Posts

MAANDAMANO YA KUMKUMBUKA MAREHEMU MWANGOSI MKOANI IRINGA

Image
Katibu wa IPC Francis Godwin akiongoza maandamano ya wanahabari na wadau huku akiwa juu ya gari na picha ya marehemu Daud Mwangosi. Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari mkoa wa Iringa ya kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi yakipita eneo ya Uhindini. Wanahabari Iringa katika maandamano ya kumuenzi marehemu Mwangosi jana. Wanahabari wa vyombo mbalimbali na wadau wa habari mkoa wa Iringa wakiwa katika maandamano ya amani ya kumuenzi aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC). Maandamano ya wanahabari na wadau wa habari yakipita eneo la soko kuu la manispaa ya Iringa.   Wananchi wakishuhudia maandamano hayo. Katibu Mtendaji wa IPC, Francis Godwin akitoa taarifa ya kuanza kwa maandamano ya kumuenzi marehemu Daud Mwangosi jana. Katibu wa IPC Francis Godwin (kushoto) akikabidhi picha ya marehemu Daud Mwangosi kwa Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard (kulia), wanaoshuhudia ni Mzee Fulgence Malangalila na

WAZIRI WA UJENZI DKT.MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI WA UCHUKUZI WA MALAWI

Image
Waziri wa Ujenzi Mh. Dkt. John Magufuli (kushoto) leo amekutana na Waziri wa Uchukuzi kutoka Malawi Mh.Sidik Mia (wapili pichani kutoka kulia) pamoja na Ujumbe wake jijini Dar es Salaam.Pichani( katikati) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Herbet Mrango. Waziri wa Ujenzi Mh. Dkt. John Magufuli (kushoto) akiongea na Waziri wa Uchukuzi wa Malawi Mh. Sidik Mia(kulia) alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam(katikati) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hebert Mrango. Waziri wa Ujenzi Mh. Dkt, John Magufuli (alienyanyua mkono) akiongea na ujumbe kutoka Malawi alipokutana nao leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam Waziri waUjenzi Mh. Dkt. john Magufuli (kushoto) akimkabidhi nyaraka Waziri wa Uchukuzi wa Malawi Mh. Sidik Mia (kulia) leo jinini Dar es Salaam,walipokutana na kuzungumza masuala mbalimbali yakiwemo kuimarisha ushirikiano katika nyaja za usafirishaji .(katikati) Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Hebert Mrango. Waz

KISIWA CHA SAANANE HIFADHI MPYA YA TAIFA

Image
Kisiwa cha Saanane kimetangazwa rasmi kuwa Hifadhi ya Taifa kufuatia Tangazo la Serikali Namba 227 lililotolewa hivi karibuni. Kutangazwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane kunafuatia kupitishwa kwa Azimio la Bunge mwezi Oktoba mwaka jana lililoridhia kupandishwa hadhi kwa kisiwa hicho kutoka Pori la Akiba na kuwa Hifadhi ya Taifa. Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane itakuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 2.18 na itajumuisha maeneo ya lililokuwa Pori la Akiba , Visiwa vya Chankende kubwa na ndogo pamoja na eneo la maji ya Ziwa Victoria linalozunguka visiwa hivyo. Kuanzishwa kwa Hifadhi mpya ya Taifa ya Saanane kutawezesha haja ya kuongeza spishi mbalimbali za wanyamapori na hivyo kuongeza utalii wa mjini, utalii wa ndani, utafiti na kutoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi na wananchi watakaotembelea hifadhi hii mpya. Aidha, uamuzi huu utasaidia kutunza hali ya bioanuwai, uhifadhi wa mazalia na makuzio ya samaki n

NHIF YAZINDUA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA YA JAMII (CHF)MJINI KILWA

Image
Adoh Mapunda Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa akipokea vifaa maalum vya kuhifadhia fedha na nyaraka mbalimbali kutoka kwa Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati wa uzinduzi wa Huduma za Bimaya Afya (CHF)katika halmashauri hiyo uliofanyika jana kwenye viwanja vya Mkapa Garden Mjini Kilwa, wa pili kulia anayeshuhudia tukio hilo ni Kaimu Mkurugenzi wa (NHIF) Khamis Mdee na kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athuman Rehani na Fortunata Raymond Msimamizi wa NHIF mkoani Lindi.wananchi mbalimbali wakiwemo wazee walijitokeza katika zoezi la upimaji wa afya yakiwemo magonjwa ya Kisukari, Shinikizo la Damu ikiwani pamoja na kupima Uzito Urefu. Ado Mapunda Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za Bima ya Afya katika Halmashauri ya wilaya ya Kilwa jana kulia ni Bw. Khamis Mdee Kaimu Mkurugenzi NHIF na kushoto ni Dr. Hilda Mwakipesile kutoka NHIF.

OZIL ATUA ARSENAL, FELLAINI AKIJIUNGA NA MAN UTD

Image
Lukas Podolski (kulia) na Mesut Ozil (kushoto) katika pozi na jezi ya Arsenal nchini Ujerumani. Mshambuliaji mpya wa Man Utd, Marouane Fellaini (kushoto) akikabidhiwa jezi na kocha wake David Moyes (kulia). Marouane Fellaini ndani ya Manchester United. -OZIL ATUA KWA KITITA CHA BILIONI  107, FELLAINI BILIONI 69.3 KLABU ya Arsenal imefanikiwa kumnasa kiungo wa Ujerumani, Mesuit Ozil kwa ada ya pauni milioni 42.5 sawa na bilioni 107 za Tanzania. Usajili wa Ozil umevunja rekodi katika klabu hiyo inayoongozwa na Mfaransa Arsene Wenger. Staa huyo wa Ujerumani aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano na atakuwa akilipwa  pauni 140,000 sawa na milioni 352.8 za Tanzania kwa wiki. Wakati Arsenal wakimnasa Ozil katika dakika za mwisho za dirisha la usajili kufungwa, Manchester United wao wamefanikiwa kumnasa Mshambuliaji wa Everton, Marouane Fellaini kwa ada ya pauni milioni 27.5 sawa na bilioni 69.3 za Tanzania. Fellaini ameungana na kocha wake wa zamani David Moyes  anayei

MSANII WA KIZAZI KIPYA AFUNGWA JAELA MIEZI 21 BAADA YA KUWATUKANA POLISI

Image
Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Tunisia amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kwa kuwatusi polisi , miezi miwili tu baada ya kuachiliwa kufuatia maandamano ya umma. Ala Yaacoubi, anayesifika kwa jina Weld El 15, alifungwa jela miaka miwili mnamo mwezi Juni kwa kutoa wimbo uliokuwa unawafananisha polisi na Mbwa ambao unasema kuwa polisi wanapaswa kunyongwa. Hata hivyo hukumu yake iliondolewa mwezi Julai alipoachiliwa ingawa inadaiwa kuwa aliendelea kuimba wimbo huo. Hukumu hii imetolewa wakati yeye mwenyewe hakuwa mahakamani na kwa hivyo atahitajika kujikabidhi kwa polisi. Wakili wake anasema kuwa kesi hiyo ilihusu zaidi kushambulia uhuru wa watu kujieleza. "nitazungumza na mteja wangu kupinga uamuzi huu , lakini hukumu zinazotolewa dhidi ya wasanii zinaonyesha kuwa vita dhidi ya

MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA TAMASHA LA 11 LA TGNP JIJINI DAR ES SALAAM YAFANA

Image
Tamasha la 11 la mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) limeanza kwa maandamano katika ofisi za TGNP eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam. Maandamano hayo yameanzia lango kuu la ofisi za TGNP na kuhitimishwa katika viwanja vya tamasha eneo hilo la TGNP. Akizungumza katika uzinduzi wa tamasha hilo mkurugenzi wa TGNP Usu Mallya alisema wakati TGNP inaazimisha tamasha hilo bado inajivunia mapambano makubwa yaliyodumu kwa miaka 16 katika kupigania jengo hilo ambalo lilikuwa na kesi mahakamani hadi wanaposhinda kesi hiyo. Hivyo alisema ushindi wa kesi hiyo dhidi ya jengo hilo utawafanya sasa kuendelea kuboresha zaidi jengop hilo na kulifanya kuwa la kisasa zaidi na kuendeleza mafunzo mbali mbali. Chanzo:Francisgodwinblog

WIMBO MPYA WA DIAMOND- MY NUMBER ONE

Image
           

Zoezi la kuaga Mwili wa Askofu Dr. Mosses Kulola linaendelea hivi sasa CCM Kirumba.

Image
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola Zoezi la Kuaga mwili wa Marehemu Askofu Dr. Mosses Kulola linaendelea hivi sasa katika Uwanja wa CCM Kirumba na Mwisho itakuwa ni Saa 10:00 Jioni, na hii ni kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Askofu Dr. Mosses Kulola. Mwili wa Marehemu utazikwa kesho Siku ya Jumatano September 4, 2013 katika Kanisa la EAGT Bugando. Imetolewa na M/Kiti - Kamati ya Mazishi 0754 394337/0688 857629 

RAIS KIKWETE AMTEUA PROFESA MLAMA KUWA MWENYEKITI WA BASATA

Image
(Na Veronica Kazimoto – MAELEZO) Dar es Salaam). Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Penina Mlama kuwa  Mwenyekiti wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari – MAELEZO leo, Uteuzi huo wa Profesa Mlama unanzia mwaka 2013 na unatarajia kumalizika mwaka 2016. Prof. Mlama ni Profesa wa Sanaa na Sanaa za Maonyesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aidha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ameteua jumla watu 12 kuwa wajumbe wa BASATA kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka huu. Walioteuliwa ni pamoja na  wawakilishi wa Vyama na Asasi mbalimbali wa Baraza hilo ambao ni Dkt. Vincensia Shule, John Kitime ,  Angela Ngowi, Dkt. Herbert Makoye, Erick Shigongo na Alex Msama. Wawakilishi wengine ni pamoja na Juma Adam Bakari, Daniel Ndagala, Michael Kadinde na Joyce Fisoo. Wanaoingia

Ethiopia yakana kukandamiza upinzani;

Image
Takriban wanachama 100 wa chama cha upinzani cha Semayawi nchini Ethiopia walikamatwa na wengine kuchapwa vibaya sana mwishoni mwa wiki. Hii ni kwa mujibu wa chama hicho. Mwenyekiti wa chama hicho Yilekal Getachew alisema kuwa vifaa kama vipaza sauti vilinaswa kabla ya mkutano wa hadhara uliokuwa umepangiwa kufanyika Jumapili kuharamishwa. Waziri wa habari na mawasiliano Shimeles Kemal alikanusha madai kuwa polisi walifanya msako kuwakamata waandamanaji hao. Serikali ilisema kuwa sehemu kulikoandaliwa mkutano wa hadhara, ilikuwa imewekewa kikundi cha wanachama wa vuguvugu linalopinga siasa kali. Chama tawala EPRDF kinasifika kwa kuweka sheria kalu sana kudhibiti maisha ya watu kukutana hadharani Maandamano ya umma yaliandaliwa mwezi Juni na yalikuwa ya kwanza makubwa kwenye barabara za mji mkuu Addis Ababa tangu mwaka 2005 wakati mamia ya waandamanaji walipouawa wakati wakiandamana. Maandamano hayo yalifanyika kutoa wito wa kuachiliwa kwa waandishi w

Pacha aliyeungana sasa atolewa ICU

Image
Mtoto Kudra aliyekuwa ameunganika na kiwiliwili cha pacha mwenza, anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Mtoto huyo alifanyiwa upasuaji Alhamisi iliyopita katika Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na kulazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), lakini mwishoni mwa wiki iliyopita alitolewa katika wodi hiyo. Mama mzazi wa mtoto huyo, Pili Hija, alisema hivi sasa Kudra ananyonya vizuri na kwamba amekuwa akitaka kufanya hivyo kila wakati . "Kwa kweli kudra za Mwenyezi Mungu ndizo zimemweka hai mpaka leo hii, nilikuwa nimeshakata tamaa kuwa nampoteza mwanangu, nazidi kumuomba Mungu amwekee mkono wake apone kabisa," alisema Hija. Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto katika Hospitali ya Muhimbili, Dk Zaitun Bokhary, alisema mtoto huyo anaendelea vizuri na mwishoni mwa mwezi huu atafanyiwa upasuaji mwingine. "Tunamwacha achangamke kwanza, mwishoni mwa mwezi huu tutamfan

RWANDA YAPANDISHA USHURU WA MAGARI YA MIZIGO YANAYOTOKA TANZANIA

Image
RWANDA imeamua ‘kucheza rafu’ kwa kuanza kuhujumu Bandari ya Dar es Salaam, kwa kupandisha ushuru wa barabara kwa magari ya mizigo yanayotoka Tanzania pekee kuanzia Rusumo hadi Kigali, kutoka dola za Marekani 152 za awali, hadi 500.   Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichomalizika hivi karibuni Arusha, ushuru huo ulianza kutozwa rasmi kwa magari hayo juzi. Hali hiyo imesababisha mtafaruku katika eneo la Rusumo, mpakani mwa Tanzania na Rwanda, ambako zaidi ya malori 200 yenye mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam, yamekwama kwa kushindwa kulipa kiwango hicho kipya cha ushuru wa barabara.   Awali nchi hiyo ilikuwa ikitoza ushuru wa dola za Marekani 16 kwa kila kilometa 100, ushuru ambao ndio uliokuwa ukitozwa na Tanzania kwa malori yaliyokuwa yakipitisha mizigo kwenda nchi za nje. Hata hivyo, katika kilichoonekana kuwa mazingira yasiyo sawa ya kupata faida kutokana na udogo wa ene

MWANAMKE ANASWA NA SARE ZA JWTZ

Image
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Saida Mohamed (30), mkazi wa Mwasonga Kigamboni, akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 31, mwaka huu, katika eneo la Mwasonga, Kigamboni. Alisema Saida alikamatwa na suruali saba, mashati saba ya kombati, kofia 10, shati mbili nyepesi, fulana mbili na kofia moja aina ya bareti, vyote vikiwa mali ya JWTZ. Alisema mtuhumiwa huyo, alikuwa na begi moja la kuwekea nguo za jeshi, cheo kimoja cha Koplo na mikanda miwili ya kijeshi. Alisema uchunguzi unaendelea juu ya mwanamke huyo ili kubaini sababu za kumiliki sare za jeshi, kabla ya kufikishwa mahakamani. Katika tukio jingine, polisi wamemkamata Husein Mkondoa (25), mkazi wa Gongolamboto Mzambarauni, akiwa anaendesha pikipiki huku akiwa amevaa nguo za kiraia na kofia ngumu ya kij

Nimepewa majina ya wabunge wauza dawa za kulevya: Wamo CCM, Chadema

Image
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Kigwangallah, amesema amepokea majina ya wabunge, viongozi wa serikali na wafanyabiashara maarufu nchini ambao ni mapapa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya. Hata hivyo, Dk. Kigwangallah ambaye amepania kuwataja bungeni watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, amesema baada ya kukabidhiwa majina hayo kutoka kwa wananchi, anafanya uchunguzi na kupata ushahidi ili kujiridhisha kabla hajachukua hatua ya kuwataja. Miongoni mwa majina ya wabunge aliyopewa wamo kutoka CCM na Chadema, na wafanyabiashara maarufu wote wanatoka mkoa wa Dar es Salaam. "Nawashukru wananchi wamenipa ushirikiano hadi jana wamenikabidhi majina ya watu saba ambao ni wabunge wawili, kiongozi mmoja mwandamizi wa serikali na wafanyabiashara wanne, ambao wote ni mapapa wauza unga na siyo madagaa," alisema Dk. Kingwangallah. Alisema katika kuhakikisha anatekeleza alichoahidi amemwandikia barua Spika wa Bunge kumuomba atoe maelezo

Kumbukumbu Ya Kuawa Kwa Mwangosi Na Swali La Mtoto Yule...

Image
Ndugu zangu, HUWEZI kutawala miili ya watu ukaacha mioyo yao. Ndiyo, mjumbe hauawi, ni kauli ya hekima ya tangu enzi za wahenga wetu. Leo ni mwaka mmoja tangu mwandishi wa habari na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa Habari mkoani Iringa, Daud Mwangosi kuawa. Ilikuwa ni Jumapili ya Septemba 2, 2012. Hakika, siku ile itabaki katika kumbukumbu za Watanzania kwa mamilioni. Ni kwa kufikiwa na taarifa za kutisha za mauaji ya mwandishi wa habari. Haya yanaingia katika historia kuwa ni mauaji ya kwanza kwa mwandishi wa habari kufanyika hadharani tangu nchi hii ipate Uhuru. Wengi watakuja kukumbuka walikuwa wapi na walifanya nini siku walipopata taarifa hizo za kutisha. Binafsi, taarifa ile ya mauaji ya Daud Mwangosi siku ile ya Jumapili ya huzuni kwa Taifa ilinikuta nikiwa Iringa Mjini. N umbali wa mwendo wa saa moja kwa gari kufika eneo la tukio, Nyololo, Mufindi. Jioni ile nilikuwa nikifundisha soka ya watoto. Mara baada ya kupata taarifa zile kwa simu, nili

MAHAFALI YA KWANZA IRINGA RETCO BUSINESS COLLEGE

Image
Mh Jaji mstaafu Raymond Mwaikasu akimtunuku Cheti cha Astashahada na Stashahada ya uongozi wa Biashara pamoja na tuzo ya uanafunzi Bora 2010 Beatrice Ndekwa. Wasanii wa kikundi cha Ngoma toka Mkwawa Magic Site wakitumbuiza, 

Waliopanda mbegu DECI hatarini kutolipwa

Image
WATEJA wa Kampuni ya DECI waliopanda mbegu, wanaweza wasilipwe fedha zao, MTANZANIA Jumatatu limebaini. Wateja hao ambao wanaidai kampuni hiyo Sh bilioni 39.27, huenda wasilipwe fedha zao kwa kuwa mchezo wa upatu hautambuliki kisheria. Utata huo ulijulikana mwishoni mwa wiki, baada ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu, kuzungumza na MTANZANIA Jumatatu. "Kwanza kabisa, niseme tu kwamba hadi sasa hatujapata nakala ya hukumu hiyo ili kujua inatuelekeza nini kuhusu mchakato wa kuwalipa hao waliopanda mbegu. "Tukipata hukumu hiyo, ndiyo tutaisoma na kufahamu tumepewa jukumu gani na gharama zitalipwa na nani katika kutekeleza mchakato huo. "Sisi tunataka tujue hiyo hukumu inamaanisha nini, maana kwa kawaida anayechezesha na anayecheza upatu wote wana makosa, sasa utamlipaje aliyecheza? "Lakini, kwa kuwa hatujaiona hiyo hukumu, hatujui imetuelekeza nini, lakini i

LAPF KUTUMIA BILIONI 35 UJENZI WA KITUO CHA MABASI MSAMVU

Image
Na Fatma Salum na Hassan Silayo- MAELEZO Mfuko wa pensheni wa LAPF unatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 35 katika mradi wa kituo cha mabasi eneo la msamvu Mkoani Morogoro. Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa mfuko huo Kanda ya Mashariki Sayi Lulyalya alisema mradi huo ambao ni ubia kati ya Manispaa ya Morogoro na mfuko wa LAPF unatarajiwa kuanza wakati wowote mwaka huu. Sayi alisema hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo ambao utakamilika baada ya miezi 18 zimeshaanza kwa kuzungushia uzio katika eneo la ujenzi wa kituo hicho. "LAPF imeamua kutenga takriban bilioni 35 za ujenzi wa kituo cha Msamvu na tunashukuru uongozi wa Manispaa ya Morogoro kwa kutoa eneo la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho na michoro imeshakamilika na shughuli za zabuni zinaendelea." Alisema Sayi. Aidha Sayi aliongeza kuwa mradi huo wa uwekezaji utahusisha ujenzi wa hoteli yenye

DIAMOND ATUHUMIWA KUIBA WIMBO WA DYNA..."MY NUMBER ONE"

Image
 Baada ya tuhuma za kuiba wimbo wa H.Baba na Pasha,Msanii Naseeb Abdul Diamond Platnum, ameingia tena ndani ya tuhuma nzito  baada ya  madai   kwamba wimbo anaotaka kuuachia wa No.1 ni wa Dayna. Inasemekana awali Dayna alimtaka Diamond wakafanye wimbo kwa Shedy, Diamond akakubali, akaskiliza mdundo na kumuahidi Dayna kwamba wangefanya wote. Lakini baadae Diamond akamrubuni Shedy na kumwambia ile bit ampe na aachane na kazi ya Dayna. Hii ni demo ya wimbo wa Dayna ambao unafanana kila kitu na wimbo wa Diamond anaotaka kuachia.