Taarifa za ndani ya familia… Diamond ‘mchafu’

dimaond.jpgDiamond Platnumz
Imelda Mtema na Musa Mateja
Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amejikuta akiwatibua baadhi ya ndugu zake huku wengine wakimuita mchafu kutokana na kitendo cha kumpachika mimba mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ kisha kuwepo madai kuwa ‘amewajaza’ pia mamodo Hamisa Hassan ‘Mobeto’ na Irene Hilary ‘Lynn’.
Mmoja wa ndugu wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, familia imeshtushwa na madai kuwa kijana wao huyo mbali na kwamba Zari a.k.a Mama Tiffah ni mjamzito, amewapa mimba tena Mobeto na Lynn.
ZARII 
Zari.
ILIKUWAJE?
Miezi kadhaa nyuma, yaliibuka madai kuwa Zari ni mjamzito lakini Diamond amekuwa mgumu kulizungumzia hilo licha ya hivi karibuni mazazi mwenziye huyo kutundika picha akionesha kitumbo chake kilichodhihirisha kuwa ndani yake kuna kiumbe.
lynnLynn
LYNN NAYE
Huku mashabiki wa Zari ‘Team Zari’ wakionesha furaha ya staa wao ‘kumshika’ mwanamuziki huyo kwa kumbebea ujauzito mwingine, zikaibuka taarifa nyingine kuwa, modo wa Wasafi Classic Baby (WCB) Lynn naye ana mimba ya jamaa huyo.
Ikadaiwa kuwa, kubeba ujauzito kwa Lynn kumekuja baada ya yeye na Diamond kuwa kwenye uhusiano wa siri huku mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akidaiwa kujua kila kitu na kubariki ujio wa mjukuu mwingine.
mobetoMIMBA YA MOBETO
Katika kile kilichoonesha kuwachefua baadhi ya wanandugu, hivi karibuni yakaibuka madai kuwa, mwanamitindo Mobeto naye ana mimba na mhusika ni baba Tiffah.
Taarifa hizo zimeonesha kuwashitua wengi akiwemo mama mzazi wa modo huyo, Shufaa Lutigunga ambaye alipoongea na mwandishi wetu alisema kuwa, amezishangaa ila anayeweza kueleza ukweli ni Mobeto.
Jitihada za kumpata modo huyo ili kuzungumzia madai hayo hazikuzaa matunda licha ya kwamba aliwahi kuongea na gazeti hili na kukanusha madai yaliyokuwa yamezagaa kuwa anatoka na Diamond.
FAMILIA YA DIAMOND ‘YAMAINDI’
Kufuatia madai hayo, ndugu wa karibu wa Diamond aliyeongea na gazeti hili alisema kuwa, hivi karibuni familia ilikaa kikao kujadili mambo ya kifamilia lakini pia wakaonesha kukasirishwa na taarifa ya Diamond kuwapachika mimba wasichana watatu.
“Hilo la madai kuwa Diamond amewapa mimba wanawake watatu licha ya kwamba hatuna uhakika nazo, zimetuchefua sana, zimetufanya tumuone Diamond ni mchafu au kwa maana nyingine ni mchafuzi.
“Nasema hivi kwa sababu, haiwezekani iwe amempa mimba Zari halafu wakati huohuo awe amempa tena Lynn na Mobeto, sisi kama familia tutaficha wapi nyuso zetu wakijifungua?
“Ishu hiyo imemfanya kila mtu kwenye familia awe muoga, kwani pamoja na hayo yote kutokea, kubwa wanalohofia ni namna watakavyomwangalia Zari (wifi yao), sasa wakijifungua sijui watamjibu nini au wataweka wapi sura zao.
“Hapa ninavyokwambia mama Diamond na Esma hawaongei vizuri na Zari kufuatia kuendelea kuwahisi wao ndiyo kikwazo kikubwa cha kumuunganisha Diamond na warembo hao,” kilidai chanzo hicho.
DIAMOND HUYU HAPA
Gazeti hili baada ya kupenyezewa taarifa hizo lilimtafuta Diamond ili kumpa nafasi ya kulizungumzia kinagaubaga suala hilo, alipopatikana alisema kwamba yote yanayozungumzwa ni maneno ya watu na hakuna hata moja la kweli.
“Hakuna hata moja la ukweli, mwenyewe najionea kwenye mitandao kama nyinyi, kwani ‘social network’ kila mmoja ana uhuru wake wa kuongea anachokiwaza na siwezi kuwafuata na kuwauliza.
“Kwa hilo sina la kuongea zaidi maana naona ni mambo ya kipuuzi tu ambayo siwezi kuyapatia nafasi yoyote kwangu, naona tuachane nayo tu,” alisema Diamond.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Diomond amekuwa na skendo kibao za ku-date na wasichana mbalimbali wakiwemo mastaa ambapo mbali na Zari, Mobeto na Lyn, jamaa huyo aliwahi pia kutoka na Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Jacqueline Wolper, Upendo Mushi, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Aunt Ezekiel na wengineo

Comments

Popular posts from this blog