WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMSHAMBULIA MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA BAADA YA KUANDIKA MANENO HAYA MTANDAONI
Kitendo cha wanachama wa klabu ya Young Africans kumruhusu mwenyekiti wao, Yusuph Manji kuikodi klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 10 kinaendelea kuwagusa watu wengi na mmoja wapo ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye amefikia hatua ya kuandika ujumbe katika mitandao ya kijamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Makonda ameandika “Unataka kujuwa kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na UTAJIRI MKUBWA WA MALIASILI tulizonazo? Soma Mkataba wa Yanga wanaosaini LEO”
Baada ya kuweka picha hiyo wadau mbalimbali wa soka nchini wamekua wakianzika maoni yao katika ujumbe wa Makonda, wengine wakimtaka asizungumze mambo ya Young Africans, na wengine wakimtaka afanye kazi za serikali na aache kujihusisha na soka na mashabiki wa klabu hiyo nguli hapa nchini.
Awali Makonda aliweka picha ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na kusema kuwa alikuwa na maswali 87 kwa kiongozi huyo wa Yanga lakini baada ya kutizama mahojiano aliyofanyiwa, aligundua kwamba kiongozi huyo bado hajaelewa ni kitu gani kinaendelea klabuni
Comments
Post a Comment