Posts

CHADEMA Wacharuka Baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Kumweka Ndani Mbunge wao Saidi Kubenea..Watoa Tamko

Image
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kama ambavyo imeripotiwa kwenye vyombo vya habari na njia zingine za upashanaji habari tangu jana kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Ndugu Saed Kubenea aliwekwa chini ya ulinzi na kuamriwa kwenda kituo cha polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye inadaiwa hakutaka mbunge huyo azungumze na wananchi ambao ni Wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Took Garment, waliokuwa wamemuita mbunge huyo kwa ajili ya kumweleza matatizo wanayokumbana nayo kazini hapo, ikiwa ni pamoja na ujira kidogo na mazingira magumu ya kazi. Aidha akitambua kuwa alichofanya matumizi mabaya ya dhamana ya uongozi, hivyo akakusudia kuficha umma usijue uovu huo, katika tukio hilo Makonda aliwaagiza polisi wakamate kamera za waandishi wa habari waliokuwa katika eneo hilo wakitimiza wajibu wao wa kikazi na kitaaluma kwa jamii. Katika hatua ya sasa, tunaomba kusema ifuatavyo; 1.  Tukitambua kuwa mamlaka ya DC kuamuru watu kukamatwa yamef

Mwanasheria Albeto Msando Afunguka Kuhusu Dr Mwaka....Adai Walikuwa Wapi Siku Zote?

Image
Kuna watu watasema ni wivu! Kuna wengine watasema Mwaka ni tapeli! Kuna ambao watakuwa upande wa Kigwangwala na kuna ambao watakuwa kwa Mwaka. Ila je kwa nini mpaka leo hii tiba inahojiwa? Siku zote mamlaka husika zilikuwa wapi? Hao waliotibiwa wakapona wako wapi?  Ambao hawajapona ni kina nani? Mkurugenzi wa Baraza la Tiba Asili mpaka anafika hapo kwenye 'kliniki' alikuwa hajui kama Mwaka ana vyeti au la? Hakuwa na taarifa zozote za ziada? Je Babu wa loliondo ilikuwaje? Wanaotibu mapenzi na kupata kazi vipi? Wale madaktari wa kusafisha nyota? Au hao kuku weusi wanaokula sio dhuluma? Nadhani Naibu Waziri ameanza kushtukiza ila AENDE NA KWENYE VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI PIA. Kuna hao madaktari waliosomea na wao ni bure kabisa huko!! Hili la Mwaka kilichomponza ni kupitiliza!! Wote huwa inatukuta tukinogewa!! Sasa ndio atajua kama bado WATAMPENDA By Alberto Msando-Instagram

WABUNGE WANNE WAKATAA UWAZIRI KWA MAGUFULI

Image
WABUNGE wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametajwa kukataa uteuzi wa nafasi ya uwaziri ili kujaza nafasi za wizara nne zilizokuwa wazi. Hatua hiyo imetokana na kile kilichoelezwa kuwa ni hofu ya wabunge hao kushindwa kwenda na kasi ya Rais Dk. John Magufuli, ambaye aliwaapisha mawaziri wapya Desemba 12, mwaka huu. Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania, wabunge wamedai kuwa kasi ya Rais Magufuli inawatia hofu. “Kasi ya Rais Dk. John Magufuli ni nzito na kwangu ni ngumu na nilifikiri niko mimi peke yangu kumbe baada ya taarifa hizi nasikia na wenzangu wawili nao walikataa uteuzi. “Niliarifiwa juu ya uteuzi lakini baada ya kupima nikaona hapana siwezi kazi ya uwaziri, bora ni baki na ubunge wangu,” alisema mbunge huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe. Wizara 4 zilizokosa Mawaziri Wakati akitangaza Baraza la Mawaziri, Desemba 10, mwaka huu, Rais Magufuli alisema kuna baadhi ya wizara hazina mawaziri kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo unyeti wa wizara hizo na kwamba a

Kubenea apandishwa Mahakamani leo

Image
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea. Baada ya taflani iliyotokea jana Jumatatu kati ya mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea wa Chadema na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda eneo la viwanda (EPZA) Mabibo jijini Dar hali iliyopelekea DC Makonda kuwaamuru polisi wamuweke chini ya ulinzi Saed Kubenea na kumpeleka Kituo cha Polisi. Leo Saed Kubenea amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake kuahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu huku uchunguzi ukiendelea.

Mwanamke wa unga jela miaka 20

Image
Anna Gemanist Mboya. Na Makongoro Oging’ Mrembo wa madawa ya kulevya ‘unga’, Anna Gemanist Mboya mkazi wa Kijitonyama, Kinondoni jijini Dar amefungwa jela miaka 20 na kupigwa faini ya shilingi milioni 148, fedha anazotakiwa kuzilipa mara atakapomaliza kifungo. Mrembo huyo ambaye ni mfanyabiashara, amefungwa Desemba, Mosi, mwaka huu mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Wilfrida Koroso kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya. Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa (pichani) amethibitisha kuhukumiwa kwa mrembo huyo na ameipongeza mahakama kwa kasi ya kuendesha kesi nyingi za madawa ya kulevya na kuzitolea hukumu. Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa, Anna alikamatwa Januari 2, mwaka 2011 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kikosi kazi (task force) kilichopo katika kiwanja hicho. “Nawaomba wananchi waendelee kuwafichua wahusika wa madawa ya kulevya ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya she

Waziri Makamba, Naibu Waziri Mpina Wakabidhiwa Ofisi

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa  Rais- Mazingira na Muungano Mh. January Makamba akipokea nyaraka za  Ofisi wakati akikabidhiwa Ofisi na Waziri aliyemaliza muda wake Dk.  Binilith Mahenge Ofisini Mtaa wa Luthuli Dar es Salaam. Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa  Rais- Mazingira na Muungano Mh. Luhaga Mpina akikabidhiwa nyaraka za  Ofisi na Naibu Waziri aliyemaliza muda wake Mh. Stephen Masele .  Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa  Rais akiwa Bwana Sazi Salula akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa  Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano Mh. January Makamba  na Waziri aliyemaliza muda wake Dkt. Binilith Mahenge mara baada ya  makabidhiano ya Ofisi.

BREAKIN NEWZZZ!!:- MBUNGE MPYA CHADEMA ATIWA MBARONI DAR

Image
SAED KUBENEA MBARONI KWA AMRI YA MKUU WA WIYALA YA KINONDONI PAUL MAKONDA  Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) amekamatwa na polisi eneo la viwanda (EPZA) Mabibo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda. Tukio hilo limetokea kukiwa na mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1800 wa kiwanda cha nguo cha TOOKU ambao walimpigia Mbunge wao aende kutatua mgogoro huo. Kubenea alifika katika eneo hilo saa 6 mchana, akakutana na wafanyakazi kusikiliza kero zao za muda mrefu. Kisha aliamua kuondoka na viongozi wa wafanyakazi hao na kufanya kikao na menejimenti ya Kiwanda hicho kuanzia saa 7 hadi saa 9.  Ilipofika saa 10:30 Makonda alikuja na kupata taarifa kwa muafaka uliofikiwa kati ya Kubenea, menejimenti na viongozi wa wafanyakazi. Alitoa amri wafanyakazi wakusanyike, akaawaambia kesho atafika huko kesho na Waziri wa Viwanda na Biashara, Waziri wa Kazi na Ajira, na waziri wa Afya wanawake, jinsia na watoto. Alimzuia Mbunge asihutubie kuaga wananchi aliokuwa nao tangu

Watoto wa vigogo TRA wamiliki majumba mabilioni

Image
Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Philip Mpango. Na Mwandishi Wetu KIMENUKA tena! Wakati Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ akiendelea kusimamia zoezi la kutumbua majipu katika sekta na idara za umma kote nchini, imebainika kuwa baadhi ya vigogo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamewamilikisha watoto wao wenye umri wa miaka mitatu hadi saba, majumba yenye thamani ya mabilioni ya shilingi, Uwazi linaripoti. TUJIUNGE NA CHANZO Chanzo makini kilicho ndani ya TRA kimeliambia gazeti hili kuwa vigogo wengi wa mamlaka hiyo, walio makao makuu jijini Dar es Salaam na mikoani, wamekuwa wakiwaandikisha watoto wao kuwa wamiliki halali wa majumba na vitega uchumi vyenye thamani ya mabilioni ya shilingi vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini. Mfano wa majumba wanayomiliki. “Wanafanya hivyo ili kukwepa mkono wa sheria kama wataambiwa kutaja mali walizonazo. Kwa hiyo unakuta jengo kama lile la… (anatajwa kigogo wa TRA anayemiliki jengo la ghorofa sita, lililopo Masaki jijini Dar) hati

BREAKING NEWS : MAUWAJI MOROGORO,MKULIMA AUWAWA,WAZIRI ATUA HARAKA

Image
Mkulima mmoja auawa, mwingine ajeruhiwa wakiwemo askari polisi wawili kwenye mapigano dhidi ya wafugaji wa kimang’ati kwenye kijiji cha Dihimba Turiani, mkoani MorogoroMkuu wa Wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa amesema mapigano hayo yametokea baada ya wafugaji kutaka kuwachukua kwa nguvu ng’ombe zaidi ya 150 waliokuwa wakishikiliwa na wakulima kwenye ofisi ya kijiji hicho  Mkwasa amesema siku ya tarehe 11 mwezi huu, mkulima mmoja aliyejulikana kwa jina la Bakari Mulunguza alikuta ng’ombe zaidi ya 150 wakila shambani kwake pasipo kuwa na mchungaji wa ng’ombe hao, ndipo Mulunguza alipoomba msaada kutoka kwa wakulima wenzake kwa pamoja waliwaswaga ng’ombe hao hadi kwenye ofisi ya serikali ya kijiji. Amesema wakulima hao waliamua kuchukua uamuzi huo ili mwenye ng’ombe ajitokeze na kupigwa faini kutokana na uharibifu uliosababishwa na ng’ombe hao. Alisema siku iliyofuata ya tarehe 12, ndipo alipojitokeza mfugaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shaabani Ikeli na kudai kuwa yeye ndiy

Mitikisiko ya Pwani yaitikisa Dar Live

Image
Mwibaji wa kundi la Excellent (katikati)akiselebuka na wanenguaji wake. Hadija Kopa nae akionyesha umahili wake wa kuimba na kucheza. Wanamuziki wa Ogopa Kopa taarabu wakiserebuka. Ma Mc wa onyesho hilo Mc pilipili na Dida wakipozi kupigwa picha. Nyota Waziri akicheza na shabiki wake.   Nyota Waziri akimpagawisha shabiki kwa sauti tamu. Msagasumu akiwarusha mashabiki. Mzee yusufu nae akikonga nyoyo za mashabiki waliofika kwenye onyesho hilo. Wanenguaji wa kibao kata wakifanya yao. Jana usiku ndani ya ukumbi wa Taifa wa burudani wa Dar Live kulikuwa na onyesho la Mitikisiko ya Pwani onyesho hilo lilizikutanisha bendi mbalimbali za taarabu za hapa jijini Dar es Salaam. Bendi hizo ni Jahazi, Excellent, Ogopa kopa na Wakali wao, pia kulikuwa na vikundi vya Baikoko, Kibao kata na Msagasumu aidha mwanadada Nyota Waziri pia alitoa burudani katika onyesho hilo.

Masogange kumzalia Davido?

Image
  Video Queen anayekimbiza Bongo, Agness Masogange. HUENDA ikawa kweli Video Queen anayekimbiza Bongo, Agness Masogange amenasa ujauzito unaosemekana kuwa ni wa staa wa muziki kutoka Naija, Davido baada ya kuweka picha tata mtandaoni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Masogange aliweka picha ya Davido na kuandika ‘I’m missing him’ na baada ya sekunde kadhaa tena akaweka picha nyingine ilioonesha majibu ya ujauzito kuwa amenasa. Hata hivyo baada ya kuandamwa na mashabiki alizifuta zote hali iliowafanya mashabiki wawe njia panda.Wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza Novemba mwaka huu katika sherehe ya kuzaliwa ya Davido. Kama kweli Masogange atakuwa na ujauzito kama inavyosemakana na ikajulikana ni wa Davido basi Davido atakuwa na mtoto wa pili baada ya wa kwanza aliyenaye ambaye amezaa na Sophie Momodu wa Nigeria. (Imetayarishwa na Andrew Carlos/Gpl)

Mwanamke wa kwanza achaguliwa Saudi Arabia

Image
Mmoja wa wanawake Saudi Arabia akipiga kura. Wananchi wa Saudi Arabia wameweka historia kwa kumchagua mwanamke wa kwanza kuwa mwakilishi wao katika uchaguzi uliofanyika jana. Tume ya uchaguzi ya Saudia Arabia imetangaza. Salma bint Hizab al-Oteibi alichaguliwa kuwa mwanamke wa kwanza mwakilishi wa wilaya katika Jimbo la Mecca. Wanawake Saudi Arabia wakitoka kupiga kura kuwachagua viongozi wao. Japo matokeo ya uchaguzi huu yanaendelea kutangazwa tangazo hilo limeibua hisia miongoni mwa wenyeji. Hii ndio iliyokuwa mara ya kwanza wanawake kupiga kura na kushiriki kama washindani. Maofisa wa Serikali walisema kuwa wanawake 130,000 walijiandikisha kupiga kura, ambayo ni moja ya kumi ya wapiga kura wanaume. Kuna zaidi ya wagombea 1,000 wanaong’ang’ania viti mbalimbali katika huo. Wanawake hawa walikuwa wakifanya kampeni zao huku wamesimama nyuma ya pazia au wakati mwingine wanawakilishwa na mwanaume. Wanawake kadhaa wa Saudi Arabia wamepongeza uchaguzi huo kama hatua muhim

WAKATI WAPINZANI WAKIPINGA UTEUZI WA WAZIRI PROFESA MUHONGO MWENYEWE ATOA KAULI NZITO AFUNGUKA KILA KITU

Image
WAKATI wapinzani wakipinga uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, waziri huyo amewasihi wananchi kumvumilia kidogo, ili baada ya muda mfupi atoe mpango wa maendeleo ya wizara hiyo, ambao pamoja na mambo mengine, utaelezea bei ya nishati hiyo itakavyoshuka.  Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, Profesa Muhongo alisema mbali na mkakati wa kushusha bei ya umeme, kasi ya kusambaza umeme vijijini kupitia miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), itarejea palepale. “Nimepokea uteuzi huo, kinachofuata ni kuwatumikia wananchi, niwaombe tu wanivumilie kidogo nitawapa mpango wangu wa maendeleo wa muda mfupi na mrefu, lakini nisisitize tu nishati sio siasa, ni suala la utaalamu, liachwe lifanywe kitaalamu,” alisema Profesa Muhongo. Akizungumzia bei ya umeme na upatikanaji wake, Profesa Muhongo alisema kupunguza bei hiyo ni ajenda muhimu itakayozingatiwa na kusema il

BREAKING NEWS:WAZIRI WA KWANZA KUTIMULIWA NA RAIS MAGUFULI HUYU HAPA

Image
Rais John Magufuli alionya Mawaziri aliowataja juzi kuwa tayari kufanya sherehe ya kufukuzwa, kama pia wataandaa sherehe za kuteuliwa kushika nyadhifa hizo katika Baraza la kwanza la serikali yake ya awamu ya tano. Katika kauli yake hiyo mbele ya waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema anataraji Mawaziri aliowachagua wawe wachapa kazi, wenye lengo la kuleta maendeleo nchini kwa kasi. Akitangaza Baraza lake hilo ikiwa ni siku ya 35 tangu aapishwe kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Rais Magufuli alisema: “Na kwa hakika, wasihangaike kufanya sherehe. Wamepata kazi ngumu, wakafanye kazi, lakini kama wapo ambao wanaopenda kufanya sherehe, pia wajiandae kufanya sherehe siku wakifukuzwa. “’Contract’ (mkataba) yetu ni miaka mitano, tukawafanyie Watanzania yale tuliyoyaahidi, bila kubagua rangi, dini, itikadi, ukanda, makabila, ndiyo maana siku zote nimekuwa nikisema Hapa ni Kazi Tu.” Lakini si lazima Waziri adumu kwa miaka mitano ya

KAMPUNI YA AZAM YAMDINDIA MAGUFULI,NI KUHUSU AGIZO LA SIKU SABA,TRA YAWAANGUKIA WATANZANIA,SOMA HAPO KUJUA

Image
Kaimu Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua za ulipaji wa kodi iliyokwepwa katoka katika kontena 329 katika bandari Kavu ya Azam,leo jijini Dar es Salaam. Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii KAMPUNI 15 zimeshindwa kulipa kodi za kontena zilizotoroshwa katika bandari kavu ya Azam inayomilikiwa na Said Salim Bakhressa na kodi iliyokuwa imekwepwa kwa kampuni 43 ni zaidi ya Sh. Bilioni 12.      Kodi iliyolipwa ya Kontena 329 hadi jana ambayo ndio ilikuwa ulipaji wa hiari kwa ndani ya siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ni zaidi ya sh. bilioni 10 pekee.       Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamisha Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni hizo zinatakiwa kulipa kodi hiyo kwani ulipaji wa hiari wa siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli umeisha jana  hivyo hatua zitachukuliwa kuh

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Mhongo katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii na Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri , leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri, leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Ashantu Kijaji katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri, leo katika ukum