KAMPUNI YA AZAM YAMDINDIA MAGUFULI,NI KUHUSU AGIZO LA SIKU SABA,TRA YAWAANGUKIA WATANZANIA,SOMA HAPO KUJUA
Kaimu
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango
akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) juu ya hatua za ulipaji
wa kodi iliyokwepwa katoka katika kontena 329 katika bandari Kavu ya
Azam,leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAMPUNI
15 zimeshindwa kulipa kodi za kontena zilizotoroshwa katika bandari
kavu ya Azam inayomilikiwa na Said Salim Bakhressa na kodi iliyokuwa
imekwepwa kwa kampuni 43 ni zaidi ya Sh. Bilioni 12.
Kodi
iliyolipwa ya Kontena 329 hadi jana ambayo ndio ilikuwa ulipaji wa
hiari kwa ndani ya siku saba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ni zaidi ya
sh. bilioni 10 pekee.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamisha Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa kampuni
hizo zinatakiwa kulipa kodi hiyo kwani ulipaji wa hiari wa siku saba za
Rais Dk. John Pombe Magufuli umeisha jana hivyo hatua zitachukuliwa
kuhakikisha wanalipa kodi hiyo ya Watanzania.
Mpango
amesema kuwa kampuni 13 tu ndio zimeweza kumaliza kodi yote iliyokuwa
imekadiriwa na TRA kwenye Kontena 329 zilizotoroshwa katika Bandari Kavu
ya Azam (ICD).
Amesema
kampuni 15 zimelipa sehemu ya kodi na wanaendelea kuwadai licha ya
kuisha kwa siku saba hivyo wanawajibu kulipa kodi iliyobaki katika
Akaunti ya TRA iliyofunguliwa Benki Kuu (BoT) yenye namba 9921169 785.
Mpango amesema kuwa wafanyabiashara ambao wameshindwa kulipa katika hicho hatua zitachukuliwa na wasubiri cha moto.
Amesema
watumishi 36 wa TRA wanatuhumiwa kushiriki katika upotevu wa kodi
kutokana na kontena 329 kuondoshwa bandarini kinyume cha taratibu za
forodha na hivyo kusababisha serikali ikose mapato.
Mpango
amesema kuwa TRA inawaomba wananchi taarifa juu mali za kifisadi na
mwenendo mbaya wa baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo.
Amewataka
watumishi kuwasilisha tamko za mali wanazomiliki pamoja na fedha zilizo
katika benki na mwisho wa kufanuya hivyo ni Desemba 15 mwaka huu
Comments
Post a Comment