Fidel Castro Agonga Miaka 90
RAIS wa zamami wa Cuba na Kiongozi mwanamapinduzi, Fidel Castro anasherehekea kutimiza miaka 90 tangu kuzaliwa kwake.
Ingawa Cuba imebadilika sana tangu mdogo
wake, Raul Castro achukue madaraka miaka nane iliyopita, na ushawishi
wa Fidel umeshuka, bado anaenziwa sana na raia wengi wa Cuba. Raul
alizaliwa mnamo June 3, 1931 huko huko Birán nchini Cuba
Hakuna hafla yoyote rasmi iliyopangiwa
kufanywa, lakini Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, taifa mshirika wa
karibu wa Cuba, amewasili Havana kushiriki katika sherehe hizo.
March 21, 2016 rais wa Cuba Raul Castro na rais wa marekani, Barack Obama.
Mtengenezaji sigara maarufu raia wa Cuba ametayarisha msokoto mrefu zaidi wa sigara duniani kwa heshima ya Castro.
Msokoto huo una urefu wa mita 90.
Comments
Post a Comment