Edward Mordrake; Binadamu Mwenye Sura Mbili.
Edward Mordrake
NI vigumu kuamini! Edward Mordrake ni Mwingereza mashuhuri wa karne
ya 19 ambaye alijinyakulia tuzo za Nobel. Mordrake aliyetokea kwenye
ukoo mashuhuri na wenye hadhi kubwa nchini humo, alitambulishwa zaidi
kwa sura zake mbili, moja ikiwa kwenye uso wake wa kawaida na nyingine
nyuma ya uso (kwenye kisogo).
Cha kushangaza zaidi inasemekana kuwa
sura yake ya kisogoni haikuweza kula wala kuongea chochote na hata
ikijaribu kuongea maneno yalikuwa hayasikiki lakini iliweza kulia,
kucheka na kusikia kila neno.
Sura yake ya mbele ya uso imeelezwa kuwa
ilikuwa ni nzuri na ya kuvutia (handsome). Watu waliomuona na
kuzungumza naye, wanamsifu Mordrake kwa uzuri wa sura yake ya usoni na
tabasamu lake, lakini balaa lipo kwenye sura yake ya kisogoni ambayo ni
ya kutisha na inayofanana na sura ya “bibi kizee mchawi”.
Simulizi za wafanyakazi wa jumba la
kifahari alimoishi Mordrake, zinatolewa kwa siri, ambapo zinaeleza hali
ya maisha ya huzuni ya kijana huyo iliyosababishwa na miujiza na mabalaa
yaliyoletwa na sura yake ya kisogoni.
Mara kadhaa aliwaomba madaktari
wamfanyie upasuaji wa “kuing’oa” sura hiyo ya kishetani, lakini sababu
za kitabibu zilizoonesha uwezekano wa yeyé kupoteza uhai endapo
atafanyiwa upasuaji huo, hivyo walikataa kufanya hivyo.
Akiwa na umri wa miaka 23, Mordrake
aliaamua kujiua kwa kunywa sumu baada ya kuchoshwa na mikasa hiyo ya
sura mbaya aliyoiita kuwa ni ya kishetani, mikasa iliyokuwa ikimtokea
mara kwa mara hasa usiku huku akiacha wosia kuwa sura hiyo mbaya ifyekwe
kisogoni kwake kabla ya kuzikwa ili isiendelee kumtesa huko kaburini.
Kiulingana na hadhi ya ukoo wa Mordrake
nchini Uigereza, historia ya maisha yake haikuweza kuwekwa wazi ili
watu wengine wakajua maisha yake.
Comments
Post a Comment