Posts

Taarifa za ndani ya familia… Diamond ‘mchafu’

Image
Diamond Platnumz Imelda Mtema na Musa Mateja Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amejikuta akiwatibua baadhi ya ndugu zake huku wengine wakimuita mchafu kutokana na kitendo cha kumpachika mimba mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ kisha kuwepo madai kuwa ‘amewajaza’ pia mamodo Hamisa Hassan ‘Mobeto’ na Irene Hilary ‘Lynn’. Mmoja wa ndugu wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, familia imeshtushwa na madai kuwa kijana wao huyo mbali na kwamba Zari a.k.a Mama Tiffah ni mjamzito, amewapa mimba tena Mobeto na Lynn.   Zari. ILIKUWAJE? Miezi kadhaa nyuma, yaliibuka madai kuwa Zari ni mjamzito lakini Diamond amekuwa mgumu kulizungumzia hilo licha ya hivi karibuni mazazi mwenziye huyo kutundika picha akionesha kitumbo chake kilichodhihirisha kuwa ndani yake kuna kiumbe. Lynn LYNN NAYE Huku mashabiki wa Zari ‘Team Zari’ wakionesha furaha ya staa wao ‘kumshika’ mwanamuziki huyo kwa kumbebea ujauzito mwingine, zikaibuka taarifa

Ray C full kicheko

Image
MSANII mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya aliye katika majaribu makubwa ya matumizi ya madawa ya kulevya, hivi sasa anadaiwa kuwa full kicheko kufuatia mabadiliko makubwa ya afya yake tangu alipoanza kupata matibabu katika kituo cha wahanga wa ‘sembe’, Sober House kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani. Kwa mujibu wa bosi wa kituo hicho, Karim Bhanji, Ray C hivi sasa yupo vizuri tofauti na zamani na kwamba kwa jinsi anavyoendelea, hali yake inazidi kutengemaa. “Unajua tatizo kubwa kwa Ray C ilikuwa kwamba alikuwa anapatiwa matibabu bila uangalizi wa kutosha. Ingawa alikuwa akinywa dawa, lakini kilichokuwa kinatokea ni kuwa anakwenda Mwananyamala kunywa dawa halafu anarudi nyumbani, huko mtaani anakutana tena na watu walewale anaendelea kutumia. “Lakini kwa kuja hapa, baada ya dawa anadhibitiwa, hatoki hivyo hapati nafasi ya kujaribu tena kutumia unga, nina imani hali yake itaimarika kadiri muda unavyoenda,” alisema Bhanji na kuongeza kuwa akiwa kituoni, Ray C amesh

Tundu Lissu Akamatwa na Polisi… Msigwa Ahutubia Iringa

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa na polisi muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Ikungi, Singida. Wakati Lissu akiwa mikononi mwa polisi, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa jana alifanya mkutano wa hadhara na kusema hakuna wa kumpangia cha kuzungumza kwenye mikutano yake. Kukamatwa kwa Lissu  Lissu, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema ndiye aliyetoa taarifa za kukamatwa kwake kwenye mtandao akisema: “Wakubwa sana salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida. ” Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer (RCO) wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander (RPC) Singida nikamatwe apparently (dhahiri) kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam.

Wabunge 3 kesi ya rushwa mil.30/- waachiwa

Image
Kangi Lugola, Mbunge wa Mwibala. MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewaachia huru wabunge watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya kuomba rushwa ya Sh milioni 30. Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage aliwaachia huru washitakiwa hao baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), kuwasilisha hati ya kuwafutia mashitaka. Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibara, Mhe. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero Mhe.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa, Mhe.Victor Mwambalaswa. Wabunge hao na majimbo yao katika mabano ni Kangi Lugola wa Mwibara mkoani Mara maarufu kama ‘Nyoka wa Shaba,’ Suleiman Saddiq ‘Murad’ (Mvomero – Morogoro) na Victor Mwambalaswa (Lupa – Songwe). Awali Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi akisaidiwa na Wakili Emmanuel Jacob kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), waliieleza mahakama kuwa kesi hiyo imetajwa kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali. Kishenyi alidai

MCHUNGAJI AFARIKI BAADA YA KUFUNGA SIKU 30 AKITAKA KUVUNJA REKODI YA YESU

Image
AFRIKA KUSINI: Mchungaji mmoja amefariki baada ya kufunga usiku na mchana siku 30 akitaka kuvunja rekodi ya Yesu aliyefunga kwa siku 40. Mchungaji huyo aliondoka nyumbani kwake na kuelekea nyikani kwa ajili ya kufunga na kuomba, huku akiweka nia kwa Mungu ya kujitenga na anasa za ulimwengu.

Breaking News: Evans Aveva akamatwa na Takukuru, pesa za Okwi zatajwa

Image
Rais wa Klaabu ya Simba, Evans Aveva anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru). Taarifa zinaelezwa kuwa Takukuru wanamshikilia Aveva kwa tuhuma za rushwa ingawa haijaelezwa ni tuhuma zipi. Habari za uhakika zinaeleza, Aveva amekamatwa jana na amelala katika moja ya vituo vya polisi jijini Dar es Salaam. Saa chache baada ya Evans Aveva kushikiliwa na Takukuru, kumeibuka sababu kadhaa ambazo zinazungumzwa kuwa ni chanzo. Kumekuwa na taarifa ambazo si rasmi kuwa Aveva aliingiza fedha za Okwi zaidi ya Sh milioni 450 kwenye akaunti yake binafsi kuhofia zichukuliwe na TRA kwa kuwa Simba inadaiwa. Simba inadaiwa zaidi ya Sh milioni 650, hali hiyo imesababisha kuonekana kama vile alikuwa akikwepa kodi. Malipo ya fedha hizo, zaidi ya Sh milioni 450 ni malipo ya ununuzi wa mshambuliaji Emmanuel Okwi ambazo Simba ilimuuza katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia. Taarifa hizo zimeeleza kwamba waliamua kuzificha ili waweze kujenga uw

MANJANO FOUNDATION WAKUTANA NA WANAWAKE WA KUJADILI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI

Image
Meneja Rasilimali watu Kutoka Benki ya NMB Dada   Edith Mwiyomela   akitoa Mada kwa Wanawake Wa Mkoa wa Dar es Salaam  walionufaika na Mradi Kutoka Taasisi ya Manjano waliokutana kujadili na Kuangalia namna ya Kutatua changamoto wanazokutana nazo kwenye Biashara yao ya Upambaji na Uuzaji wa Vipodozi, Ambapo wameaswa Kuwafanya Kazi kwa Bidii,kuwa na Nidhamu na Pia kuweka akiba Pamoja na Kuwa na uvumilivu kwenye kazi zao za kila siku ili kuweza  Kufikia Malengo waliyojiwekea.    Washiriki wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali kwenye mkutano huo Afisa Mtendaji Mkuu wa wa Shear Illusions na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser (kushoto) Akimsiliza Mmoja wa Wanawake aliyekuwa akieleza namna anavyopambana na Changamoto zinzowakabili Wanawake wengi kwenye  Biashara zao.Kwa Upande Mwingine Mama Shekha Nasser Amawataka Wanawake   waliohudhuria namna gani ya kuweza kutofautisha faida na mtaji. Biashara nyingi za kina mama hufa baada

Lowassa, Sumaye Hatarini Kushtakiwa

Image
KAMISHNA wa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma, Jaji mstaafu Salome Kaganda, amewataka viongozi wastaafu kuacha kutoa siri za serikali kwani bado wapo kwenye kiapo na kuonya wakikaidi, watachukuliwa hatua. Bila kuwataja kwa majina wala siri walizotoa, Jaji Kaganda alisema: “Tusiweke maslahi binafsi mbele kwa kutoa siri za mikataba kwa kuangalia manufaa binafsi, jambo ambalo limelifikisha taifa pabaya. Viongozi wastaafu wafunge midomo yao kwani bado wako ndani ya kiapo hata kama wamestaafu.” Waziri mstaafu, Frederick Sumaye. Jaji Kaganda alisema wapo wastaafu ambao wameingia kwenye nyanja mbalimbali ikiwamo siasa, ambapo hutumia majukwaa kutoa siri za serikali na kwamba wanapaswa kukumbuka wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria. Jaji Kaganda aliyasema hayo juzi alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Runinga cha ITV. Kwa siku za karibuni, mbali na watumishi wa umma walioacha kazi zao na kushiriki siasa ikiwa ni pamoja na ku

Mwalimu aliyetuhumiwa kujihusisha kimapenzi na wanafunzi auawa

Image
MWALIMU Daniel Msalika (42) wa shule ya msingi Nyasosi, wilayani Bariadi, mkoa wa Simiyu amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikokuwa amelazwa akitibiwa majeraha. Majeraha hayo yalitokana na kushambuliwa na baadhi ya wananchi kwa madai ya kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wa kike wa shule hiyo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga aliwaeleza waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa mwalimu huyo alifariki dunia Julai 31 mwaka huu saa nane usiku. Kamanda Lyanga alisema kuwa siku ya tukio Julai 27 mwaka huu saa 6.30 usiku, wananchi hao ambao idadi yao haijafahamika, walivamia nyumba ya mwalimu huyo baada ya kupata taarifa kuwa kuna mwanafunzi ambaye amelala nyumbani kwake, jambo ambalo halikuwa la kweli. “Wananchi hao walipata taarifa ya kuwa nyumbani kwa mwalimu kuna mwanafunzi ambaye amelala humo hivyo walimvamia kwa kuvunja mlango na kuanza kumshambulia kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi na kumsababishia majeraha makubwa s

Wastara agombewa kuosha magari

Image
Wastara Juma akiwa bize kuosha gari. Na Dustan Shekidele, RISASI Mchanganyiko MOROGORO: Msanii maarufu wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, mwishoni mwa wiki iliyopita aligeuka gumzo wakati wa harambee maalum ya kuchangia madawati kwa njia ya kuosha magari iliyofanyika mjini hapa, ambapo wateja wengi walikuwa wakimgombea awaoshee magari yao. Harambee hiyo iliyofanyika kwenye kumbi za Samaki Sport na Nyumbani park, iliandaliwa na kundi la wanawake wanaojiita Best Friends Forever (BFF) ambao waliosha magari ya wateja kwa lengo la kukusanya fedha za madawati kuunga mkono harakati za Rais Dk. John Pombe Magufuli kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini. Mwandishi wetu alimshuhudia Wastara akiwa bize kuosha gari la mheshimiwa diwani wa Kata ya Mafiga, Spear Komanya huku wateja wengine nao wakimsubiri amalize kisha aoshe yao, jambo lililomfanya muda wote aonekane kuwa bize. “Leo tumeamua kuja hapa kwa sababu watu wengi wenye magari huja kustarehe hapa kwa

Kingunge azua hofu

Image
  Na Mwandishi Wetu, RISASI Mchanganyiko DAR ES SALAAM: Ukimya wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru umezua hofu kubwa baada ya kutoonekana katika matukio muhimu tangu alipojiondoa kutoka Chama Cha Mapinduzi mwishoni mwa mwaka jana. Kingunge alijiondoa ndani ya chama tawala, muda mfupi baada ya kukatwa kwa jina la Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kiongozi huyo kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambako alipewa fursa ya kuwania urais wa Tanzania, akichuana na aliyeibuka mshindi, Dk John Pombe Magufuli. “Huyu mzee yuko wapi jamani, maana yupo kimya sana, wenzake wote tunawaona na kuwasikia, wengine wanarudi CCM, wengine wanaonekana katika matukio, lakini yeye haonekani kabisa, anatupa hofu kwa kweli,” alisema msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Giggs, akitokea mkoani Mtwara. Msomaji mwingine, Samson Bilal wa Tabora, alisema kimya cha mwanasiasa huyo huenda kikawa na mshindo mkuu, kwani ukimya wake umekuwa siyo

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 03.08.2016

Image

EXCLUSIVE…MWANA DADA WA CHADEMA JOYCE KIRIA AMKATAZA MUMEWE KUSHIRIKI KAMPENI YA UKUTA.

Image
HIVI NDIYO ALIVYO ANDIKA KUPITIA MTANDAO WAKE WA FACEBOOK Nimeshamuomba sana shemeji yenu asome alama za nyakati jamani..Mkuu wa Kaya wa sasa kwa kweli hapanaaaaa wasimshike sharubu pls…. Hii UKUTA uuuuuwiiii nimemwomba jamani waipige chini watafute njia nyingine ya kumaliza migogoro ya kisiasa . . Kinamama wenzangu Hasa WAKE wa hawa wanaUKUTA pls tuwashauri waume zetu jamani tusisubiri mambo yaharibike kisha ndo tuanze kulia wakati tunaweza kuwazuia wasifanye jazba jamaniii… Hats kwenye nyumba hamuwezi wote kuwa wa babe jamani lazima mmoja awe chini jamaniii … . . Kiukweli wamefanya kazi kubwa nzuri katika Taifa hili na mbinu zao zilifanikiwa sana kwa serikali iliyopita kwa sababu Dady alikuwa hana neno mkwere wa watu, anawachekea na kuwapa nafasi ya kuwasikiliza na juice wanapewa, lakini sasaivi uuuuuuwiiiii wapunguze spidi na wasome sana mchezo, HUU MCHEZO HAUHITAJI HASIRA huyu BABA hacheki jamaniiiii .. Wasimjaribu jamaniiiii . . Yaani ki