Mzungu Dar Afumwa Live Akilawitiwa na Vijana 3
Mzungu akilawitiwa, OFM wamfumania.
MWANDISHI WETU, WIKIENDA
DAR ES SALAAM: Ushoga? Mzungu
mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja lakini
akijitambulisha kuwa ni raia kutoka nchini Italia, hivi karibuni
alinaswa akiwa katika harakati za kulawitiwa na vijana watatu, Wikienda
limeinyaka.
Tukio hilo lililotafsiriwa kuwa
linakwenda kinyume na msimamo wa Serikali ya Tanzania kuhusu sheria za
makosa ya kujamiina, lilijiri Agosti 4, mwaka huu, nyumbani kwa Mzungu
huyo, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
YALIANZA MALALAMIKO
Awali, kijana mmoja alipiga simu kwenye
ofisi za Global Publishers na kutaka msaada kutoka kwa kitengo maalum
cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ na kusema kuwa kuna Mzungu amekuwa
akimtaka awapeleke vijana nyumbani kwake kwa ajili ya mambo yasiyopendwa
na watu wengi na pia ni kinyume na msimamo wa serikali. Lakini atatoa
mshiko wa nguvu.
Baada kudakwa na polisi, kupigwa pingu na kupelekwa kituoni.
“Jamani kuna Mzungu anatushangaza
kidogo. Ameniambia niwatafute vijana pamoja na mimi mwenyewe twende
nyumbanai kwake. Anasema anataka mapenzi yale yanayokemewa na serikali
yetu ya Tanzania, mimi nahisi anatakiwa kukomeshwa kama ni tabia yake,”
alisema mtoa habari huyo.
BAADA YA TAARIFA
Kufuatia madai hayo, Wikienda
lilijipanga kufanya uchunguzi kupitia OFM lengo likiwa ni kujiridhisha
kuhusu maneno ya mtoa habari huyo.
Lilikutana na kijana huyo (jina tunalo)
ambapo walitafutwa vijana wengine wawili akiwemo OFM mmoja, jumla wakawa
watatu na kumkubalia Mzungu huyo.
KIASI CHA PESA
Katika mazungumzo yake na Mzungu huyo,
kijana huyo ambaye ndiye kinara na wenzake waliahidiwa kupewa shilingi
laki moja (100,000) kila mmoja kama malipo ya shughuli hiyo ambayo wao
haikuwa kwenye ratiba ya siku.
OFM POLISI
Ili kukamilisha uchunguzi wake, OFM
ilitinga Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar ili kutoa
taarifa za madai ya uwepo wa Mzungu huyo na ‘michezo’ ambayo anadaiwa
kuifanya Bongo.
Baada ya kujieleza kituoni hapo, askari
wa kituo hicho walitoa ushirikiano mkubwa kwa kufungua jalada lenye
namba KJN\ RB\8514\16 TAARIFA na kumtaka kijana huyo kutoa ushirikiano
kwa OFM.
ENEO LA TUKIO
Baada ya hapo, safari ya kwenda nyumbani
kwa Mzungu huyo ilianza huku kijana huyo akiwa anawasiliana naye kwa
taarifa kuwa, wapo njiani.
MAZINGIRA YA NYUMBA
Ugumu ulikuwepo kwenye kuingia ndani ya
nyumba hiyo kwani, ilizungukwa na fensi ya ukuta wa matofali, akiishi
peke yake. Mzungu huyo aliwaingiza vijana hao watatu waliokusudiwa huku
OFM wengine na askari polisi mmoja wakijibanza sehemu kusubiri.
NDANI YA CHUMBA
Baada ya kuingia chumbani, OFM alianza
kupiga picha kwa siri, aliweza kumfotoa Mzungu huyo akiwa na wenzake
katika mapozi mbalimbali.
Hata hivyo, OFM aligoma kushiriki tukio
hilo jambo linalodaiwa kumkera mtuhumiwa huyo na kuamua kuwafukuza wote
ndipo songombingo kubwa ilizuka ambapo Mzungu huyo aliwataka waondoke
wote.
Akiwa anawatoa nje, ndipo OFM wa nje na
askari mmoja walimnasa Mzungu huyo kwa mapicha na kumfunga pingu ambapo
kazi ya kumpeleka kituoni ilikuwa chini ya polisi huyo. Wikienda
linaendelea kufuatilia ili kujua kilichoendelea.
MAKONDA APONGEZWA
Hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda alitoa kauli ya kupambana na watu wanaojihusisha na
vitendo vya ushoga akisema ni kinyume na msimamo wa serikali.
Wakati wa kumkamata Mzungu huyo, baadhi
ya watu waliokuwa kwenye nyumba za jirani walimpongeza Makonda kwa tamko
lake hilo wakisema lililenga kuiweka jamii ya Dar es Salaam katika
maadili ya Kimungu.
“Jamani huyo Mzungu aende tu. Juzijuzi
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda alitoa tamko la kupinga ushoga, si jadi
yetu jamani! Makonda aliliona hilo ndiyo maana Mungu alimtumia aseme
vile, tunampongeza ila mwambieni alifanyie kazi na hili,” alisema mkazi
mmoja bila kutaja jina lake.
Juzi, Wikienda lilimpigia simu Makonda
kwa lengo la kumpongeza kwa kauli yake hiyo lakini pia kumjulisha hili
la Mzungu lakini simu yake mara zote ilikatwa hali iliyoashiria kuwa,
alikuwa kwenye kikao au tukio ambalo asingeweza kuongea.
Comments
Post a Comment