Wastara agombewa kuosha magari
Na Dustan Shekidele, RISASI Mchanganyiko
MOROGORO: Msanii maarufu wa
filamu za Kibongo, Wastara Juma, mwishoni mwa wiki iliyopita aligeuka
gumzo wakati wa harambee maalum ya kuchangia madawati kwa njia ya kuosha
magari iliyofanyika mjini hapa, ambapo wateja wengi walikuwa
wakimgombea awaoshee magari yao.
Harambee
hiyo iliyofanyika kwenye kumbi za Samaki Sport na Nyumbani park,
iliandaliwa na kundi la wanawake wanaojiita Best Friends Forever (BFF)
ambao waliosha magari ya wateja kwa lengo la kukusanya fedha za madawati
kuunga mkono harakati za Rais Dk. John Pombe Magufuli kuhakikisha
hakuna mwanafunzi anayekaa chini.
Mwandishi
wetu alimshuhudia Wastara akiwa bize kuosha gari la mheshimiwa diwani
wa Kata ya Mafiga, Spear Komanya huku wateja wengine nao wakimsubiri
amalize kisha aoshe yao, jambo lililomfanya muda wote aonekane kuwa
bize.
“Leo
tumeamua kuja hapa kwa sababu watu wengi wenye magari huja kustarehe
hapa kwa hiyo wakati wenyewe wakistarehe sisi tunapiga kazi kuhakikisha
tunapata fedha za kununulia madawati,” alisema Wastara.
Alipoulizwa
kama hayo ni maandalizi ya kugombea tena ubunge mwaka 2020 baada ya
kuanguka kwenye kura za maoni kwenye uchaguzi mkuu uliopita ambapo
alikuwa akiwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia viti
maalum, Wastara alisema:
“Siyo
kweli, kwanza baada ya kushindwa ubunge mwaka jana sitarajii kugombea
tena nafasi hiyo mwaka 2020. Kumbuka kufanya kazi hizi za jamii
nimerithishwa na marehemu mume wangu, Sajuki (Juma Kilowoko), unajua
enzi za uhai wake tulianzisha kituo cha watoto yatima kilichopo Kimamba,
Kilosa na mpaka leo nakihudumia kwa hiyo wala sifanyi kwa sababu ya
siasa.”
Comments
Post a Comment