BREAKING NEWS:WAZIRI WA KWANZA KUTIMULIWA NA RAIS MAGUFULI HUYU HAPA
Rais
John Magufuli alionya Mawaziri aliowataja juzi kuwa tayari kufanya
sherehe ya kufukuzwa, kama pia wataandaa sherehe za kuteuliwa kushika
nyadhifa hizo katika Baraza la kwanza la serikali yake ya awamu ya tano.
Katika
kauli yake hiyo mbele ya waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam,
Rais Magufuli alisema anataraji Mawaziri aliowachagua wawe wachapa
kazi, wenye lengo la kuleta maendeleo nchini kwa kasi.
Akitangaza Baraza lake hilo ikiwa ni siku ya 35 tangu aapishwe kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Rais Magufuli alisema:
“Na kwa
hakika, wasihangaike kufanya sherehe. Wamepata kazi ngumu, wakafanye
kazi, lakini kama wapo ambao wanaopenda kufanya sherehe, pia wajiandae
kufanya sherehe siku wakifukuzwa.
“’Contract’
(mkataba) yetu ni miaka mitano, tukawafanyie Watanzania yale
tuliyoyaahidi, bila kubagua rangi, dini, itikadi, ukanda, makabila,
ndiyo maana siku zote nimekuwa nikisema Hapa ni Kazi Tu.”
Lakini si lazima Waziri adumu kwa miaka mitano ya mkataba baina ya serikali na wananchi huo, Rais Magufuli aliashiria.
Ni kipi hasa kinaweza kumfanya Waziri wa Serikali ya Magufuli awe wa kwanza kwenda na maji?
Kupoteza uadilifu, uzalendo, uzembe na kutokuwa tayari kupokea maagizo na kuyatekeleza kwa wakati, uchuguzi wa Nipashe umebaini.
Akizungumza
na gazeti hili jana, Mwalimu wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally, alisema Baraza la Mawaziri limekidhi
kwa kiasi kiu ya Watanzania, japo hajakamilisha kwa kujaza wizara
ambazo zipo wazi.
Alisema
katika watu aliowateua anaamini alitumia muda mwingi kuangalia watu
wanaoweza kufanya kazi kwa maelekezo ya katiba ya nchi, inayoweka wazi
kuwa kiongozi lazima awe muadilifu, mchapakazi na elimu ya kutosha.
“Bahati
mbaya Rais hana mshirika katika kumchagua mtu, habanwi na sheria wala
katiba lakini naamini mawaziri aliowateua alizingatia mambo muhimu,”
alisema Bashiru.
Alifafanunua
kuwa mawaziri hao wakitaka kwenda na kasi ya kiongozi huyo wanatakiwa
kuwa wazalendo na wawajibikaji kwa kuifanya kazi ya umma kwa juhudi na
na maarifa ya ziada.
Kwa
upande wake, Dk. Mohamed Bakari wa UDSM pia alisema anachoona katika
safari ya mawaziri hao itakuwa ngumu kutimiza wajibu wao na linaweza
kubadilishwa endapo hakutatokea mabadiliko ya haraka katika kasi ya
kutumbua majipu kama anavyotaka Rais.
Aidha, Dk. Bakari alimsifu Rais kwa kuangalia ushirikishwaji wa kila eneo la nchi na usawa wa kijinsia.
Alifafanua
kuwa katika vigezo hivyo aligusa kila eneo la nchi kwa kumteua Waziri
au Naibu kwa ajili kufanya serikali iwe shirikishi.
Wakati
huo huo, Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),
umelitahadharisha Baraza la Mawaziri lililoteuliwa juzi lisiwe mizigo
kwa Rais John Magufuli.
Pia
umewataka mawaziri kuhakikisha mchakato wa kuundwa Baraza la Taifa la
Vijana unakamilika ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za kisiasa,
kiuchumi na kijamii.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Idara ya Uhamasishaji,
Sera, Utafiti na Mawasiliano ya UVCCM, Egla Mwamoto, alisema ingawa
baraza hilo ni dogo wanatarajia wafanye kazi kwa nguvu na bidii zaidi.
Alisema
mawaziri wengi ni vijana na UVCCM inaamini kwamba iwapo watajituma
kikamilifu wanaweza kuleta maendeleo na kubadilisha mfumo wa nchi.
Aidha,
aliwataka mawaziri hao wasimamie kutenga maeneo ya uzalishaji mali,
kuviwezesha vikundi vya kukopa na kuweka vya vijana (Saccos), kuweka
vituo maalumu vya vijana kila wilaya, pamoja na kuhakikisha kuwa
wananufaika na Shilingi milioni 50 zitakazotolewa na serikali kwa kila
kijiji.
“Sisi
wadau wa vijana tunawataka mawaziri walioteuliwa wamsaidie Rais Magufuli
kutatua changamoto zinazozikabili sekta mbalimbali ikiwamo ya vijana
hasa katika suala la ajira na tunawakumbusha watekeleze ilani ya CCM,
kwa kasi ambayo ameanza nayo Rais katika maeneo mbalimbali,” alisema
Mwamoto.
Alisema
mawaziri lazima wamuunge mkono Rais katika kuzuia matumizi yasiyo ya
lazima ili fedha hizo zielekezwe kwenye maboresho ya huduma za kijamii
zinazosuasua.
“Tatizo
kubwa ni rushwa na ubadhirifu wa mali za umma, tunaamini kazi ya
kudhibiti kundi hilo italeta mafanikio kutokana na jitihada
zilizoelekezwa huko. Wananchi tushirikiane na viongozi wetu kuleta
maendeleo ya taifa,” alisema.
WALIOTEULIWA
Mawaziri
Ofisi ya Nchi Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George
Simbachawene na Angela Kairuki, Naibu ni Jafo Suleiman; Makamu wa Rais,
Muungano na Mazingira, Waziri ni Januari Makamba, Naibu ni Luhaga Mpina.
Waziri wa
Ofisi ya Nchi, Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu, ni Jennista Mhagama, Naibu Mawaziri ni Profesa Possi Abdallah
na Anthony Mavunde; Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba,
Naibu ni William Tate Ole Nashe.
Wizara ya
Katiba na Sheria, Waziri ni Dk. Harrison Mwakyembe; Dk. Augustine
Mahiga, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Naibu ni Dk. Susan Kolimba; Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa, Waziri ni Dk. Hussein Mwinyi; Wizara ya Nishati na
Madini, Waziri ni Profesa Sospeter Muhongo na Naibu ni Medard Kalemani.
Wizara ya
Mambo ya Ndani, Waziri ni Charles Kitwanga; Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Naibu Angelina Mabula; Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Waziri ni Charles Mwijage; Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri ni Ummy
Mwalimu, Naibu Dk. Hamis Kigwangala.
Wizara ya
Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Waziri ni Nape Nnauye, Naibu ni
Anastazia Wambura; Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Waziri ni Profesa
Makame Mbarawa, Naibu Mhandisi Isaack Kamwela.
WIZARA ZILIZOKOSA MAWAZIRI
Katika uteuzi huo Wizara nne zimekosa mawaziri ambao alisema atawateua siku zijazo na kuteua manaibu pekee.
Wizara
hizo ni Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, Mawasiliano (haina Waziri), Naibu ni
Injinia Edwin Ngonyani; Fedha na Mipango (haina Waziri), Naibu ni Dk.
Ashaji Kijachi.
Nyingine
ni Wizara ya Maliasili na Utalii (Haina Waziri), Naibu ni Mhandisi Lamo
Makani; Wizara ya Elimu, Teknolojia na Ufundi (haina Waziri), Naibu ni
Mhandisi Stellah Manyanya.
KUVUJA JASHO
Tofauti
na miaka ya hivi karibuni ambapo nafasi za juu za uongozi zikiwamo za
uwaziri zilikuwa zikichukuliwa kuwa ni ‘ulaji’ kiasi kwamba watu
walikuwa wakipongezana, inaonekana wazi kuwa mawaziri wa Rais Magufuli
watakuwa tofauti.
Mianya
mingi iliyokuwa ikitajwa kuwapatia mawaziri mamilioni ya fedha inaelekea
kuzibwa kutokana na amri kadhaa alizotangaza tangu aapishwe kuwa Rais,
lengo likiwa ni kubana matumizi na kuwezesha fedha zinazopatikana
zitumike kumaliza kero mbalimbali zinazowakabili Watanzania.
Baadhi ya
maeneo yaliyokuwa yakitajwa kuwaingizia fedha nyingi mawaziri, lakini
sasa yameondoshwa na hivyo kubana matumizi holela ya serikali ni pamoja
na hafla za kupongezana, safari za nje; posho za semina elekezi,
kuchapisha kadi za Krismasi, Mwaka Mpya, Iddi na sikukuu nyingine,
manunuzi ya bidhaa mbalimbali yenye fedha za ziada maarufu kama ‘cha
juu’, posho za vikao vya kikazi mikoani, manunuzi ya kila mara ya samani
za ofisi zilizokuwa zikitoka ughaibuni na pia posho za vikao vya kamati
za Bunge.
Rais
alisema serikali yake imechelewa kuteua Baraza la Mawaziri kwa muda wa
mwezi mmoja kwa ajili ya kuokoa fedha za mishahara na marupurupu ya
Mawaziri na Manaibu ambazo zingetumika kwenye shughuli nyingine za
maendeleo ya taifa.
CHANZO: NIPASHE
Comments
Post a Comment