Mume, Mke Wachinjwa Kinyama.
Majeneza yenye miili ya marehemu hao. Na Gregory Nyankaira, RISASI MCHANGANYIKO MARA: Hali mbaya! Wanandoa Said Somba (48) na Kadogo Ehijo (47), wakazi wa Kitongoji cha Rugala, Kijiji cha Mazami, Kata ya Bukabwa wilayani Butiama mkoani hapa wameuawa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana, Risasi Jumatano lina kila kitu. Marehemu Somba (kushoto) na marehemu Kadogo kulia. Diwani wa Kata ya Bukabwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Rugala, Jonas Maswe aliliambia gazeti hili kuwa, tukio hilo lilijiri usiku wa Mei 25, mwaka huu ambapo watu hao wakiwa na mapanga walivamia nyumbani kwa Somba akiwa amelala na mkewe na kuwachinja. Baadhi ya watoto wa marehemu wakilia juu ya jeneza la baba yao Alisema wakati wanachinjwa, wanandoa hao hawakupiga kelele na baada ya ukatili huo wauaji hao waliifunika miili yao kitandani kisha wakatokomea kusikojulikana. Alisema mauaji hayo yalifanyika kimyakimya kwani hata watoto wa marehemu waliokuwa wame...