Taswira za sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Vikosi vya Ulinzi liliandaliwa rasmi katika kilele cha sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika jana katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi wakati wa kilele cha sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Salim Ahmed Salim.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein mara alipowasili katika kilele cha sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika kilele cha sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Pichani kutoka kushoto Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange.
Baadhi ya Wananchi na Maafisa mbali mbali wa Serikali wakiwa katika sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakati alipowasili katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja katika Kilele cha sherehe za Mapinduzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi walioshiriki katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium jana akiwa katika gari maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wananchi walioshiriki katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium jana akiwa katika gari maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteremka katika gari maalum alilopanda wakati akiwasalimia wananchi katika kilele cha Sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 katika Uwanja wa Amaan Studium.
Baadhi ya Maafisa mbali mbali wa Vikosi vya Ulinzi na Taasisi za Serikali wakiwa katika sherehe za kilele cha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52 zilizofanyika katika uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakibeba Picha la Marehemu Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Karume wakati wa Maandamano ya kusherehehekea Kilele cha Mapinduzi Kutimia miaka 52.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini wakibeba mabango yenye ujumbe tofauti kama yanavyoonekana wakati wa Maandamano ya kusherehehekea Kilele cha Mapinduzi.

Comments

Popular posts from this blog