Kubenea apandishwa Mahakamani leo


said1Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.
Baada ya taflani iliyotokea jana Jumatatu kati ya mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea wa Chadema na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda eneo la viwanda (EPZA) Mabibo jijini Dar hali iliyopelekea DC Makonda kuwaamuru polisi wamuweke chini ya ulinzi Saed Kubenea na kumpeleka Kituo cha Polisi.
Leo Saed Kubenea amepandishwa kizimbani kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake kuahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu huku uchunguzi ukiendelea.

Comments

Popular posts from this blog