Ray C full kicheko

Kwa mujibu wa bosi wa kituo hicho, Karim
Bhanji, Ray C hivi sasa yupo vizuri tofauti na zamani na kwamba kwa
jinsi anavyoendelea, hali yake inazidi kutengemaa.

“Lakini kwa kuja hapa, baada ya dawa
anadhibitiwa, hatoki hivyo hapati nafasi ya kujaribu tena kutumia unga,
nina imani hali yake itaimarika kadiri muda unavyoenda,” alisema Bhanji
na kuongeza kuwa akiwa kituoni, Ray C ameshaanza kuandika baadhi ya
mistari ya Bongo Fleva.
Ray C alipelekwa katika kituo hicho na
wasamaria wema Juni 18, mwaka huu, baada ya video kusambaa mitandaoni,
ikimuonesha akiokolewa na polisi baada ya kudaiwa kutaka kujidhuru
kutokana na kuzidiwa na matumizi ya madawa ya kulevya.
Kituo hicho cha Sober House pia kiliwahi kumpokea Mbongo Fleva mwingine, Chid Benz ambaye hata hivyo hakukaa kwa muda mrefu.
Comments
Post a Comment