Posts

Yanga yashinda bao 1-0 dhidi ya Mo Bejeia

Image
Straika mpyawa Yanga, Obrey Chirwa (katikati) akiwatoka wachezaji wa Mo Bejaia. Kikosi cha Mo Bejaia wakipasha kabla ya mechi. Kikosi cha Yanga wakipasha kabla ya mechi. TIMU ya Yanga imeshinda bao 1-0 dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria katika Kombe la Shirikisho Afrika, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam  na kufikisha point 4.  Bao la Yanga limefungwa kipindi cha kwanza Dakika ya pili na Amissi Tambwe. Kikosi cha Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Said Juma ‘Makapu’ dk46, Mwinyi Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’/Kevin Yondan dk17, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na Deus Kaseke/Juma Mahadhi. MO Bejaia; Chamseddine Rahmani, Ismail Benettayeb, Faouzi Rahal, Sofiane Khadir, Soumaila Sidibe, Zakaria Bencherifa, Mohamed Yacine Athmani, Morgan Betorangal, Sofiane Baouali, Amar Benmelouka na Kamel Yesli.

VERA SIDIKA AELEZA SABABU NA KIASI ALICHOTUMIA KUONGEZA MATITI YAKE

Image
Mrembo maarufu kutoka Kenya,Vera Sidika ameweka wazi kuwa alifanya plastic surgery ili aweze kuwa na matiti makubwa. Vera aliyasema hayo akiwa kwenye mahojiano ya Tv na kipindi cha FNL cha EATV ambapo alieleza kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kuona sehemu zingine za mwili wake ni kubwa kasoro matiti,hivyo akaamua kutafuta mwili wenye uwiano. “Kipindi nakua kutoka utotoni na kuwa kijana,mwili wangu ulianza kuwa mkubwa na ukaanza kuwa mkubwa sehemu nyingine huku kwa juu nikawa kama nimenyimwa kidogo,halafu kwenye industry kama hollywood sio big deal,watu wanafanya surgery kama kawaida ila kwa Afrika ni kitu kipya..Nilifanyiwa surgery ya matiti,inaitwa boob job,nilikuwa nataka niwe na mwili wenye uwiano,nilifanyiwa Marekani mjini hollywood na iligharimu kama dola elfu 30” alifunguka vera sidika ambaye pia alidai kuwa uamuzi huo ulichangiwa na ukweli kwamba alitaka avutie zaidi kwenye show biz na kuongeza kuwa hela alizotumia kufanya plastic surgery zinarudi kutokan...

Fidel Castro Agonga Miaka 90

Image
Fidel Castro RAIS wa zamami wa Cuba na Kiongozi mwanamapinduzi, Fidel Castro anasherehekea kutimiza miaka 90 tangu kuzaliwa kwake. Fidel Castro alizaliwa Agosti 13, 1926  huko Birán nchini Cuba na aliyetawala Kisiwa hicho kwa zaidi ya miaka 50, hajaonekana hadharani kwa miezi mingi na bado haijabainika iwapo atajitokeza leo. April 19, 2011, Fidel Castro, kushoto, akinyanyua mkono wa mdogo wake, Rais wa Cuba, Raul Castro, wakati wa Mkutano wa Chama cha Congress, Havana, Cuba. Ingawa Cuba imebadilika sana tangu mdogo wake, Raul Castro achukue madaraka miaka nane iliyopita, na ushawishi wa Fidel umeshuka, bado anaenziwa sana na raia wengi wa Cuba. Raul alizaliwa mnamo June 3, 1931 huko huko Birán nchini Cuba Picha za Fidel Castro, kuanzia kushoto akiwa Havana Aprili 29, 1961 kuzungumza na wanahabari, Washington, D.C., Aprili 6, 2000 na Februari. 13, 2016. Hakuna hafla yoyote rasmi iliyopangiwa kufanywa, lakini Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, taifa mshi...

Kitwanga, JPM Wakutana Uso kwa Uso

Image
Rais John Magufuli jana alikutana ana kwa ana na rafiki yake, Charles Kitwanga ikiwa ni siku 80 baada ya kumvua cheo cha Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kosa la kuingia bungeni kujibu maswali akiwa amelewa. Wawili hao walikutana kwenye Jimbo la Misungwi ambako Rais alisimama akitokea Wilaya ya Sengerema ambako alihutubia wananchi. Rais alitengua uteuzi wa Kitwanga Mei 20, wakati sakata la utekelezwaji mbovu wa mkataba wa Sh37 bilioni baina ya Jeshi la Polisi na kampuni ya Lugumi Enterprises likivuma kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano. Lakini jana, hali ilionekana ya kikazi zaidi wakati Rais alipofika kwenye jimbo hilo. Kitwanga, ambaye ni mbunge wa Misungwi mkoani Mwanza, alitumia nafasi hiyo kukutana na Rais kwa mara ya kwanza hadharani, kuwasilisha kero za wananchi wake, hasa ya maji. Katika tukio hilo lililovutia hisia za waliokuwepo, Rais aliuthibitishia umma kuwa yeye na Kitwanga ni marafiki wa muda mrefu, alipokuwa akijibu ombi la mbunge huyo la kutaka Ser...

Njemba Avamia Makao Makuu ya Trump, Apanda Ghorofa 21 kwa Saa 3

Image
Polisi wakijitahidi kumtoa njemba huyo aliyepanda juu ya ghorofa. Njemba huyo katika haakati za kukwea jengo hilo la ghoofa 58. Akikazana kukwea. Hali ilivyokuwa Mashuhuda wakitahauki. Polisi wakijitahidi kumdhibiti Akitolewa na polisi NEW YORK: Njemba mmoja nchini Marekani aliyejiita kuwa ni mtafiti binafsi na shabiki wa Donald Trump, jana Agosti 10, 2016 alitumia masaa matatu kupanda jengo la mfanyabiashara huyo maaufu duniani ambaye pia ni mgombea urais wa nchi hiyo kwa tiketi ya Chama cha Republican lililopo jijini New York. Taarifa zimeeleza kuwa njemba huyo mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Virginia alitumia vifaa maalum kupanda ghorofa hilo lililojengwa kwa vioo ambalo pia ni Makao Makuu ya Kampeni za Bwana Trump na ndiyo Makao yake Makuu Kibiashaa kabla ya polisi kumtoa akiwa amefikia ghorofa ya 21 huku akiwa amechomwa vibaya na vioo vya jengo hilo. Trump anaishi kwenye ghorofa ya ya juu kabisa ya jengo hilo lakini kwa sasa an...

RAIS DKT. MAGUFULI AANZA ZIARA YAKE MKOANI MWANZA.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili akitokea Chato mkoani Geita. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wanakwaya wa UWT Kisima cha maji Chumvi mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza.     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu Mstaafu wa Shule ya Sekondari Sengerema Wilson Fumbuka Mbanga ambaye walifundisha naye shule hiyo tokea mwaka 1982-1985 mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara Sengerema Mkoani Mwanza.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wakazi wa Sengerema mkoani Mwanz...

WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMSHAMBULIA MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA BAADA YA KUANDIKA MANENO HAYA MTANDAONI

Image
Kitendo cha wanachama wa klabu ya Young Africans kumruhusu mwenyekiti wao, Yusuph Manji kuikodi klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 10 kinaendelea kuwagusa watu wengi na mmoja wapo ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye amefikia hatua ya kuandika ujumbe katika mitandao ya kijamii. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda ameandika “Unataka kujuwa kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na UTAJIRI MKUBWA WA MALIASILI tulizonazo? Soma Mkataba wa Yanga wanaosaini LEO” Baada ya kuweka picha hiyo wadau mbalimbali wa soka nchini wamekua wakianzika maoni yao katika ujumbe wa Makonda, wengine wakimtaka asizungumze mambo ya Young Africans, na wengine wakimtaka afanye kazi za serikali na aache kujihusisha na soka na mashabiki wa klabu hiyo nguli hapa nchini. Awali Makonda aliweka picha ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na kusema kuwa alikuwa na maswali 87 kwa kiongozi huyo wa Yanga lakini baada ya kutizama mahojiano aliyofanyiwa, aligundua kwamba kiongozi ...

Hukumu Kesi Ya Babu Tale Bofya Hapa!

Image
ILE kesi inayomkabili Meneja wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Babu Tale ya kusambaza na kuuza DVD za mawaidha ya Shehe Hamis Mbonde bila ridhaa yake imeahirishwa tena na Mahakama Kuu ya Kanda ya Dar es Salaam hadi Agosti 24, mwaka ambapo hukumu itatolewa. Akizungumza mbele ya mawakili na wahusika wa pande zote mbili leo asubuhi, Msajili wa Mahakama, Kayonza alianza kwa kutupilia mbali hoja ya mawakili wa upande wa Babu Tale, Robert Mkoba na Augustino Aluta iliyoomba kupewa muda zaidi kwa sababu ya mmoja kati ya mawakili wao (Paul Mgaya) ana udhuru na kwamba yupo jijini Arusha kwa semina. “Mawakili mnaosikiliza kesi hii kwa upande wa Tale mpo watano, siwezi kuruhusu tena kuahirishwa kwa kesi hii kisa mmoja hayupo. Agosti 24 itakuwa siku ya hukumu na kutekelezwa ambacho kipo na niwaombe wote muwepo,” alisema Kayonza. Awali kesi hiyo ilitakiwa itolewe hukumu Agosti 1 lakini kutokana na Mgaya kuumwa ilibidi kuahirishwa hadi leo (Agosti 10). Wakili wa ...

REAL MADRID NA SEVILLA WALIVYOTOANA JASHO KWENYE MCHEZO WA UEFA SUPER CUP USIKU WA KUAMKIA LEO

Image
Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos akishangilia huku akinyanyua kombe na wenzake baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa Super Cup baada ya kushinda 3-2 dhidi ya Sevilla huko Norway  Beki wa Real Madrid Dani Carvajal akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la tatu na ushindi dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa Uefa Super Cup. Sergio Ramos akiifungia Real Madrid goli la kusawazisha kwa kichwa na kufanya matokeo kuwa 2-2 dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa Uefa Super Cup, kabla ya kuibuka na ushindi ndani ya dakika 120.  Konoplyanka, ambaye hakuwa kwenye kiwango bora kwenye Michuano ya Euro 2016 na Ukraine, akifunga mkwaju wa penati na kuipa Sevila uongozi wa mabao 2-1.

Mzungu Dar Afumwa Live Akilawitiwa na Vijana 3

Image
  Mzungu akilawitiwa, OFM wamfumania. MWANDISHI WETU, WIKIENDA DAR ES SALAAM: Ushoga? Mzungu mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja lakini akijitambulisha kuwa ni raia kutoka nchini Italia, hivi karibuni alinaswa akiwa katika harakati za kulawitiwa na vijana watatu, Wikienda limeinyaka. Tukio hilo lililotafsiriwa kuwa linakwenda kinyume na msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu sheria za makosa ya kujamiina, lilijiri Agosti 4, mwaka huu, nyumbani kwa Mzungu huyo, Mikocheni jijini Dar es Salaam.   YALIANZA MALALAMIKO Awali, kijana mmoja alipiga simu kwenye ofisi za Global Publishers na kutaka msaada kutoka kwa kitengo maalum cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na kusema kuwa kuna Mzungu amekuwa akimtaka awapeleke vijana nyumbani kwake kwa ajili ya mambo yasiyopendwa na watu wengi na pia ni kinyume na msimamo wa serikali. Lakini atatoa mshiko wa nguvu.   Baada kudakwa na polisi, kupigwa pingu na kupelekwa kituoni. “J...