RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI AWAMU YA KWANZA YA MIUNDOMBINU NA UTOAJI HUDUMA YA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT) JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wa kwanza kulia wavivuta kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakwanza (kulia) akivuta utepe kuashiria Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe