Wema Sepetu na Aunt Ezekiel
Miongoni mwa mastaa wa filamu na muziki
Bongo wamekuwa na viashiria vya vitendo visivyofaa hasa wanapokuwa
kwenye sehemu za starehe na wengi wao ni wale wanaotumia kinywaji chenye
kilevi.
Wanaotajwa sana kwenye tabia hiyo mni
pamoja na hawan wafuatao kutokana na picha zao kuzagaa nsana mitandaoni
na kwenye magazetin mbalimbali.
Hapa nawazungumzia Aunt Ezekiel na Wema Sepetu, Isabela Mpanda na Baby Madaha, Rayuu na Skaina nk.
Mastaa hawa kwa nyakati tofauti wamekuwa
wakionesha wazi viashiria hivyo kwa kupigana picha na picha hizo
kuzagaa kwenye vyombo vya habari.
Wao kwao imekuwa kama fasheni na muda
mwingi hulichukulia suala hili kama la kawaida kwa madai kuwa ni
kutokana na ukaribu wa urafiki walionao.
Skaina na Rayuu
Je, kabla ya ustaa walikuwa wakisalimiana na kuwa karibu hivi?
Ni swali ambalo linaulizwa na kila msomaji pengine na hata wazazi wanaowazunguka kwani kwao ni vitu vigeni.
Ustaa ndiyo shinikizo la viashiriahivi ama veepe?
Wasanii wengi wanapokuwa wameshaingia
kwenye tasnia ndiyo huanzisha mambo ya ajabu na wengine hudiriki
kujifunza tabia ambazo hawakuwa nazo kabla.
Bela na Baby Madaha
Imefikia hatua ya wazazi kushindwa
kuwaingiza watoto wao kwenye tasnia hususan Bongo Muvi kutokana na jinsi
wengi wao wanavyoharibiwa na mchanganyiko wa watu wanaokutana nao.
Ni ustaa ama veepe, kwani kila anayeonekana akimbusu mwenzake lazima liwe busu lenye viashiria vya vitendo vichafu.
Swaga hii ya mabusu ilianzia kwa mastaa
wakubwa, Aunt Ezekiel na mwenzake Wema Sepetu sasa imekuwa kama mtindo
kwa mastaa wanaotoka.
Hivi hamuoni kuwa nyie ni chanzo cha
mastaa wajao kuharibika? Busu hili si utamaduni wetu Watanzania na mbaya
zaidi hufanya kitendo hicho baada ya kulewa.
Comments
Post a Comment