Hukumu Kesi Ya Babu Tale Bofya Hapa!
Akizungumza mbele ya mawakili na
wahusika wa pande zote mbili leo asubuhi, Msajili wa Mahakama, Kayonza
alianza kwa kutupilia mbali hoja ya mawakili wa upande wa Babu Tale,
Robert Mkoba na Augustino Aluta iliyoomba kupewa muda zaidi kwa sababu
ya mmoja kati ya mawakili wao (Paul Mgaya) ana udhuru na kwamba yupo
jijini Arusha kwa semina.
“Mawakili mnaosikiliza kesi hii kwa
upande wa Tale mpo watano, siwezi kuruhusu tena kuahirishwa kwa kesi hii
kisa mmoja hayupo. Agosti 24 itakuwa siku ya hukumu na kutekelezwa
ambacho kipo na niwaombe wote muwepo,” alisema Kayonza.
Awali kesi hiyo ilitakiwa itolewe hukumu Agosti 1 lakini kutokana na Mgaya kuumwa ilibidi kuahirishwa hadi leo (Agosti 10).
Wakili wa Shehe Mbonde, Mwesiga Muhingo
akitolea ufafanuzi kuahirishwa kwa kesi hiyo alisema, siku hiyo ya
hukumu iliyotolewa na msajili ni kuhusu kutekeleza yale ambayo mahakama
iliagiza ambayo ni Tale kumlipa mteja wao (Shehe Mbonde) Sh. milioni 250
ama kwenda jela.
Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL
Comments
Post a Comment