitoa ufafanuzi wa mashine kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alipokagua Kivuko hicho jijini Dar es Salaam.   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akiangalia moja ya vifaa vilivyoko kwenye chumba cha kuendeshea kivuko katika kivuko cha MV. Kazi kinachojengwa jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kitakabidhiwa tarehe 15 Mwezi huu. Wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), Dkt. Musa Mgwatu.   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia),  akifafanua jambo kwa Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV Kazi ambacho kinatengenezwa jijini Dar es salaam na Kampuni ya Songoro Marine Transport.   Mafundi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport, wakiendelea na kazi ya

BOSI ALIYEMPA RC MAKONDA HEKARI 1500 AHOJIWA

Image
Mkurugenzi wa kampuni ya Azimio Housing Estate, Mohamed Ikbal, ambaye hivi karibuni alimgawia ardhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amehojiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka za Serikali. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha jana kwamba mfanyabiashara huyo aliitwa kwa ajili ya mahojiano, lakini aliachiwa kwa dhamana baada ya muda kuonekana hautoshi. “Alikuja na wakili wake, lakini ameachiwa kwa dhamana ataripoti siku nyingine (hakutaja siku),” alisema Sirro. “Anatuhumiwa kughushi nyaraka za Serikali na sasa upelelezi unaendelea.” Mfanyabiashara huyo inadaiwa kuwa aliripoti polisi jana saa tano asubuhi na kuhojiwa kabla ya kuachiwa kwa dhamana jioni. Kuhojiwa kwa Ikbal, ambaye kampuni yake iliwahi kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika miradi kadhaa tata ya ujenzi, kumekuja siku chache baada ya kumgawia Makonda eneo la ekari 1500 katika kitong

AIS MAGUFULI AZINDUA UWANJA WA NDEGEVITA WA KAMBI YA NGERENGERE, MOROGORO

Image
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli na Balozi wa China nchini Dkt wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017 Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017. Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli akijiandaa kufyatua risasi ya bastola kuashiria matumizi rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017 Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli na Balozi wa China nchini Dkt katika picha ya pamoja na viiongozi mbalimbali baada ya uzinduzi rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017. PICHA NA IKULU

MBUNGE WA ARUSHA MH GODBLES LEMA AFUNGUKA TENA,AFICHUA MAZITO

Image
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amesema hana kinyongo wala uadui na mtu yeyote kuhusu hatua ya serikali kumweka mahabusu kwenye gereza la Kisongo kwa muda wa miezi 4 kwa kukosa dhamana. Kauli hiyo aliitoa Jumapili hii mjini Arusha wakati akizungumza katika ibada ya kwenye Kanisa la Winners Chaple, ambapo alitoa sadaka na shukrani kwa Mungu na waumini wa kanisa hilo. Alisema amefurahi kwa sababu Mungu alimpa likizo muhimu kwa kumpendelea kwa kuwa mbunge wa kwanza kula Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya akiwa gerezani.“Nimeomba sana, nimewaombea sana nikiwa gerezani na sikuwa najua nina uwezo wa kuomba masaa manne ila nimemhubiri Mungu sana gerezani nimeombea taifa, viongozi, Bunge, Mahakama, Ofisi ya DPP na Rais Dk. Magufuli,” alisema.Aliongeza “Ukweli kabisa sina adui kwenye jambo hili na sina kinyongo kwenye jambo hili, ni mara ya kwanza nilimuona mke wangu akinitetea gerezani kwa hiyo mimi nilipendelewa kuliko ninyi na hamtakaa mlie Krismasi gerez

HATMA YA DHAMANA YA MBUNGE LEMA KUJULIKANA LEO JIJINI ARUSHA

Image
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe ( wa pili kutoka kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt. Vincent Mashinji ( Wa kwanza kulia), Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Edward Lowassa (Wa pili kushoto) na Waziri Mkuu Msaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Federick Sumaye wakiwa ndani ya Mahakama Kuu jijini Arusha, Leo Ijumaa 03/03/2017 ambapo kesi ya Mbunge wa Arusha, Mhe. Godbless Lema kuhusu dhamana yake.

IRENE UWOYA AMLIPUA WEMA SEPETU NA WENZAKE,AWAPA MAKAVU LIVE

Image
Baada ya kashikashi za hapa na pale ya wasanii wa bongo movie kuingia kwenye siasa huku Wema Sepetu akihamia CHADEMA na kusema anaidai CCM, swahiba wake, Batuli amekanusha. Wakati vita vya maneno vikiendelea, mwenzao, Irene Uwoya amewachana. Irene ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika maneno yenye busara ndani: Katika maisha siku zote ushauri unaruhusiwa kutolewa au kupokelewa… Lakin sio lazima mtu kupokea ushauri unaotolewa… Kila mtu anauhuru wakuamua kitu ambacho anahisi kinamfaa kwenye maisha sababu… Sazingine kwenye maisha Kuna sehemu inafika unacho jiskia kwenye moyo wako sio rahisi mtu mwingine kujiskia … Sasa ni mbaya sana kuishi kwa hisia… Ifikie Wakati tujitaidi kuheshimu hisia Za mtu… Lakin pia kunavitu vingine nazani Nivyema vkabaki kwa wausika wavinaowahusu…yani sio lazima kuongea kila kitu kwenye jamiii… Watu wanatamani sazingine kuskia vtu ambavyo wanahisi vinafaida kwa Jamaniii… Kunavitu vingine ukiongea havina maana.” Mfano mim ni CCM da

WATANO WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA

Image
Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata watuhumiwa watano kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya ikiwemo bangi kilo mia moja, mirungi kilo sitini, heroine kete tatu na vifungashio vya dawa hizo katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro, ikiwa ni jitihada za kuendeleza vita dhidi ya matumizi na uuzaji wa dawa hizo. Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo tofauti ya mkoa wa Morogoro ikiwemo wilaya za Mvomero, Morogoro manispaa na Kilombero,wakiwemo watuhumiwa waliokuwa wakisafirisha dawa hizo kwa magari ya abiria, basi la BM Coach huko Mkindo Turiani, na gari ndogo aina ya Hiace maeneo ya Kihonda, pamoja na pikipiki maarufu kama boda boda. Baadhi ya watuhumiwa waliohojiwa kuhusiana na dawa hizo, wamekuwa na majibu tofauti, wengi wakidai kutumwa na watu mizigo hiyo ikiwemo mirungi na bangi, ambapo aliyekuwa amebeba debe nne za bangi kwa kuficha ndizi mbichi juu ya kiroba kilichokuwa na mzigo huo

ALLY KIBA APOKEWA KISHUJAA, AISIMAMISHA JIJI LA DAR ES SALAAM NA VIUNGA VYAKE

Image
 Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika                  Mashabiki wa AlyKiba ambao walifika katika uwanja wa ndege wa JNA jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango kama wanavyoenekana pichani  Kiba kielekea kwenye gari maalum aliyoandaliwa mara baada ya kuzngumza na mashabiki wake  Aly Kiba akiwa na Meneja wake  Seven Mosha mara baa da ya kuingia katika gari hiyo maaalum  Ally Kiba akiwa katika mitaa ya Kariakoo huku akiwa amezunguskwa na mashabiki mbalimbali ambao walipata fursa ya kuona Tunzo yake ya Mtv base kama msanii bora wa kiume Afrika  Mashabikiw a Ally Kiba wakiwa wamezunguka gari ya msanii huyo katik

Waziri Nape: Sikupinga vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya bali nilishauri busara itumike

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa ufafanuzi juu ya kauli iliyonukuliwa ikionyesha kuwa alipinga vita dhidi ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Amedai kuwa hakupinga vita hiyo bali alitaka busara itumike kwa washukiwa. Waziri Nape alitoa ufafanuzi huo katika kipindi cha dakika 45 cha ITV, alipoulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho kutaka kujua kuhusu kauli yake iliyoonesha kupinga utaratibu uliotumika wa kuwakamata au kuwapata watuhumiwa wa dawa za kulevya. “Niseme kwanza ilitokea nilikuwa na mkutano na waandishi wa habari, ukienda leo ukanitaja Nape ukaniambia baada ya siku mbili njoo kituoni, hata kama nilikuwa na madawa ya kulevya nyumbani kwangu hivi unayakutaje?  'Kwasababu kwa vyovyote vile nitayachukua, ntayaficha, ntakuja kituoni ntaripoti utanibana ntakwambia twende nyumbani kwangu ukakague mnaenda mnakagua mnakuta hamna, si basi!  &q