TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA RWANDA-MAJALIWA.
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Rwanda nchini, Eugene Kayihura. Ambapo amemuahidi kuwa Tanzania
itaendelea kushirikiana na Rwanda.
Akizungumza
na Balozi Kayihura jana ,(Jumatano 13, 2016) ofisini kwake, Magogoni
jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo kwa
kumtembelea na ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendeleza
ushirikiano ulipo baina ya nchi hizi mbili.
“Nia yetu
ni kushirikiana kwa pamoja kwa kuunganisha wafanyabiashara wetu, kwa
kutumia Bandari ya Dar es salaam na reli ya kati, ambayo tutajenga kwa
kiwango cha kisasa ‘standard gauge’ ili ziweze kubeba mizigo mingi na
kwenda mwendo wa kasi” alisema Waziri Mkuu.
Kwa
upande wake, Balozi wa Rwanda, Kayihura amesema Tanzania na Rwanda ni
nchi marafiki na zinafanyakazi wa pamoja, Rwanda iko tayari kushirikiana
na Tanzania kikanda na kimataifa.
“Tunatumia
Bandari ya Dar es salaam na Mombasa, tunashukuru kwa namna ambavyo
mnaboresha Bandari ya Dar es Salaam, kwani Rwanda inafaidika pia kwa
vile mizigo yetu mingi karibu asilimia 75 husafirishwa kupitia bandari
hii” alisema Balozi Kayihura.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
ALHAMISI, JANUARI 14, 2016.
Comments
Post a Comment