MISS TANZANIA APEWA TALAKA KISA SOMA HAPA



IMG_0050
Miss Tanzania 2011, Salha Israel.
IMELDA MTEMA, AMANI
Ndoa ya Miss Tanzania 2011, Salha Israel aliyofunga na Abdulatif Fundikira ‘Tiff’ ambaye ni mtalaka wa mwanamitindo Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ aliyeko gerezani kwa msala wa madawa ya kulevya huko Macau, China, inasemekana kuingia mdudu mbaya baada ya mrembo huyo kudaiwa kupewa talaka moja.

Kwa mujibu wa chanzo makini, kumekuwa na kutoelewana kati ya wanandoa hao, jambo ambalo limewafanya kuwa kwenye sintofahamu kila wakati huku wakimsaka mchawi wa ndoa yao.
1
Salha Israel akiwa na mumewe.
“Awali wale watu walikuwa wanapendana sana lakini cha ajabu kumekuwa na migogoro midogomidogo kwenye ndoa yao hadi kufikia wakati wenyewe wanajiuliza mchawi ni nani ilihali wao wanaonekana wanapendana sana,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa wanandoa hao.
Baada ya ishu hiyo kutua kwenye dawati la gazeti hili, mwanahabari wetu alianza kwa kumsaka Tiff ambaye alipoulizwa kuhusu taa nyekundu kuiwakia ndoa yake alifunguka kuw anachokijua yeye ni kwamba amepata mke mwema lakini kuna watu wanataka kumharibia ndoa yake huku akimwachia Mungu kumsimamia. “Hakuna asiyejua kama mimi nimepata mke mwema sana lakini kuna watu hawapendi kuona ndoa yangu inaendelea.
Mimi namuachia Mungu kwani yupo pamoja nasi siku zote,” alisema Tiff huku akishindwa kukubali au kukataa kumtwanga talaka Salha. Salha na Tiff walifunga ndoa ya siri ya kiserikali mwaka 2014, nyumbani kwa wazazi wa mrembo huyo, Sinza-Mori jijini Dar, mwaka 2014.

Comments

Popular posts from this blog