OZIL ATUA ARSENAL, FELLAINI AKIJIUNGA NA MAN UTD

Lukas Podolski (kulia) na Mesut Ozil (kushoto) katika pozi na jezi ya Arsenal nchini Ujerumani.
Mshambuliaji mpya wa Man Utd, Marouane Fellaini (kushoto) akikabidhiwa jezi na kocha wake David Moyes (kulia).
Marouane Fellaini ndani ya Manchester United.
-OZIL ATUA KWA KITITA CHA BILIONI  107, FELLAINI BILIONI 69.3
KLABU ya Arsenal imefanikiwa kumnasa kiungo wa Ujerumani, Mesuit Ozil kwa ada ya pauni milioni 42.5 sawa na bilioni 107 za Tanzania. Usajili wa Ozil umevunja rekodi katika klabu hiyo inayoongozwa na Mfaransa Arsene Wenger. Staa huyo wa Ujerumani aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano na atakuwa akilipwa  pauni 140,000 sawa na milioni 352.8 za Tanzania kwa wiki.
Wakati Arsenal wakimnasa Ozil katika dakika za mwisho za dirisha la usajili kufungwa, Manchester United wao wamefanikiwa kumnasa Mshambuliaji wa Everton, Marouane Fellaini kwa ada ya pauni milioni 27.5 sawa na bilioni 69.3 za Tanzania. Fellaini ameungana na kocha wake wa zamani David Moyes  anayeiongoza Man Utd kwa sasa.
Fellaini ameeleza kuwa amemfahamu Moyes kwa miaka mingi na anamheshimu sana katika ufundishaji wake na alipopata nafasi ya kufanya naye kazi kwa mara nyingine alichangamkia fursa.
Moyes yeye amesema kuwa amefanya kazi miaka mitano na Marouane na anamfahamu kama mchezaji mwenye uwezo mkubwa na imara. Pia ana matumaini makubwa na mshambuliaji huyo ya kwamba ataleta mabadiiko katika kikosi chake.

Comments

Popular posts from this blog