Mwanamke wa unga jela miaka 20
- Get link
- X
- Other Apps
Anna Gemanist Mboya.
Na Makongoro Oging’
Mrembo wa madawa ya kulevya ‘unga’, Anna Gemanist Mboya mkazi wa Kijitonyama, Kinondoni jijini Dar amefungwa jela miaka 20 na kupigwa faini ya shilingi milioni 148, fedha anazotakiwa kuzilipa mara atakapomaliza kifungo.

Mrembo huyo ambaye ni mfanyabiashara, amefungwa Desemba, Mosi, mwaka huu mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Wilfrida Koroso kwa kosa la kusafirisha madawa ya kulevya.
Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, SACP Godfrey Nzowa (pichani) amethibitisha kuhukumiwa kwa mrembo huyo na ameipongeza mahakama kwa kasi ya kuendesha kesi nyingi za madawa ya kulevya na kuzitolea hukumu.
Kwa mujibu wa Kamanda Nzowa, Anna alikamatwa Januari 2, mwaka 2011 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kikosi kazi (task force) kilichopo katika kiwanja hicho.
“Nawaomba wananchi waendelee kuwafichua wahusika wa madawa ya kulevya ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuokoa taifa letu na biashara hii haramu,” alisema Nzowa.
“Nawaomba wananchi waendelee kuwafichua wahusika wa madawa ya kulevya ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuokoa taifa letu na biashara hii haramu,” alisema Nzowa.
TUMIA LIKIZO HII KUJIANDAA VIZURI
NAFAHAMU kabisa kuwa, Desemba hii wanafunzi wengi mko kwenye mapumziko (likizo). Lakini haitakuwa na maana kwako kama utapumzika kwa kuyaweka kando mambo yote ya shule wakati kuna baadhi ya masomo yanakusumbua.

Kufanya hivyo hakuna maana yoyote kwa sababu unakaaje mapumziko wakati unajua somo f’lani linakusumbua, mara zote umekuwa ukifanya vibaya kwenye mitihani yako?
Napenda kukushauri kuitumia vizuri likizo hii ili iwe na manufaa kwako na pindi utakaporudi shuleni uwe na mabadiliko katika masomo, ufahamu na uelewa wako.
Napenda kukushauri kuitumia vizuri likizo hii ili iwe na manufaa kwako na pindi utakaporudi shuleni uwe na mabadiliko katika masomo, ufahamu na uelewa wako.
Nasikitika ninapoona baadhi yenu mmekuwa na tabia ya kufanya mambo ya ajabu wakati huu wa likizo, wengi utawaona klabu, ufukweni ‘beach’ na kwingineko wanakojirusha.
Jaribu kutumia likizo hii kuziba mapengo ambayo ulikuwa nayo, kurejea masomo ambayo yamekuwa kikwazo kwako katika kufaulu.
Chukua muda kutafakari ni namna gani nimekuandikia makala nyingi za mbinu za kujisomea na wewe ni kwa kiasi gani umefanya utekelezaji.
Pata wakati wa kujiuliza na kutafakari kwa nini uonekane mjinga darasani wakati binadamu wote ni sawa? Ukifanikiwa kupata majibu ya maswali hayo basi naamini tatizo lako la kushika nafasi mbaya shuleni utakuwa umelimaliza.
Nafahamu utakuwa na viporo vingi vya masomo basi muda huu wa likizo siyo wa kujirusha ni muda wa kumalizia mapengo uliyonayo.
Huu ndiyo muda wa kutafuta matirio, muda wa kumtafuta mtu ambaye anafanya vizuri katika masomo yanayokutatiza wewe. Jaribu kumtafuta na kuzungumza naye yeye anasom saa ngapi, anafanyaje, anapumzika muda gani na kadhalika.
Kwa kufanya hivyo naamaini utaitendea haki likizo yako na wewe utakuwa ni sawa na ule msemo usemao ‘mtembea bure si sawa na mkaa bure,’ kwa sababu tu wewe likizo yako umeitumia kujifunza, kupata mbinu na namna ya kukabiliana na masomo ambayo yamekuwa ni kikwazo kwako katika kufanya vizuri.
Nachukua nafasi hii kuwahimiza tena wanafunzi wote kuhusu kuitumia vizuri likizo hii. Nawapenda sana na ninawatakia likizo njema.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment