Mbunge: Simu za watu mil.6 kwenda na maji!



lusinde
Stori: GABRIEL NG’OSHA, WIKIENDA
DAR ES SALAAM: Zikiwa zimebaki siku tatu sawa na saa 72 kabla ya kufungiwa kwa simu feki nchini Tanzania, Alhamisi wiki hii na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA -Tanzania Communication Regulation Authority), inakadiriwa simu za watu zaidi ya milioni 6 zitakwenda na maji.
Imeelezwa kuwa unapozungumzia watu zaidi ya milioni sita maana yake yake ni zaidi ya simu feki milioni sita kwani kuna wengine wana simu zaidi ya moja.
Kufuatia hali hiyo, Wikienda lilizungumza na watu mbalimbali akiwemo Mbuge wa Mtera (CCM) mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde ambaye alisema serikali imefanya makosa kama ilitaka udhibiti wa vitu feki basi ingedhibiti kwenye uingiaji na siyo kujitwisha mzigo kwa dhambi ya kuwasababishia Watanzania kutumia vitu feki.
“Kiukweli serikali ilichofanya ilifikiri ni kama kuhamisha mfumo wa mawasiliano wa analojia kwenda digitali lakini imekosea sana, imejitwisha mzigo mkubwa wa dhambi, kwanza serikali itapoteza mapato lakini hata hizo kampuni na hata Watanzania wenyewe zaidi ya milioni kama sita watapoteza mawasiliano,’’ alisema Lusinde.
TCRA iliahidi kuzifungia simu zote feki ifikapo Juni 16, mwaka huu na hakutakuwa na muda wa nyongeza.

Comments

Popular posts from this blog