NHIF YAZINDUA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA YA JAMII (CHF)MJINI KILWA

13_ab4bb.jpg
Adoh Mapunda Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa akipokea vifaa maalum vya kuhifadhia fedha na nyaraka mbalimbali kutoka kwa Balozi Ali Mchumo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati wa uzinduzi wa Huduma za Bimaya Afya (CHF)katika halmashauri hiyo uliofanyika jana kwenye viwanja vya Mkapa Garden Mjini Kilwa, wa pili kulia anayeshuhudia tukio hilo ni Kaimu Mkurugenzi wa (NHIF) Khamis Mdee na kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athuman Rehani na Fortunata Raymond Msimamizi wa NHIF mkoani Lindi.wananchi mbalimbali wakiwemo wazee walijitokeza katika zoezi la upimaji wa afya yakiwemo magonjwa ya Kisukari, Shinikizo la Damu ikiwani pamoja na kupima Uzito Urefu.

23_286be.jpg
Ado Mapunda Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za Bima ya Afya katika Halmashauri ya wilaya ya Kilwa jana kulia ni Bw. Khamis Mdee Kaimu Mkurugenzi NHIF na kushoto ni Dr. Hilda Mwakipesile kutoka NHIF.
43_5dab2.jpg
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya NHIF Balozi Ali Mchumo akipata huduma ya vipimo kutoka kwa mmoja wa madaktari wa NHIF jana anayeshuhudia ni mama Fatma Said Ali Mke wa Balozi Ali Mchumo

Comments

Popular posts from this blog