Posts

Pichaz 15: CRDB wamemkabidhi Paul Makonda milioni 100

Image
  Baada ya Rais Magufuli kutangaza elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka kufikia kidato cha nne, kumekuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa madawati ambapo Serikali ilianzisha kampeni ya uchangiaji wa madawati, leo June 14 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam   Paul Makonda  amepokea milioni 100 kutoka Bank ya CRDB kwa ajili ya manunuzi ya madawati katika Mkoa wa Dar es Salaam , ‘ Nimeshaongea na wakuu wangu wote wa Wilaya popote pale ambapo upo waje na mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nitapokea chochote kile hata kama liwe ni dawati moja nitalipokea ‘ >>> Paul Makonda

Aina mbalimbali ya maumivu ya tumbo

Image
Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumivu yalipo. Maumivu chini ya mbavu: Kulia yanaweza kusababishwa na mawe kwenye mfuko wa nyongo, maambukizi kwenye mfuko wa nyongo Cholecystitis , uvimbe wa ini, jipu kwenye ini, saratani ya kongosho na kifuko cha nyongo. Maumivu chini ya chembe ya moyo: Husababishwa na vidonda vya tumbo, kiungulia, saratani ya tumbo na saratani ya kongosho. Maumivu pembeni mwa kitovu: husababishwa na mawe ya figo Kidney Stones, maambukizi ya figo, Pyelonephritis na  maambukizi kidoletumbo Acute Appendicitis Maumivu chini ya kitovu: huweza kusababishwa na maambukizi ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya zinaa kama klamidia, PID, vivimbe vya mji wa uzazi, mimba kuharibika na saratani ya kibofu cha mkojo. Maumivu ya tumbo: Ni utumbo kujiziba Intestinal Obstruction,  utumbo kujisokota Volvulus, kula sumu na  mzio wa chakula fulani au ugonjwa wa Crohn Crohn’s Disease,  Ngiri He...

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AGAWA FUTARI KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NA KUJIONEA MABASI YA MWENDO KASI

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteremka kwenye basi la mwendo kasi baada ya kupanda na kujionea ubora na uzuri wa mabasi hayo ambayo yamerahisisha usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.( Picna na OMR) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalumu wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongoza dua hiyo Mussa Salum . Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Futari Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Baraza la Waislam mkoa wa Dar es Salaam Bibi Pili Abdala Mwale wakati wa shu...

Umuhimu wa maziwa mwilini

Image
Unywaji wa maziwa unaopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)  ni mtu mmoja kunywa lita 200 kwa mwaka. Tovuti za Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) zinaonesha kuwa Mtanzania hunywa wastani wa lita 47 tu kwa mwaka. Wakati unywaji huo wa maziwa si wa kuridhisha, kiwango cha watoto wetu kudumaa bado ni kikubwa ambapo asilimia 35 hudumaa. Sababu kubwa inayofanya watoto hao kudumaa ni ukosefu wa vyakula vyenye virutubisho mwilini. Maziwa yana virutubisho vyote muhimu kwa ujenzi wa afya ya binadamu kwani yana protini ya daraja la kwanza, mafuta, madini, vitamin na sukari ya asili ya lactose na maji. Maziwa hutupatia takriban vitamini zote ambazo huyeyuka kwenye mafuta. Nazo ni vitamini A, D, E na K. Vitamini A huhusika na shughuli mbalimbali mwilini. Mfano afya bora ya ngozi zetu kuwa nyororo na ng’avu na pia kuwa na uwezo wa kuzuia wadudu wasiingie mwilini. Vile vile vitamini A hutumika pia kuyapatia macho uimara wa kuona. Na hasa kuona usiku au kwenye mwanga hafifu. Ukosefu wake...

PROFESA LIPUMBA AOMBA MADARAKA TENA…. ..AANDIKA BARUA YA KUOMBA KUENDELEA UENYEKITI WA CUF.

Image
Mwenyekiti wa zamani wa CUF,Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa amemwandikia Katibu Mkuu wa chama hicho barua ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu Uenyekiti wa CUF. Sasa anasubiri majibu toka kwa Katibu Mkuu,Maalim Seif,baada ya ombi lake kujadiliwa na ngazi za juu za kichama. Pia amesema Bajeti ya mwaka wa Fedha 2016/17 yenye thamani ya zaidi ya Trilioni 29.5 haiendani na uhalisia.

Baada ya Sintofahamu… Zitto Kabwe ajitokeza

Image
                   Kiongozi Mkuu wa ACT Zitto Kabwe amejitokeza leo kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam baada ya taarifa kutolewa jana na chama chake kuwa hawajui alipo tangu juzi Jumamosi juni 11. Akizungumza na wanahabari leo baada ya kujitokeza, Mh. Zitto Kabwe amesema kuwa hatishiki na vitisho vinavyotolewa na Jeshi la Polisi nakwamba amekusudia kufanya kongamano la kujadili bajeti kesho Makao Makuu ya Chama hicho huku akiitaka jeshi la Polisi kuacha kumvizia na badala yake limkamate kwa kufuata Sheria. Hii hapa ni taarifa iliyolewa jana Jumapili na uongozi wa Chama Cha ACT wazalendo kuhusu kupotea kwa Kiongozi wao Zitto Kabwe. TAARIFA KWA UMMA Tunaujulisha UMMA kwamba Kiongozi wa Chama chetu cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe amekuwa anatafutwa na Polisi tangu jana usiku. Mpaka sasa hatujui Kiongozi wetu yupo wapi na yupo kwenye Hali g...

JPM Awaapisha Mwigulu Nchemba na Tizeba

Image
Rais Magufuli akimuapisha Mh. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba wakipongezana mara baada ya kuapishwa Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara ...

Trich; hushambulia sehemu nyeti za mwanamke

Image
Ugonjwa wa Trich ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya jamii ya Protozoan na huathiri mrija wa kupitisha mkojo unaojulikana kama Urethra na tupu ya mwanamke Vagina . Ugonjwa huu huweza kuwapata wanaume lakini huwapata na kuonekana zaidi kwa wanawake na daktari anaweza kumuambia mgonjwa anayeugua maradhi haya kuwa ana Trichomonas Vaginalis. UNAAMBUKIZWAJE? Mwanamke au hata mwanaume anaweza kukumbwa na ugonjwa huu akifanya tendo la ndoa na mtu mwenye maambukizi bila kutumia kinga. Kwa kawaida vimelea vya Trichomonas Vaginalis ni vidogo mno ni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe kwa upana (10 μm) ingawa wakati mwingine ukubwa waweza kutofautiana kulingana na mazingira.Wengine huuita ugonjwa huu Trichomoniasis. Watu walio na ugonjwa wa Trich wana hatari ya kupata ugonjwa wa Ukimwi (HIV) au magonjwa mengine ya zinaa kwa sababu bakteria hawa huharibu seli aina ya Epithelium na kusababisha vidonda Microulcerations katika tishu zilizo ndani ya utupu wa mwakamke. DALILI K...

Staa wako ni Wema, Shilole, Kajala, Rose Ndauka au Wolper?

Image
<a href='http://kwanza.co.tz/login/www/delivery/ck.php?n=a397efbc&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE' target='_blank'><img src='http://kwanza.co.tz/login/www/delivery/avw.php?zoneid=31&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE&n=a397efbc' border='0' alt='' /&g 58

Aliyedai ‘wakala’ wa Freemason ala kichapo!

Image
     Bahati Anthony akichezea kichapo. Stori: DUSTAN SHEKIDELE, WIKIENDA, MOROGORO Fundi nguo maarufu mjini hapa, Bahati Anthony aliyedai ni ‘wakala’ wa jamii ya siri inayohusishwa na utajiri wa ghafla na imani za kishetani ya Freemason, amenusa kifo baada ya kunaswa kwa utapeli kwa wakala wa mitandao yasimu inayotoa huduma ya kuweka na kutoa fedha. Akiokolewa na polisi Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Masika katikati ya Mji wa Morogoro kwenye duka la wakala aitwaye Gelasi Assenga ambapo jamaa huyo alijikuta akiloa damu chapachapa. Akisimulia tukio hilo, Assenga alikuwa na haya ya kusema: “Jana huyu jamaa alikuja hapa akatuma shilingi 15, leo amekuja ameniambia nitume laki tatu kwenye namba ileile aliyonipa jana. “Baada ya kutuma, nimemwambia anipe hiyo laki tatu anadai yeye ni wakala wa Freemason hivyo baada ya dakika 10, begi alilobeba litajaa fedha na atanilipa. Nimesubiri dakika 10 zimepita. “Nimemwambia anipe fedha zangu, a...

Mbunge: Simu za watu mil.6 kwenda na maji!

Image
Stori: GABRIEL NG’OSHA, WIKIENDA DAR ES SALAAM: Zikiwa zimebaki siku tatu sawa na saa 72 kabla ya kufungiwa kwa simu feki nchini Tanzania, Alhamisi wiki hii na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA -Tanzania Communication Regulation Authority), inakadiriwa simu za watu zaidi ya milioni 6 zitakwenda na maji. Imeelezwa kuwa unapozungumzia watu zaidi ya milioni sita maana yake yake ni zaidi ya simu feki milioni sita kwani kuna wengine wana simu zaidi ya moja. Kufuatia hali hiyo, Wikienda lilizungumza na watu mbalimbali akiwemo Mbuge wa Mtera (CCM) mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde ambaye alisema serikali imefanya makosa kama ilitaka udhibiti wa vitu feki basi ingedhibiti kwenye uingiaji na siyo kujitwisha mzigo kwa dhambi ya kuwasababishia Watanzania kutumia vitu feki. “Kiukweli serikali ilichofanya ilifikiri ni kama kuhamisha mfumo wa mawasiliano wa analojia kwenda digitali lakini imekosea sana, imejitwisha mzigo mkubwa wa dhambi, kwanza serikali itapoteza mapato lakini hata hi...

Nafasi za kazi United States African Development Foundation

Image
Job Vacancy >  Program Driver Location >  Dar Es Salaam  Position Type >  Full Time Organization Type >  NGO Website > http://www.usadf.gov Application Deadline: 23 Jun 2016 PROGRAM DRIVER POSITION DESCRIPTION: Position Description Document (download) APPLICATION INSTRUCTIONS: Applications should be e-mailed thru  APPLY NOW  with the subject line "TFSAADF16CI0008 Tanzania Program Driver, attention JMCCLEAD/TAYERS" and received before 11.59pm EST on June 23 rd 2016 AVOID SCAMS: NEVER PAY TO HAVE YOUR CV / APPLICATION PUSHED FORWARD. ANY JOB VACANCY REQUESTING PAYMENT FOR ANY REASON IS A SCAM. IF YOU ARE REQUESTED TO MAKE A PAYMENT FOR ANY REASON, PLEASE USE THE  REPORT ABUSE , OR CALL +255 768 982 800 TO REPORT THE SCAM. IF YOU ARE QUALIFIED FOR THIS POSITION  Apply Now  report abuse or errors AddThis Sharing Buttons

Mbowe na Wenzake wa Chadema Wakamatwa, Alipo Zitto Bado ni Utata

Image
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Wakati Polisi ikimshikilia kwa saa mbili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe mkoani Mwanza, jeshi hilo limefuta kongamano la kujadili Bajeti ya Serikali lililoandaliwa na ACT Wazalendo jijini Dar es Salaam huku kiongozi wake, Zitto Kabwe akisakwa. Jeshi hilo lilizuia mkutano wa hadhara wa Chadema uliokuwa ufanyike wiki iliyopita mjini Kahama ambako lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama na wafuasi wa chama hicho, katika kile kilichoelezwa kulikuwa na dalili za uvunjifu wa amani. Jeshi hilo pia lilizuia msafara wa viongozi wa chama hicho kuingia katika ofisi zake za Shinyanga walipokuwa wakielekea Mwanza. Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene ilieleza kuwa mbali na Mbowe, jeshi hilo pia lilikuwa linawashikilia Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi na Katibu Mkuu wa Bavicha, Julius Mwita. Wengine ni Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka na viongozi wengine na w...

BREAKING NEWS : GOODLUCK OLE MEDEYE AIKIMBIA CHADEMA,AHAMIA UDP

Image
​ Kada wa CHADEMA na mbunge wa zamani wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye leo ametangaza kuhamia UDP. Asema inasimamia haki na demokrasia. Anasema anataka demokrasia ya kweli na jukwaa la haki ktk kuleta haki na maendeleo kwa Watanzania. Ameyasema haya akiongea na waandishi wa habari muda mfupi uliopita.

Utafiti umeonesha wanaume wenye vipara ni wanaume wenye mvuto zaidi kimapenzi!

Image
Kuna vitu vingi humvutia mtu inapokuja swala la kumchagua mpenzi, siwezi taja sifa zote, kila mtu anasifa zake na vigezo vyake, ila ngoja tuongelee mvuto wa kipekee unaopatikana kwa wanaume wenye vipara. Nikiongelea vipara naongelea wale walio na vipara asili, achilia mbali wale wanaopenda kunyoa vipara japokuwa kuna baadhi ya sifa hapa wanaweza wakawa nazo pia. Muonekano wa kiume: wanaume wenye vipara wengi huwa na muonekana wa kiume zaidi,muonekano nadhifu  sina maana kama wanaume wengine walio na nywele ndefu ama wastani hawana mvuto lah, nauongelea mvuto zaidi ama mvuto wa kipekee. Ujasiri: wanaume wa aina hii wengi huonekana ni wajasiri kwa muonekano wao tu, hii huwafanya kuwa kivutio kwa wanawake. Wana hisia kali za kimapenzi: daktari kutoka Chuo cha Yale Marekani , James B. Hamilton alisema katika utafiti wake wanaume wengi walio na vipara miili yao huwa inazalisha mbegu nyingi za kiume kuliko wanaume wenye nywele, japokuwa si kwa asilimia 100 alisem...

SERIKALI YATANGAZA UTARATIBU MPYA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, PIA YAFAFANUA FEDHA ZILIZOOKOLEWA KUTOKANA NA WATUMISHI HEWA

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah Kairuki akiongea na waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2016.   Na. Aron Msigwa – Dar es salaam. SERIKALI imetangaza utaratibu mpya utakaofuatwa wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia Juni 16 hadi 23, 2016 ambapo imewaagiza Watendaji Wakuu katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali kutenga siku moja ya kukutana na watumishi katika sehemu zao za kazi kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi. Aidha, imewaagiza watendaji hao kutenga siku nyingine moja kwa ajili ya kukutana na wananchi, kusikiliza na kuzitafutia ufumbuzi kero zao zinazohusiana na huduma zinazotolewa na Taasisi zao. Akitangaza utaratibu huo leo jijini Dar es salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa Serikali imeamua kubadili mfumo wa maadhimis...