MISS TANZANIA APEWA TALAKA KISA SOMA HAPA
Miss Tanzania 2011, Salha Israel. IMELDA MTEMA, AMANI Ndoa ya Miss Tanzania 2011, Salha Israel aliyofunga na Abdulatif Fundikira ‘Tiff’ ambaye ni mtalaka wa mwanamitindo Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ aliyeko gerezani kwa msala wa madawa ya kulevya huko Macau, China, inasemekana kuingia mdudu mbaya baada ya mrembo huyo kudaiwa kupewa talaka moja. Kwa mujibu wa chanzo makini, kumekuwa na kutoelewana kati ya wanandoa hao, jambo ambalo limewafanya kuwa kwenye sintofahamu kila wakati huku wakimsaka mchawi wa ndoa yao. Salha Israel akiwa na mumewe. “Awali wale watu walikuwa wanapendana sana lakini cha ajabu kumekuwa na migogoro midogomidogo kwenye ndoa yao hadi kufikia wakati wenyewe wanajiuliza mchawi ni nani ilihali wao wanaonekana wanapendana sana,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa wanandoa hao. Baada ya ishu hiyo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari wetu alianza kwa kumsaka Tiff ambaye a