VERA SIDIKA AELEZA SABABU NA KIASI ALICHOTUMIA KUONGEZA MATITI YAKE


Mrembo maarufu kutoka Kenya,Vera Sidika ameweka wazi kuwa alifanya plastic surgery ili aweze kuwa na matiti makubwa.
Vera aliyasema hayo akiwa kwenye mahojiano ya Tv na kipindi cha FNL cha EATV ambapo alieleza kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kuona sehemu zingine za mwili wake ni kubwa kasoro matiti,hivyo akaamua kutafuta mwili wenye uwiano.

“Kipindi nakua kutoka utotoni na kuwa kijana,mwili wangu ulianza kuwa mkubwa na ukaanza kuwa mkubwa sehemu nyingine huku kwa juu nikawa kama nimenyimwa kidogo,halafu kwenye industry kama hollywood sio big deal,watu wanafanya surgery kama kawaida ila kwa Afrika ni kitu kipya..Nilifanyiwa surgery ya matiti,inaitwa boob job,nilikuwa nataka niwe na mwili wenye uwiano,nilifanyiwa Marekani mjini hollywood na iligharimu kama dola elfu 30” alifunguka vera sidika ambaye pia alidai kuwa uamuzi huo ulichangiwa na ukweli kwamba alitaka avutie zaidi kwenye show biz na kuongeza kuwa hela alizotumia kufanya plastic surgery zinarudi kutokana na madili anayopata kwenye show biz kutokana na muonekano wake ikiwemo kuonekana kwenye videos za wasanii,magazines na special appearance kwenye clubs.

Comments

Popular posts from this blog