JPM Awaapisha Mwigulu Nchemba na Tizeba

Rais Magufuli akimuapisha Mh. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba wakipongezana mara baada ya kuapishwa Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba mara baada ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba (kulia) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya kuwaapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  leo amewaapisha Mh. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuchukuwa nafasi ya Dkt. Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwana huku Injinia Dkt. Charles Tizeba akiapishwa kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Ikulu, Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kuapishwa, Mh. Mwigulu Nchemba ametoa agizo la kuwataka wafanyabiashara haramu ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo badala yake watafute shughuli halali za kujiingizia kipato.
Aidha Waziri Nchemba alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na utulivu katika nchi.
Naye Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na wataalum wa sekta tatu zilizo katika Wizara yake ili kufanya mapinduzi katika maeneo hayo yaliyoajiri zaidi ya asiimia 80 ya Watanzania.
Pia Waziri Dkt. Tizeba alisema kuwa Wizara itahakikisha inashugahulikia changamoto zinazozokabili vyama vya ushirika ambavyo vimekuwa havifanyi vizuri katika miaka ya hivi karibuni.
Mawaziri walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayejaza nafasi iliyoachwa wazi baada ya Rais kutengua uteuzi wa Mh. Charles Kitwanga.

Comments

Popular posts from this blog