Tundu Lissu Akamatwa na Polisi… Msigwa Ahutubia Iringa
Mbunge
wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amekamatwa na polisi muda
mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Ikungi,
Singida.
Wakati Lissu akiwa mikononi mwa polisi, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji
Peter Msigwa jana alifanya mkutano wa hadhara na kusema hakuna wa
kumpangia cha kuzungumza kwenye mikutano yake.
Kukamatwa kwa Lissu
Lissu, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema ndiye aliyetoa taarifa za kukamatwa kwake kwenye mtandao akisema: “Wakubwa sana salaam. Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi Singida.
” Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki. Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer (RCO) wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander (RPC) Singida nikamatwe apparently (dhahiri) kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam.

“Kwa hiyo niko nguvuni na
ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya wanakotakiwa kunipeleka. It’s likely
(inawezekana) nitasafirishwa Dar usiku huu. In fact (hakika) ni usiku
huu kwa taarifa za sasa hivi. Kwa vyovyote itakavyokuwa, there’s no
turning back. There’s no shutting up (hakuna kurudi nyuma, hakuna
kunyamaza).
“Nitapambana kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote
nitakapokuwa, whether in freedom or in jail (niwe huru au jela)… Aluta
continua!. “
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alithibitisha kukamatwa kwa Lissu lakini alikataa kutoa sababu za hatua hiyo.
Chadema jana jioni ilitoa taarifa kuhusiana na kukamatwa kwa Lissu ikisema: “Tunaweza kuthibitisha kwa vyombo vya habari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama Mh. Tundu Lissu anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Singida kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.”

Taarifa hiyo iliyotolewa na Ofisa
Habari wa Chadema, Tumaini Makene ilibainisha kuwa Polisi walimkamata
jana jioni baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara alioufanya Ikungi
jimboni kwake na kueleza kuwa viongozi wa chama hicho mkoani humo
walikuwa polisi kuhakikisha anapata haki zake kama inavyostahili na
kwamba ofisi ya katibu mkuu inafuatilia kwa ukaribu kujua sababu hasa ya
kushikiliwa kwake na kutoa msaada wa haraka kadri itakavyohitajika.
Lissu amekuwa kwenye misukosuko na
Jeshi la Polisi mara kadhaa na kwa siku za karibuni alikamatwa na
kufikishwa mahakamani akituhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kwenye
gazeti la Mawio.
Sambamba na kesi hiyo, Lissu
alikamatwa na polisi kwa madai ya kutoa maneno ya uchochezi baada ya
kupata dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Msimamo wa Msigwa
Mkoani Iringa, Msigwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kwanza wa kibunge tangu alipochaguliwa uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa, alisema hakuna wa kumpangia hoja za kuzungumza kwenye mikutano yake.

Juzi, mbunge huyo alipewa barua na
Jeshi la Polisi iliyoeleza kuwa imempa kibali cha kufanya mikutano hiyo,
lakini ikimuwekea masharti mbalimbali likiwamo la kutozungumzia
viongozi wengine na badala yake ajikite kwenye shughuli za maendeleo na
kuchukua maoni ya wananchi anaowawakilisha.
Pia, alitakiwa kuhakikisha kuwa hakuna
mtu kutoka nje ya Mkoa wa Iringa au eneo lolote lililo nje ya mamlaka
atakayeruhusiwa kuzungumza.
Lakini jana akihutubia alisema: “Ninaona watu wote mna nyuso za
hofu na mimi nimekuja kuwaondoa hofu …hakuna mtu mwenye mamlaka ya
kunipangia cha kuzungumza, sipo hapa kwa matakwa ya polisi … mimi nipo
kwa matakwa ya kisheria na ninazungumza kwa mamlaka mliyonipatia.
“Pia Katiba inaeleza wazi mad raka
na kinga ya Mbunge… mbunge anayo haki ya kuitisha na kufanya mkutano wa
hadhara kwa mjibu wa sheria.”
Kuhusu Rais kuzuia mikutano ya vyama
vya siasa, Msigwa alisema hakubaliani na hatua hiyo kwa madai kuwa
kufanya hivyo ni ukiukaji wa Katiba ya nchi na Sheria ya Vyama vya Siasa
ya mwaka 1992 ambavyo nchi inayoongozwa chini ya utawala wa
kidemokrasia inapaswa kuvifuata.
“Ninamuunga mkono na ninampongeza
Rais John Magufuli kwa kupambana na ufisadi, anapinga rushwa… lakini
siungani naye kwa kitendo chake cha kukandamiza demokrasia nchini na
niwaombe wananchi wa Iringa kuungana na mimi kumpinga mtu anayekandamiza
demokrasia nchini,” alisema.
Kuhusu Serikali kuhamia Dodoma, mbunge
huyo ambaye pia ni waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje, alikosoa
uamuzi huo akisema hajawahi kuona katika mipango yote iliyowasilishwa na
Serikali bungeni inayoelekeza hilo.
“Serikali ilileta mpango wake wa
miaka mitano, mwaka mmoja na Bajeti, hivi vyote vinaletwa bungeni na
baada ya kujadiliwa na kupitishwa, vinatungiwa sheria ili viweze
kutekelezwa hivyo vipaumbele vyake ni lazima vifiti kwenye mipango
hiyo,” alisema Msigwa na kuongeza:
“Lakini katika vyote vitatu vya mwaka huu, mpango wa miaka
mitano, mwaka mmoja na hata katika bajeti ya mwaka huu sijaona mahali
popote palipoandikwa kipaumbele cha Serikali ni kuhamia Dodoma.”
Msigwa alisema kuhamisha Serikali ni
gharama kubwa na kuwataka wakazi wa Iringa na maeneo mengine kuhoji
suala hilo kama ndicho kipaumbele cha maendeleo na mahitaji yao.
Alisema wamejipanga kufanya shughuli za maendeleo ikiwamo miradi ya
barabara, kuboresha huduma za afya, usafi wa mazingira na miundombinu.
Mkutano huo ulihudhuriwa na madiwani wa halmashauri hiyo wakiongozwa na Mstahiki Meya, Alex Kimbe.
Comments
Post a Comment