Mwanamke wa kwanza achaguliwa Saudi Arabia

saudia kura
Mmoja wa wanawake Saudi Arabia akipiga kura.
Wananchi wa Saudi Arabia wameweka historia kwa kumchagua mwanamke wa kwanza kuwa mwakilishi wao katika uchaguzi uliofanyika jana. Tume ya uchaguzi ya Saudia Arabia imetangaza.
Salma bint Hizab al-Oteibi alichaguliwa kuwa mwanamke wa kwanza mwakilishi wa wilaya katika Jimbo la Mecca.
saudia
Wanawake Saudi Arabia wakitoka kupiga kura kuwachagua viongozi wao.
Japo matokeo ya uchaguzi huu yanaendelea kutangazwa tangazo hilo limeibua hisia miongoni mwa wenyeji.
Hii ndio iliyokuwa mara ya kwanza wanawake kupiga kura na kushiriki kama washindani.
Maofisa wa Serikali walisema kuwa wanawake 130,000 walijiandikisha kupiga kura, ambayo ni moja ya kumi ya wapiga kura wanaume.
Kuna zaidi ya wagombea 1,000 wanaong’ang’ania viti mbalimbali katika huo.
Wanawake hawa walikuwa wakifanya kampeni zao huku wamesimama nyuma ya pazia au wakati mwingine wanawakilishwa na mwanaume.
Wanawake kadhaa wa Saudi Arabia wamepongeza uchaguzi huo kama hatua muhimu.
Hata hivyo wengine wanasema kuwa hauna umuhimu wowote kwa sababu maisha yao yana vizuizi vingi kama vile kutoruhusiwa kuendesha magari.

Comments

Popular posts from this blog