Trich; hushambulia sehemu nyeti za mwanamke

TRICH Ugonjwa wa Trich ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya jamii ya Protozoan na huathiri mrija wa kupitisha mkojo unaojulikana kama Urethra na tupu ya mwanamke Vagina . Ugonjwa huu huweza kuwapata wanaume lakini huwapata na kuonekana zaidi kwa wanawake na daktari anaweza kumuambia mgonjwa anayeugua maradhi haya kuwa ana Trichomonas Vaginalis.
UNAAMBUKIZWAJE?
Mwanamke au hata mwanaume anaweza kukumbwa na ugonjwa huu akifanya tendo la ndoa na mtu mwenye maambukizi bila kutumia kinga.
Trichomoniasis_01
Kwa kawaida vimelea vya Trichomonas Vaginalis ni vidogo mno ni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe kwa upana (10 μm) ingawa wakati mwingine ukubwa waweza kutofautiana kulingana na mazingira.Wengine huuita ugonjwa huu Trichomoniasis.
Watu walio na ugonjwa wa Trich wana hatari ya kupata ugonjwa wa Ukimwi (HIV) au magonjwa mengine ya zinaa kwa sababu bakteria hawa huharibu seli aina ya Epithelium na kusababisha vidonda Microulcerations katika tishu zilizo ndani ya utupu wa mwakamke.
DALILI KWA WANAWAKE Dalili za Trich huanza kuonekana kuanzia siku ya 4 mpaka 28 baada ya mtu kupata maambukizi ya ugonjwa huu. Kwa wanawake Trich huathiri shingo ya kizazi Cervix, mrija wa mkojo, tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo, tezi zinazojulikana kama Bartholin Glands na Skene Gands.
Wanawake waliokumbwa na ugonjwa huu hutokwa na uchafu sehemu zao za siri na huwa na rangi ya njano, kijani au kijivu na huwa mzito. Dalili nyingine ni kuwa na maumivu wakati wa kujamiiana na kutoka harufu mbaya.
Mgonjwa pia hujisikia maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo na shingo ya kizazi huwa nyekundu lakini hili
ataligundua daktari akifanya uchunguzi kwa mgonjwa. Dalili nyingine ni kuwasha sehemu za siri, kupata maumivu chini ya kitovu. Wanawake wengine wanaweza kuwa na vimelea hivi na wakaishi navyo kwa mwaka mzima bila kugundua kama hawatakwenda kupimwa.
UGUNDUZI
Mgonjwa hugundulika baada ya kufanyiwa vipimo. Kipimo cha hadubini Microscope hutumika ambapo daktari huingiza kifaa maalum katika tupu ya mwanamke kinachojulikana kama Speculum na kuchukua kipimo kwa kutumia pamba maalum Cotton Swab na kupeleka maabara kuangalia kama kuna vimelea vya Trichomonas Vaginalis.
Itaendelea wiki ijayo.

Comments

Popular posts from this blog