Mdosi mbaroni kwa ujambazi Moshi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Wilbroard Mtafungwa. Issa Mnally na Richard Bukos, UWAZI DAR ES SALAAM: Watu watatu akiwemo mmoja mwenye asili ya Kiasia ‘Mdosi,’ wametiwa mbaroni na polisi Moshi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za ujambazi, Uwazi limeezwa. Akizungumza na waandishi wetu kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki iliyopita, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Wilbroard Mtafungwa alisema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya kukamatwa kutokana na ushirikiano wa polisi na raia wema. Akielezea jinsi polisi walivyowanasa watuhumiwa hao, Kamanda Mtafungwa alisema kuwa walimkamata kwanza mmoja Fredil Guston maarufu kwa jina la Chedieli ambaye ni mkazi wa Majengo, Moshi. Aidha, alisema Chedieli aliwataja wenzake ambao ni Frank Nkya maarufu kwa jina la Chabufa na Frank Mbesanyo Domani ‘Ausho’ mkazi wa Pasua na walipopekuliwa walikutwa na vitu kadhaa vya wizi. “Sasa hawa wakamtaja bosi wao ambaye ni kiongozi wao mkuu wa