Aliyedai ‘wakala’ wa Freemason ala kichapo!
Stori: DUSTAN SHEKIDELE, WIKIENDA, MOROGORO
Fundi nguo maarufu mjini hapa, Bahati Anthony aliyedai ni ‘wakala’ wa jamii ya siri inayohusishwa na utajiri wa ghafla na imani za kishetani ya Freemason, amenusa kifo baada ya kunaswa kwa utapeli kwa wakala wa mitandao yasimu inayotoa huduma ya kuweka na kutoa fedha.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Masika katikati ya Mji wa Morogoro kwenye duka la wakala aitwaye Gelasi Assenga ambapo jamaa huyo alijikuta akiloa damu chapachapa.
Akisimulia tukio hilo, Assenga alikuwa na haya ya kusema: “Jana huyu jamaa alikuja hapa akatuma shilingi 15, leo amekuja ameniambia nitume laki tatu kwenye namba ileile aliyonipa jana.
Akisimulia tukio hilo, Assenga alikuwa na haya ya kusema: “Jana huyu jamaa alikuja hapa akatuma shilingi 15, leo amekuja ameniambia nitume laki tatu kwenye namba ileile aliyonipa jana.
“Nimemwambia anipe fedha zangu, anasema haijaingia, nikaamua kumpekua kwenye begi nikakuta mshumaa.”
“Wakati napekuwa ndipo akaanza kukimbia. Nilipoona nitapoteza fedha zangu, nikaona nimwitie mwizi ndipo watu wakamkamata na kumshushia kichapo.
“Hata hivyo, polisi walimwamuru kurudisha fedha zangu ambapo aliwapigia simu ndugu zake kutoka Kigoma ambao walidai kuwa watanitumia fedha yangu ndipo aachiwe huru.”
“Baadaye waliniambia ninunue begi jipya ndani yake niweke mshumaa na udi kisha niende palepale kwa wakala wa jana yake niwatumie shilingi laki tatu. “Niliwaambia fedha hiyo sina, wakaniambia nimwambie wakala anitumie tu baada ya dakika 10 begi langu litajaa fedha lakini haikuwa hivyo ndiyo maana ssenga akaniitia mwizi nikapigwa.”
Kumekuwa na utapeli wa aina hiyo mkoani hapa hivyo Wikienda linawataka wasomaji wake kuwa macho ili wasilizwe.
Kumekuwa na utapeli wa aina hiyo mkoani hapa hivyo Wikienda linawataka wasomaji wake kuwa macho ili wasilizwe.
Comments
Post a Comment